Halmashauri ya Mbozi Kitengo cha Utumishi pameoza pananuka rushwa

Ibanda1

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
705
1,092
Wasalaam wanajamvi,

Halmashauri ya Mbozi inapatikana katika mkoa mpya wa Songwe na ni moja kati ya HJalmashauri kongwe sana lakini pia Wilaya ya Mbozi imejizolea umaarufu kutokana na uwepo wa kimondo ambapo tulikuwa tukiisoma tangu shule ya msingi.

Niende kwenye hoja moja kwa moja, katika ofisi za halmashauri ya Mbozi idara ya utumishi pamekuwa na watumishi wasio waadilifu wapenda rushwa na wanajisifu kuwa ukiwa na mkono mfupi utaishia kupigwa kalenda.

Kuna utaratibu wa taasisi za fedha kwenda kuingiza makato ya mikopo ya waajiri kupitia mfumo wa Lawson, kiutaratibu bank officer kazi yake ni kwenda kuthibitisha kama makato yameingizwa kwa usahihi lakini katika hali ya kushangaza hawa maafisa utumishi wamejitengenezea mradi wa kujipatia fedha kwa njia isiyo rasmi kwani bank officer ukienda kufanya capturing kama hujawapatia pesa utazungushwa hata mwezi mzima huku ukiambiwa network hamna ila wanaingia watu wa benki nyingine, kazi wanawahudumia baada ya kuwapa rushwa tena wanajipangia kiasi kabisa wanahitaji elfu hamsini aisee imagine una application moja tu ya mteja haizidi hata million tano na umesafiri kutoka Tunduma alafu mtu anakuomba rushwa ya 50k?

Kibaya zaidi DED pamoja DHRO wanafahamu huu uozo wa hawa watumishi ila wanawafumbia macho, huu mchezo mmeucheza kwa muda mrefu nadhani mnatakiwa kuuacha mara moja la sivyo mtapoteza kazi kwa sababu ya elfu hamsini.
 
Kama mmechoshwa na huo upuuzi na mnajua upo na una mizizi so mchomeshe afisa utumishi mmoja TAKUKURU ili akili ziwakae sawa waache ujinga
 
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua. Nimejipa Kazi Ya Mtumbua Jipu.

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
So mbozi tu. Halmashauri nyingi nchini bank officer wenyewe wamejenga upuuzi Wa kutoa tena ni 10elf tu. Nmb,posta,crdb,na BoaT nimejiridhisha 100percent
Alafu hawa jamaa sijui wakoje hata huku ni hao hao wanaendekeza huu upuuzi na kinachowapa kiburi ni customer base kubwa waliyonayo lakini hata mifumo yao ya kibenk imejaa rushwa kwa hiyo hawashtushwi na hili jambo...let say wao wanapeleka loan application 20 kwa siku hivyo wanaona 50k si chochote ila kimbembe sie wengine yani uko na application moja na wanahitaji rushwa pia.

Sent from my SM-J320F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom