Halmashauri ya Ilala indaendesha wizi wa maeneo ya wananchi wa Kinyerezi

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Katika mpango wa upimaji wa maeneo ya makazi ya mji katika sehemu ya Kinyerezi, halmashauri ya Ilala imekamilisha mpango wake wa kuwanyanganya wananchi wanyonge ardhi yao kwa lengo la kujipatia kipato kikubwa.

Haiwezekani kwa kiwanja cha chini ya sq m 1600 mwenye kiwanja akitaka kubakia na kiwanja chake basi anatakiwa kuwalipa halimashauri ya ilala zaidi ya shs mil 8 lakini halmashauri hiyo hiyo ikichukua kiwanja hicho toka kwa mwenye kiwanja kutaka kumlipa fidia ya wastani wa laki tatu.

Daima wanchi walizoea kutapeliwa na watu binafsi lakini kitendo cha serikali kuanza kutapeli wananchi wake wa kinyerezi ni tukio jipya na la kushangaza sana.
 
Kimantiki ni kwamba kama bei la soko la ardhi ni Tshs. 10,000/sq meter wanatakiwa walipwe kiasi hicho. Lakini pia kuna gharama za kupima nazo zinatakiwa ziangaliwe. Pamoja na hayo yote lakini kumeibuka na unyang'anyi wa ardhi ya wananchi.

Nendeni mahakama.
 
Kimantiki ni kwamba kama bei la soko la ardhi ni Tshs. 10,000/sq meter wanatakiwa walipwe kiasi hicho. Lakini pia kuna gharama za kupima nazo zinatakiwa ziangaliwe. Pamoja na hayo yote lakini kumeibuka na unyang'anyi wa ardhi ya wananchi.

Nendeni mahakama.

Nakubaliana nawewe kwamba kuna gharama za upimaji lakini sidhani kwa mradi mkubwa kama ule gharama hizo zifike zaidi ya mil 5 kwa kiwanja kimoja wakati fidia ikiwa chini kiasi kile. lazima kuwe na utaratibu wa kuwahusisha wenyeji kwani zoezi la upimaji wa miji linatakiwa kuwanufaisha wenyeji na si kuwafanya masikini
 
Back
Top Bottom