Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa wanatumbuana wenyewe majipu kabla hawajatumbuliwa

laurent Msembeyu

Senior Member
Oct 5, 2015
121
101
Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kumenuka, kila mtumishi wa halmashauri hiyo hamwamini mwenziwe kwa siku za hizi za karibuni, huii ulisini wewe , ulisaini wewe mimi sikuwepo ndiyo lugha inayotumika, pia simu mala nyingi zinakuwa zimefungwa.

HALI HALISI ILIVYO

Kuna madudu ya kutisha, jamaa wamepiga hela za serikali kama vile hawana akili nzuri, pia kama vile hela za ruzuku na makusanyo ya ushuru wa ndani hazina mwenyewe.
Kwa uchache sana:-
  • Daraja la kupitisha maji kwa chini la kitongoji cha ng`ambo ilitumika mifuko 14 ya cement, trip 2 za mawe na trip 2 za mchanga na trip 2 za changarawe, mafundi na vibarua hela iliyotumika ni shs, million 89( 89.000.000).
  • Kuhamisha makaburi Kata ya Mtera kijiji cha Chipogolo kupisha ujenzi wa barabara ya Dodoma/Iringa kwa kiwango cha lami, makaburi 54 wana ndugu walilipwa kati ya sh 30.000 na 50.000 hela iliyotumika ni sh 43.000.000/=
  • Ujenzi wa ukumbi wa mikutano ya halmashuri kama vile full council na mikutano mingine ilitengwa sh, 235,000.0000/=, ukumbi haujaisha, umeishia kwenye rental , mabati yaliyozungushiwa yameisha chukuliwa, cement ingine imeganda mkandarasi kaisha lipwa hela yote na hayupo ameisha kimbiya.
  • Ujenzi wa uzio wa kwenye nyumba ya mkuu wa wilaya hela iliyoyutumika ni sh 300,000.000 lakini fundi Miraji amelipwa shs 45,000.000/= tu.
  • Semina za kuelimisha kuhusu kupunguza maambukizi ya ukimwi vijiji vya Lukole na Kingiti na Kibakwe, attendance register za walengwa na payment voucher zimesainiwa ila hakuna mafunzo yaliyoisha fanyika hela iliyotumika ni sh 60.000.000/= walitia saini ya mahudhurio wahusika na hela wakajilipa wenyewe
  • Makusannyo ya ushuru wa ndani hela hazijulikani zilipo wala kazi zilizofanyika ila Siwajibu anazidi kununua magari
Madudu ni mengi mengi daraja la godegode, la gulwe n.k ndio maana wameanza kujitumbua wenyewe, wahusika wakija hawatapata shida kuwatumbua.
 
kumbuka gharama, za upembuzi yakinifu;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; ndo zinatugharimu
 
alisema kabla hajafika mkuu wa mkoa awe amefanya kazi yake, sasa akiacha yy ndo atatumbuliwa,mila nahisi amepata taarifa, na anazifanyia kazi
 
Rais wetu alishasema bayana kuwa huko Halmashauri kuna madudu kibao. Hiyo Halmashauri Moja tu je huko kwingine?
 
Ccm Inakwenda Kufa Na Kuzaliwa Chama Kipya Maana Yote Haya Ni Ccm Yenyewe Sasa Inajivua Gamba Taratibu.
 
Mpwapwa ni kama sikonge, pale napo panahitaji brush ya hatari
 
Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kumenuka, kila mtumishi wa halmashauri hiyo hamwamini mwenziwe kwa siku za hizi za karibuni, huii ulisini wewe , ulisaini wewe mimi sikuwepo ndiyo lugha inayotumika, pia simu mala nyingi zinakuwa zimefungwa.

