Halmashauri ya Jiji la Arusha yasaini Mkataba wa Bilioni 1.3

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
HALMASHAURI ya jiji la Arusha imetiliana saini mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 na Kampuni ya Ujenzi ya BQ Constractors limited ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya mama na mtoto itakayojengwa kwenye hospital ya wilaya iliyopo eneo la Engutoto,Jijini Arusha.

Hafla hiyo imetiwa saini leo baina ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha,Dakta Maulid Madeni,Mstahiki meya wa jiji la Arusha Karisti Lazaro na Mtendaji mkuu wa kampuni ya ujenzi ya BQ ,Mhandisi John Bura, kwenye ukumbi wa halmashauri ya jiji la Arusha na kushuhudiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro.

Akizungumza mara baada ya utiwaji saini ,Kaimu mhandisi wa jiji la Arusha, Samweli Mshuza, amesema jengo hilo ambalo ujenzi wake unatakiwa kuanza leo , utachua muda wa miezi saba na litakuwa na ukubwa wa ghorofa moja.

Amesema ujenzi wa jengo hilo ni mwendelezo wa ujenzi wa majengo ya hospital hiyo ya wilaya ambapo tayari jengo la wagonjwa wa nje OPD, lenye ghorofa moja limeshakamilika na sasa linatoa huduma ya chanjo.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ya BQ ,Mhandisi John Bura, amewahakikishia viongozi wa serikali kuwa ujenzi huo utakamilika ndani ya muda na anatarajia kukabidhi jengo hilo mapema January mwakani.

Nae mkuu wa wilaya ya Arusha , Gabriel Daqaro, amesema,ujenzi wa hospital hiyo utapunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaopata huduma kwenye hospital ya mkoa ya Mount Meru.

Amesema upatikanaji wa dawa kwenye hospital za serikali, Vituo vya afya Zanati katika wilaya ya Arusha ni asilimia 98%.

Amesema majengo mengine yataendelea kujengwa kulingana na upatikanaji wa fedha na tayari huduma zingine zimeshaanza kutolewa kwenye jengo ambalo limeshakamilika .

Daqaro ,amesema hiyo ni historia tangia Uhuru wilaya ya Arusha ilikuwa haina hospital ya wilaya na pia kwenye mipango iliyopo ni kujenga kituo cha Afya kata ya Olasti.

Mkuu wa wilaya ameongeza kuwa muda hautaongezwa hivyo mkandarasi huyo ahakikishe anakamilisha ujenzi ndani ya muda uliowekwa.

Kwa upande wake mstafiki Meya wa jiji la Arusha Karisti Lazaro, amesema ujenzi huo unafanywa kwa fedha za ndani na akatoa wito kwa wananchi kuendelea kulipa ushuru na kodi mbalimbali kwa kuwa manufaa yanaonekana.

Amesema kuwa atahakikisha jengo hilo linakamilika na hivyo kuweka historia ya kuwa Meya wa awamu ya Tano ambaye Hospital ya wilaya inajengwa




IMG_20190624_112455.jpeg
IMG_20190624_114757.jpeg
IMG_20190624_111857.jpeg
IMG_20190624_120741.jpeg
 
Back
Top Bottom