Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kushirikiana na wadau wapanda miti 360 kata ya Muriet

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Halmashauri ya jiji la Arusha kupitia ofisi ya mazingira na utalii imepanda miti 3600 katika kata ya Muriet katika mitaa 13 kwa kushirikiana na wadau wa mazingira kutoka Tanzania Chember of commerce na Trias zote za jijini Arusha

Akizungumza wakati wa kukabithi miti hiyo kwa viongozi wa mitaa hiyo, Afisa mazingira na utalii wa jiji la Arusha Maiko Ndaisaba, amesema lengo la kupanda miti hiyo ni kutunza mazingira na kuvutia utalii katika kata hiyo .

Amesema kuwa, jiji la Arusha baadhi ya kata zake zimezungukwa na miti ya kivutio lakini kata hiyo imekuwa na changamoto kubwa ya upandaji wa miti ikilinganishwa na kata zingine ambazo zimekuwa kivutio kwa watalii wanaofika kutembelea mkoa wa Arusha.

Amewaomba wananchi kupitia viongozi wa kata na mitaa kusimamia vyema zoezi hilo la upandaji wa miti ambapo wananchi zaidi ya 1000 kutoka kila mtaa watapata miti miwili ya kupanda na baada ya mwezi moja watafika kutembelea kuona maendeleo ya miti hiyo na utunzaji wake.

"kabla ya hapo wananchi walipatiwa semina ya upandaji wa miti kupitia ofisi ya mazingira jiji la Arusha na namna ya kutunza na kusaidia kutunza mazingira hayo na zoezi hili ni endelevu."alisema .

Wakizungumza mara baada ya kupata miti hiyo viongozi wa serikali Mwenyekiti wa serikali ya mtaa,Frank Mollel ameshukuru halmashauri ya jiji la Arusha pamoja na serikali kuu kwa ujumla kwa kuwapatia miti 360 pamoja na mafunzo ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira .

Mollel amesema kata ya muriet na mitaa ilikuwa ni jangwa kwa muda mrefu, lakini kwa sasa wananchi watapata kivuli na vivutio vya utalii Mara baada ya kuhamasika kupanda miti hiyo yenye kuleta mvuto kwa watalii pamoja na kuboresha mazingira.

Baadhi ya wananchi wa Muriet,Miraji amesema wamepokea zoezi la upandaji wa miti kwa furaha kwani muda mwingi kata imekuwa kama jangwa kwa kukosa miti ya kivuli na kupendezesha mazingira na kuwa na mvuto.

Kwa upande wake Mdau wa mazingira kutoka chama cha wafanya biashara Mkoa wa Arusha ambao wamefanikisha zoezi hilo Sia Marunda amesema katika vikao vilivyo pita walikubaliana na wadau wa utalii na masoko kupanda miti na kuboresha mazingira ya jiji la Arusha kuwa ya kijani na kupambana na tabia ya mabadilko ya tabia ya nchi .

Sia amesema jiji la Arusha pamoja na Mkoa kwa ujumla unaendesha kampeni kwa kushirikiana na wadau wa mazingira na utalii wa masoko kuboresha vivutio kwa kupanda miti pamoja na kuhamasisha wananchi kuacha kukata miti hovyo bila kufuata taratibu za uvunaji wa miti ulio wekwa na mamlaka husika.

Mwisho.

IMG_8326.JPG
IMG_8358.JPG
IMG_8317.JPG
IMG_8335.JPG
 
Back
Top Bottom