Halmashauri ya Kishapu kuhakiki kadi za benki za watumishi wake. Je, kadi hizo ni mali ya Serikali au mtu binafsi?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
kioja.jpg
 
Kwavile Watanzania wengi ni kama misukule tu; sina shaka watumishi watatii agizo hilo bila kuhoji! Kadi ya benki ni mali ya mwenye kadi na wala sio mali ya mwajiri! Sasa kwanini wanalazimisha kukagua kadi za watumishi?! Of course, ni mwajiri ndie kaingia mkataba na benki ili mishahara ya watumishi wake ipitie benki husika! Sasa kama lengo ni kuhakiki akaunti, kwanini mwajiri asipeleke updated payroll bank ili hatimae na wenyewe (bank) wa-update the payroll?

Labda uelewa wangu ni mdogo! Hivi kuna anayeweza kunielewesha uhalali na umuhimu wa hilo zoezi?! Wanataka kuhakiki ATM Card against nini?! Kama lengo ni kufahamu idadi ya wafanyakazi halali, ina maana halmashauri haiwaamini wakuu mbalimbali walipo kwenye taasisi zake?! Hawa si ndio wanatakiwa kuwasilisha majina ya wafanyakazi waliopo kwenye taasisi zao?!
 
tarehe 22/05
njoo uchukue kadi yako. uirudishe tare 23/05 ukitoka kuhakikiwa.


mshahara unatoka kabla ya tare 23/05 tunakuwa tushachota madeni yetu.


fanyeni hivi:
ombeni video za nani anachukua pesa kwwnye akaunti
 
ATM card ina namba ambazo mtaalamu asiyemuaminifu akizifahamu tu pesa yako ni rahisi kuibiwa, ATM card ni mali ya mtu Binafsi sio ya umma.

Kwanini baadhi ya halmashauri zinaendesha zoezi hili? Haya Mambo yanaanzaga hivihivi mwishowe yanakuwa kwa watumishi wote, lengo lake ni nini?
FB_IMG_1558168204503.jpeg
 
Lengo lao wajue account yako Ina shilingi ngapi walambeKama beure de change
ATM card ina namba ambazo mtaalamu asiyemuaminifu akizifahamu tu pesa yako ni rahisi kuibiwa, ATM card ni mali ya mtu Binafsi sio ya umma.

Kwanini baadhi ya halmashauri zinaendesha zoezi hili? Haya Mambo yanaanzaga hivihivi mwishowe yanakuwa kwa watumishi wote, lengo lake ni nini?View attachment 1101141
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom