Halmashauri ya Nzega inaongozwa na CCM, kwanini wafanyabiashara wamegoma?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,058
Wakati sehemu nyingine watu wakijipiga vifua kumuunga mkono Rais Magufuli, jimbo LA Nzega mjini linaloongozwa Mhe.Hussein Bashe WAFANYABIASHARA wamegoma Leo na kufunga maduka huku wakidai kuweka mgomo mpaka jumatatu.

Hatua hii imeleta sintofahamu kubwa na kuwafanya RAIA kukosa Huduma muhimu za kila siku.

Tukio hiki linakuja wakati ambapo wajasiriamali wengi wakiwa wamefunga biashara zao kutokana na kudorora kwa biashara.

Mgomo huo unaelezwa kuchagizwa na ubabe wa mkurugenzi wa Mji wa Nzega. Inadaiwa kuwa Mkurugenzi anawalazimisha WAFANYABIASHARA kukabidhi vibanda vyao vya biashara kwa halmashauri bila fidia yoyote wakati vibanda hiyo vilijengwa na walalahoi bila serikali kuchangia katika eneo LA soko kuu miaka kadhaa iliyopita.

Hii inaelezwa na wadadisi wa mambo ya uchumi mdogo kwamba ni matokeo ya serikali kushindwa kufanya maamuzi kwa weledi badala yake hutumia ubabe jambo ambalo linaathiri vipato vya watu na kuzidisha idadi ya masikini hohehahe.
Nini mtazamo wako katika hili?
IMG_20170812_154811.jpg
IMG_20170812_154721_1.jpg
IMG_20170812_154721.jpg


Kwa Hisani Ya Watu Wa Mbeya!
 
SHAURI YAO HAO WANANCHI.WATAPELEKEWA MAABARA KUPIMWA MKOJO WILAYA NZIMA
 
Back
Top Bottom