HALI HALISI ILIVYO

Kuna madudu ya kutisha, jamaa wamepiga hela za serikali kama vile hawana akili nzuri, pia kama vile hela za ruzuku na makusanyo ya ushuru wa ndani hazina mwenyewe.
Kwa uchache sana:-
  • Daraja la kupitisha maji kwa chini la kitongoji cha ng`ambo ilitumika mifuko 14 ya cement, trip 2 za mawe na trip 2 za mchanga na trip 2 za changarawe, mafundi na vibarua hela iliyotumika ni shs, million 89( 89.000.000).
  • Kuhamisha makaburi Kata ya Mtera kijiji cha Chipogolo kupisha ujenzi wa barabara ya Dodoma/Iringa kwa kiwango cha lami, makaburi 54 wana ndugu walilipwa kati ya sh 30.000 na 50.000 hela iliyotumika ni sh 43.000.000/=
  • Ujenzi wa ukumbi wa mikutano ya halmashuri kama vile full council na mikutano mingine ilitengwa sh, 235,000.0000/=, ukumbi haujaisha, umeishia kwenye rental , mabati yaliyozungushiwa yameisha chukuliwa, cement ingine imeganda mkandarasi kaisha lipwa hela yote na hayupo ameisha kimbiya.
  • Ujenzi wa uzio wa kwenye nyumba ya mkuu wa wilaya hela iliyoyutumika ni sh 300,000.000 lakini fundi Miraji amelipwa shs 45,000.000/= tu.
  • Semina za kuelimisha kuhusu kupunguza maambukizi ya ukimwi vijiji vya Lukole na Kingiti na Kibakwe, attendance register za walengwa na payment voucher zimesainiwa ila hakuna mafunzo yaliyoisha fanyika hela iliyotumika ni sh 60.000.000/= walitia saini ya mahudhurio wahusika na hela wakajilipa wenyewe
  • Makusannyo ya ushuru wa ndani hela hazijulikani zilipo wala kazi zilizofanyika ila Siwajibu anazidi kununua magari
Madudu ni mengi mengi daraja la godegode, la gulwe n.k ndio maana wameanza kujitumbua wenyewe, wahusika wakija hawatapata shida kuwatumbua.

Kama haya yaliyoandikwa ni ya kweli: Yafuatayo yafanyike:

DC aliyekuwepo ni lazima achukuliwe hatua. Najua siyo kazi yake lakini ni wazi madudu haya kufanyika wilayani kwake ni kashfa na ni lazima kwa namna moja ama nyingine baadhi ya fedha alikula kutoka halmashauri.

Mkurugenzi wa Halmashauri lazima aende na maji na kufikishwa mahakamani

Mhasibu Mkuu wa halmashauri ni lazima naye afikishwe mahakamani

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa halmashauri ni lazima afikishwe mahakamani

DAS naye ni lazima aende na maji

Mkuu wa utawala wa Halmashauri ni lazima afikishwe mahakamani

wakaguzi waliofanya ukaguzi na kupitisha malipo wafikishwe mahakamani

Cashier wa Halmashauri ni lazima afikishwe mahakamani

Wahasibu waliosaini vouchers ni lazima wafikishwe mahakamani

Wahusika walioandika dokezo la malipo iwe ni UTAWALA, Ustawi, ujenzi ni lazima nao wafikishwe mahakamani

NB: Kesi zote zisichukue zaidi ya miezi mitatu. hakimu na polisi na waendesha mashtaka na takukuru watakaochelewesha waachishwe kazi.
 
Eti wana ccm nao wana shangaa wakati walikuwa wanajitapa ndio chama kinacho ongoza nchi kwa misingi ya haki na uzalendo! unafik mbaya sana........yote haya walaaniwe ccm tena haswa mwenyekiti wao ndio wa kubebeshwa msalaba wa chuma
 
Halmashauri ya wilaya ya mpwapwa binafsi niseme ni halmashauri yenye madudu kuliko halmashauri yeyote tanzania sema haijamulikwa na sijui ni kwa nini mfano hapa kata ya mtera miaka kumi(10)iliyopita tuliambiwa world bank imetoa sh milioni mia sita(6) kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji ambao ungetumiwa na vitongoji vinne yaani hapa kisima yenyewe,chungu ,kibwegele,msangambuya na kilimbe na fedha imeshatoka lakini kwa sharti kwamba na sisi tuchange sio chini ya milion 15 kwahiyo ukawekwa utaratibu ng'ombe mmoja 1500/-,nguruwe 1000/-,mbuzi na kondoo sh 500/-mpaka tarehe 6-11-2010 pesa tulizochanga wananchi ilikuwa sh. milioni5 na laki 2 na michango iliendelea cha ajabu mpaka leo hakuna mradi wa milioni mia sita(6) uliofika hapa kijiji cha kisima na hakuna maelezo yeyote hata ya pesa tulizochanga yaani ni uhuni wa mchana kweupe,pili kuna mjapani alijitolea shilingi milion 115 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na kwa sharti kwamba halmashauri mpwapwa itoe sh mil 54 kwa mujibu wa mkataba ule lakini tunaenda mwaka wa 15 huu bweni halijaisha na halijaanza kutumika kwani halijakamilika kwakweli kunahitajika nguvu kubwa ya ziada kuimulika halmashauri ya mpwapwa ususani jimbo la kibakwe la mh george simbachawene.
 
mh simbachawene waziri wa tamisemi hujuma jimboni kwako hizo na lazima unazifahamu na rungu unalo
 
Hii safii, kulikuwa na uzushi kuwa mleta mada ulikufa kumbe walikuwa wanakutabiria vibaya ili usilete ubuyu jamvini.

