Halmashauri ya Temeke jitokezeni muwape ufafanuzi juu ya utwaaji ardhi unaonekana ni wa kiholela unaondelea kwa baadhi ya maeneo

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau..!
Napita pita zangu baadhi ya mitaa ya Temeke,Chang'ombe,Vetenary,Keko kote huko kuna harakati za watu kuhamishwa makazi yao wengine wanavunja nyumba zao wanakubali kupokea pesa kidogo kutoka kwa watu wanaozaniwa wawekezaji pia kuna baadhi ya watu wanawatisha wenyeji wenye nyumba zao bora wakubali hiyo pesa la sivyo wanaweza kubomolewa nyumba zao na Halmashauri na wasilipw hata shilingi moja kwa kuwa ni makazi holela.

Cha ajabu hakuna kiongozi yeyote aliyejitikeza kuwapa watu ufafanuzi na kuwapa elimu kuhusu haki na wajibu wao kisheria ,hii inasikitisha sana
Nashauri Halmashauri wajitokeze watu wanaumizwa wengine wana msogo wa mawazo kwa nn nyinyi wau wa ardhi na Halmashauri amuonekani.

Jana kuna watu wamekaa kikao na mtu mmoja ambaye ni mwananchi wa kawaida tu akiwaambia eneo lao linahitajika na wawekezaji,wazee wameogoma wanasema wanahitaji kuongea na muwekezaji hawataki kuburuzwa ina maana baadhi ya maeneo watu wameburuzwa na wanaendelea kubuuruzwa .

Wapo watu wanaunda kamati ili wapige mpunga kwa kila nyumba inayobomolewa mtu anadai alipe pesa kamati ,hii sio sawa kabisa .Haki yako mtu anataka umlipe.

Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa wilaya tunaomba ufuatilie na utoe neno kwa maeneo husika wananchi wanataka kusikia kauli zenu ,mnawaweka wakati mgumu sio mnakaa tu kimya haisaidii kuna wananchi wanaambiwa pesa inalipwa kwa square meter masikini hata square meter hawazijui si ndioo kupigwa huko
 
Back
Top Bottom