Halmashauri ya mji wa Moshi yatimua wapiga debe

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
4,915
2,452
Katika hali ya kusikitisha ,halmshauri ya mji wa Moshi inayoonngozwa na chadema wameamua kwa makusudi kabisa kuwafukuza wapiga debe wote katika kituo cha mabasi ya abiria waendao mikoani na pembezoni mwa mji.Uamuzi huu ni wa ajabu sana haswa ukizingatia ya kwamba vijana zaidi ya mia moja wataathirika na uamuzi huu wa ajabu kabisa
 
Kama ni kweli hilo limefanyika, basi ni hatua nzuri kwa mustakabali wa Taifa! Binafsi sikubaliani na dhana ya "Upiga debe"! Vijana wanaitwa ni "nguvu kazi ya Taifa", hivyo wanapaswa wajishughulishe na shughuli za uzalishaji na sio "kupiga debe stendi"!!! Makampuni ya usafirishaji yanapaswa yawe na ofisi zinazoeleweka! Ustaarabu hujengwa na una gharama zake!
 
Katika hali ya kusikitisha ,halmshauri ya mji wa Moshi inayoonngozwa na chadema wameamua kwa makusudi kabisa kuwafukuza wapiga debe wote katika kituo cha mabasi ya abiria waendao mikoani na pembezoni mwa mji.Uamuzi huu ni wa ajabu sana haswa ukizingatia ya kwamba vijana zaidi ya mia moja wataathirika na uamuzi huu wa ajabu kabisa

Mbona ikikaribia uchaguzi chadema ndio wa kwanza kuwapa hawa vijana skafu; bendera na kuwanunulia viroba. Au kipindi hicho hamuwatambui kama wapiga debe?
 
Kwa moshi sishangai maana hawaangalii chama wanaangalia muongozo wa kusonga mbele kimaendeleo, usafi nk. Mimi kwa wanaofiatilia post au coments zangu atanipata vyema.

Aliyeleta mada ni mwanachadema kwa mtazamo wangu akijidai ccm kumbe ukweli hiyk ndiyo sera ya ccm kwa muda mrefu. Vijana wafanye kazi siyo kubangaiza. Vijana wengi moshi wanakula msuba, viroba na kudukua mifuko ya wenzao.

Nawapongeza wanahalmashauri ya moshi wala msivimjwe moyo na wachokonozi, vijana wapiga debe hata kura huwa hawapigi ila ni chambo kizuri kwenye maandamano maana hawana cha kupoteza.

Nakumbuka John Mnyika aliwapa kichwa sana wapiga debe wa ubungo lakini naamini natamrudia siku chadema ikichukua nchi. Nawasihi wanamoshi wawaunge mkono viongozi wao bila kujali interest za vyama maana moshi ni yenu si ya chama fulani. TANU haipo ila Tanzania ipo. Vivyohivyo vyama vya sasa vitapita ila Moshi na Tanzania ipo pale pale
 
Ninawapa hongera Hao halmashauri ya Moshi wengine wajifunze kutoka kwao, alafu wacha uchonganishi mbona wamefanya kitu kizuri au haujui usumbufu wa hao wapiga debe
 
Katika hali ya kusikitisha ,halmshauri ya mji wa Moshi inayoonngozwa na chadema wameamua kwa makusudi kabisa kuwafukuza wapiga debe wote katika kituo cha mabasi ya abiria waendao mikoani na pembezoni mwa mji.Uamuzi huu ni wa ajabu sana haswa ukizingatia ya kwamba vijana zaidi ya mia moja wataathirika na uamuzi huu wa ajabu kabisa

Kuna kitu unataka kutuambia lkn unakwepesha, hebu tuambie nyie CCM ndiyo mnalea wale wapiga debe pale ubungo? Kule kinondoni, mwenge, tandika n.k
Na kusema kwamba mmewapatia ajira??
Au ndiyo ajira 1000 za Mr. Dhaifu?
 
Katika hali ya kusikitisha
,halmshauri ya mji wa Moshi inayoonngozwa na chadema wameamua kwa
makusudi kabisa kuwafukuza wapiga debe wote katika kituo cha mabasi ya
abiria waendao mikoani na pembezoni mwa mji.Uamuzi huu ni wa ajabu sana
haswa ukizingatia ya kwamba vijana zaidi ya mia moja wataathirika na
uamuzi huu wa ajabu kabisa

Tatizo ni chadma au wapga debe. uliepost uzi huu yamkin hujui ulichosema. zoez gil lintakiwa liwe nchi nzima kwan wamekuwa kero na ndo chanzo cha wiz na kupanda nauli kiholela. nawapongeza wana moshi. kaz nzuri
 
Hongera hivi wapiga debe wanafaida gani zaid ya kuongeza wezi na vurugu stend? kwakwel nimekaa mosh kwa muda mrefu kwel wapga debe wa magar ya arusha n kero
 
HAKUNA watu wananiboa stand yoyote hapa Tanzania kama wapiga debe. Basi tu ni kutokana na udhaifu wa viongozi wa ccm na serikali yao hii. Hawa wapiga debe ilitakiwa wawe wanakamatwa na kuswekwa rockup,halafu vinashuka viboko vya maana kwenye ------ yao,mbona wangeenda kufanya kazi tu hata mashambani,maana hao ndiyo nguvu kazi yenye. Wanashnda stand wakiwa wanavuta bange na kupora wapita njia. Hongereni Moshi,Miji mingine uongozi uige katka hilo.
 
Katika hali ya kusikitisha ,halmshauri ya mji wa Moshi inayoonngozwa na chadema wameamua kwa makusudi kabisa kuwafukuza wapiga debe wote katika kituo cha mabasi ya abiria waendao mikoani na pembezoni mwa mji.Uamuzi huu ni wa ajabu sana haswa ukizingatia ya kwamba vijana zaidi ya mia moja wataathirika na uamuzi huu wa ajabu kabisa

Wakabebe ndizi kutoka Uru kishimundu waje wauze mjini. Waache kuwaibia abiria!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom