Halmashauri ziache kuwalazimisha Watumishi kuchangia Mwenge

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
667
1,795
Hii tabia ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwataka watumishi wa umma ndani ya Halmashauri imetoka wapi?

Yaani mkuu wa wilaya anaagiza wakuu wa idara kusimamia zoezi na kuomba majina ya wachangiaji, sasa hatujui wasiochangia wafanywaje.

Pia wakuu wa idara wamekuwa wakionywa endapo atashindwa kulazimisha watumishi wa idara yake watapokonywa madaraka.

Wanatumishi wa umma huwa wanajiuliza wizara ya TAMISEMI haina bajeti kwa ajili ya mwenge?

Mh Rais piga marufuku hiki kitu,kinakera na kuudhi watumishi wa umma,kama utaratibu huu upo wa kuchangia mwenge watumishi wawe wanakatwa asilimia fulani huko hazina kwa ajili ya mwenge lakini si hii tabia ya kushupalia kuchangia.
 
Serikali ya JMT, iwe inapanga bajeti ya kukimbiza mwenge wa Uhuru. Mfano, bajeti ya 2021/2022 ni Tsh 34 trillion hatuoni huko bajeti ya kukimbiza mwenge wa Uhuru.
 
Halmashauri za majiji, manispaa, miji, wilaya, na vijiji zinachangisha watumishi na wanachi baada ya kukubaliana kwenye vikao na mikutano yao.

Mwenge ni tunu na alama inayotambulisha nchi yetu. Makubaliano yakifikiwa ni ya wengi wape kame ilivyo ada kwenye vikao.

TUNAUPENDA MWENGE

UNAWAMRIKA WAZEMBE , WALA RUSHWA NA KUFICHUA MAOVU KWENYE MIRADI.
MWENGE HOYEEEEE

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 
Halmashauri za majiji, manispaa, miji, wilaya, na vijiji zinachangisha watumishi na wanachi baada ya kukubaliana kwenye vikao na mikutano yao.
Mwenge ni tunu na alama inayotambulisha nchi yetu.
Huo Mwenge si una bajeti yake.
 
Halmashauri za majiji, manispaa, miji, wilaya, na vijiji zinachangisha watumishi na wanachi baada ya kukubaliana kwenye vikao na mikutano yao.
Mwenge ni tunu na alama inayotambulisha nchi yetu.
Makubaliano yakifikiwa ni ya wengi wape kame ilivyo ada kwenye vikao.
TUNAUPENDA MWENGE
UNAWAMRIKA WAZEMBE , WALA RUSHWA NA KUFICHUA MAOVU KWENYE MIRADI.
MWENGE HOYEEEEE

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
Mwenge hauna maana yoyote,ile ni ibada ya sanamu tu
 
Hii tabia ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwataka watumishi wa umma ndani ya Halmashauri imetoka wapi?

Yaani mkuu wa wilaya anaagiza wakuu wa idara kusimamia zoezi na kuomba majina ya wachangiaji ,sasa hatujui wasiochangia wafanywaje....
Ukikataa utasikia mwenge utaondoka na mtu hapa ho hooo!
 
Wadau nimekuwa najiuliza huu Mwenge wa uhuru ni wa chama au serikali?

Kama ni wa chama ni CCM kwanini watumishi walazimishwe kuchangia na hawa wakurugenzi wa halmashauri wakati chama kina ruzuku kubwa bungeni?

Kama ni wa serikali kwanini wasitenge fedha ya bajeti kuhudumia Mwenge badala ya wakurugenzi wa halmashauri kuwalazimisha watumishi kuchangia?

Huu no uonevu wa hali ya juu wabunge wanalipwa mamilioni kwanini nao hawachangii kwenye majimbo yao ambayo huo Mwenge unapitia tunaomba watumishi tusilazimishwe.
 
Mnajitakia wenyewe kuchangia...

Puuzeni wito batili wa namna hiyo na endeleeni na shughuli zenu. Hakuna sheria yoyote mtakayokuwa mmevunja...

Mimi toka uanze sijawahi kuchangia hata 500 na ni mtumishi wa umma...

Açheni kutishwa na mkatishika. Acheni WOGA. Stand for your rights. Never get intimidated...!!
 
Hii tabia ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwataka watumishi wa umma ndani ya Halmashauri imetoka wapi?

Yaani mkuu wa wilaya anaagiza wakuu wa idara kusimamia zoezi na kuomba majina ya wachangiaji, sasa hatujui wasiochangia wafanywaje.

Pia wakuu wa idara wamekuwa wakionywa endapo atashindwa kulazimisha watumishi wa idara yake watapokonywa madaraka.

Wanatumishi wa umma huwa wanajiuliza wizara ya TAMISEMI haina bajeti kwa ajili ya mwenge?

Mh Rais piga marufuku hiki kitu,kinakera na kuudhi watumishi wa umma,kama utaratibu huu upo wa kuchangia mwenge watumishi wawe wanakatwa asilimia fulani huko hazina kwa ajili ya mwenge lakini si hii tabia ya kushupalia kuchangia

Moja ya mambo ya kijinga yanayonifanya niseme sitaki kufanya kazi Tamisemi ni hili.

Kuna mambo ya kijinga sana Tamisemi.

Kuliko nifanye kazi Tamisemi bora hata niwe askari polisi potelea mbali.
 
Back
Top Bottom