Tumekuelewa mzee, kumbe upo hai tuletee vitu
 
Kama haya yaliyoandikwa ni ya kweli: Yafuatayo yafanyike:

DC aliyekuwepo ni lazima achukuliwe hatua. Najua siyo kazi yake lakini ni wazi madudu haya kufanyika wilayani kwake ni kashfa na ni lazima kwa namna moja ama nyingine baadhi ya fedha alikula kutoka halmashauri.

Mkurugenzi wa Halmashauri lazima aende na maji na kufikishwa mahakamani

Mhasibu Mkuu wa halmashauri ni lazima naye afikishwe mahakamani

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa halmashauri ni lazima afikishwe mahakamani

DAS naye ni lazima aende na maji

Mkuu wa utawala wa Halmashauri ni lazima afikishwe mahakamani

wakaguzi waliofanya ukaguzi na kupitisha malipo wafikishwe mahakamani

Cashier wa Halmashauri ni lazima afikishwe mahakamani

Wahasibu waliosaini vouchers ni lazima wafikishwe mahakamani

Wahusika walioandika dokezo la malipo iwe ni UTAWALA, Ustawi, ujenzi ni lazima nao wafikishwe mahakamani

NB: Kesi zote zisichukue zaidi ya miezi mitatu. hakimu na polisi na waendesha mashtaka na takukuru watakaochelewesha waachishwe kazi.
Au wewe ni JPM katika koti la 1954? Sawa mh.watakuwa wamekupata
 
Halmashauri ya wilaya ya mpwapwa binafsi niseme ni halmashauri yenye madudu kuliko halmashauri yeyote tanzania sema haijamulikwa na sijui ni kwa nini mfano hapa kata ya mtera miaka kumi(10)iliyopita tuliambiwa world bank imetoa sh milioni mia sita(6) kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji ambao ungetumiwa na vitongoji vinne yaani hapa kisima yenyewe,chungu ,kibwegele,msangambuya na kilimbe na fedha imeshatoka lakini kwa sharti kwamba na sisi tuchange sio chini ya milion 15 kwahiyo ukawekwa utaratibu ng'ombe mmoja 1500/-,nguruwe 1000/-,mbuzi na kondoo sh 500/-mpaka tarehe 6-11-2010 pesa tulizochanga wananchi ilikuwa sh. milioni5 na laki 2 na michango iliendelea cha ajabu mpaka leo hakuna mradi wa milioni mia sita(6) uliofika hapa kijiji cha kisima na hakuna maelezo yeyote hata ya pesa tulizochanga yaani ni uhuni wa mchana kweupe,pili kuna mjapani alijitolea shilingi milion 115 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na kwa sharti kwamba halmashauri mpwapwa itoe sh mil 54 kwa mujibu wa mkataba ule lakini tunaenda mwaka wa 15 huu bweni halijaisha na halijaanza kutumika kwani halijakamilika kwakweli kunahitajika nguvu kubwa ya ziada kuimulika halmashauri ya mpwapwa ususani jimbo la kibakwe la mh george simbachawene.
Hivi huyu Simbachawene ni diwani wa halmashauri gani?
 
halmashauri ya mpwapwa.
Ngoja tusubiri unafiki wake, jamaa Simbachawene, kama sikosei amekuwa mbunge wa eneo hilo (hio halmashauri), kwa awamu ya tatu sasa kama siyo 4, ina maana amekuwa akishuhudia hayo madudu au na yeye ni mnufaika? Sasa kwa kuwa ni Waziri wa TAMISEMI I hope atawapiga mkwara wa kinafiki ama ataogopa kuwagusa ili asijiharibie
 
swala hili kushughurikiwa na simbachawene ni sawa na kumwambia mama anna kilango apeleke ripoti ya wafanyakazi hewa mkoa wa shinyanga kwa mh JPM
 
Back
Top Bottom