mchimbadhahabutz
Member
- Oct 15, 2016
- 56
- 49
Katika kile wanachokiita halmashauri kubuni vyanzo vya mapato, msalala imepitisha na kuamulu kila mtumishi wa kwenye mgahawa na mama lishe na bar med kupima Virusi Vya Ukimwi (V.V.U) kwa kulipia sh. 10000 kwa kila mfanyakazi wa bar, mgahawa au hoteli.
Matangazo hayo yanaendelea kutangazwa katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo hasa katika kata ya BULYANHULU ikiwemo kijiji cha KAKOLA NA BUSHINGWE. "Ni lazima kila mfanyakazi wapimwe na ikibainika anafanya kazi bila kupimwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mmiliki na mfanyakazi huyo" alisisitiza mtangazaji aliyekua akipita kila kona ya kata hiyo.
Swali langu kwa asasi na wadau tofauti tofauti ni je suala la kupima V.V.U limekua ni lazima? na je lengoni kukusanya fedha tu ama unsaidiaje mtu anayegundulika na V.V.U?
Binafsi nadhani ukurupukaji umefanyika kwa kulazimisha watu ili tu halmashauri ipate pesa maana kama kweli pangekua na nia njema huduma hii ingetolewa bure na kwa utashi wa mtu.
Ujumbe uwafikie wahusika wote!