proff g
Senior Member
- Jul 16, 2016
- 113
- 55
Katika mwaka huu wa masomo 2020 serikali imejitahidi kuleta fedha kwa ajili ya maendeleo hasa maboresho katika miundombinu ya shule pamoja na kujenga miundo mbinu mipya ya shule hizi hasa za Halmashauri ya wilaya ya Bunda. changamoto iliyopo, pamoja nakuletwa fedha hizi bado halmashauri imeshindwa kutoa ushauri kwenye matumizi ya fedha hizi kwa mfano ipo shule x iliyo ingiziwa kiasi cha sh milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni. chakushangaza shule hii haina maabara, haina maktaba madarasa ya kujifunzia hayatoshi, walimu hawana meza na viti vya kukalia. Ombi langu mkuregenzi wa Halmashauri ya wilaya Bunda pitieni upya mahitaji ya msingi ya shule hizi kwasababu kuto kukamilishwa kwa mahitaji haya shule hizi zimekuwa na maendeleo hafifu ya kitaaluma.