Halmashauri wanataka kunipeleka mahakamani Naomba ushauri wa kisheria

Tibalikwenda

JF-Expert Member
Aug 27, 2020
285
595
Mimi ni afisa wa serikali wilaya x nililipa pesa mbichi kwa watumishi 3 baada ya kukusanya Mapato ya minada ya mifugo wilaya x jumla y fedha tsh.2,500,000/:

Ninadaiwa kwenye poss machine yangu mm nimekataa kuzilipa Mana zimetumika kwa idhini ya mkurugenzi sasa nimeamriwa na pccb nilipe la sivyo nipelekwe mahakamani kwa kosa la kutumia fedha ya serikali sasa naombeni ushauri wenu je Hawa pccb nitawashinda mahakaman au watanishinda?
 
Mi ni afisa wa serikali wilaya x nililipa pesa mbichi kwa watumishi 3 baada ya kukusanya Mapato ya minada ya mifugo wilaya x jumla y fedha tsh.2,500,000/: ninadaiwa kwenye poss machine yangu mm nimekataa kuzilipa Mana zimetumika kwa idhini ya mkurugenzi sasa nimeamriwa na pccb nilipe la sivyo nipelekwe mahakamani kwa kosa la kutumia fedha ya serikali sasa naombeni ushauri wenu je Hawa pccb nitawashinda mahakaman au watanishinda?
Acha uhuni, ulikusanya mil na laki tano. Ni fedha za serikali huwa zinaingia kwenye akaunti ya serikali. Kama zilitumika wewe unahusika vipi? Kuna viashiria ulikuwa unatoa control namba lakini hutoi risiti za serikali. Kaa mkao wa kupigwa mvua.
 
Mi ni afisa wa serikali wilaya x nililipa pesa mbichi kwa watumishi 3 baada ya kukusanya Mapato ya minada ya mifugo wilaya x jumla y fedha tsh.2,500,000/: ninadaiwa kwenye poss machine yangu mm nimekataa kuzilipa Mana zimetumika kwa idhini ya mkurugenzi sasa nimeamriwa na pccb nilipe la sivyo nipelekwe mahakamani kwa kosa la kutumia fedha ya serikali sasa naombeni ushauri wenu je Hawa pccb nitawashinda mahakaman au watanishinda?

Pole subiri wataalamu watakuja kukupa muongozo
 
Mi ni afisa wa serikali wilaya x nililipa pesa mbichi kwa watumishi 3 baada ya kukusanya Mapato ya minada ya mifugo wilaya x jumla y fedha tsh.2,500,000/: ninadaiwa kwenye poss machine yangu mm nimekataa kuzilipa Mana zimetumika kwa idhini ya mkurugenzi sasa nimeamriwa na pccb nilipe la sivyo nipelekwe mahakamani kwa kosa la kutumia fedha ya serikali sasa naombeni ushauri wenu je Hawa pccb nitawashinda mahakaman au watanishinda?
acha usanii sasa ulilipaje pesa za serekali kwa watumishi

hapo kuna harufu ya rushwa,
 
Nilikua nawalipa kwa kazi ya kukusanya ushuru mnadani ni watumishi waliokua wanalinda mnada ili mifugo inayonunuliwa isitoroshwe na wafugaj wasiopenda kulipia ushuru pindi wanaponunua mifugo mnadani ,,,hivyo pesa hizo zilitumika kwa matumizi hayo ya ulinzi na chakula kwa watumishi hao.
 
sasa si ulitakiwa uoneshe risit kwamba ulilipa
 
Mi ni afisa wa serikali wilaya x nililipa pesa mbichi kwa watumishi 3 baada ya kukusanya Mapato ya minada ya mifugo wilaya x jumla y fedha tsh.2,500,000/: ninadaiwa kwenye poss machine yangu mm nimekataa kuzilipa Mana zimetumika kwa idhini ya mkurugenzi sasa nimeamriwa na pccb nilipe la sivyo nipelekwe mahakamani kwa kosa la kutumia fedha ya serikali sasa naombeni ushauri wenu je Hawa pccb nitawashinda mahakaman au watanishinda?
Pole Sana mtendaji wa Kijiji,Ila nanyi mnachamgamoto ya ulaji wa pesa za gvt,lipa hiyo pesa,Kuna mwenzako huku kala milioni tatu ya vitambulisho vya ujasiriamali,sasa hivi tumbo joto.

Kiufupi tambua kuwa pesa ya gvt sio makande ya kwenye msiba kwamba kila mtu anajichotea tu,Ina utaratibu wake,kaama hukufuata utaratibu imekula kwako
 
Nilikua nawalipa kwa kuwa sign Sha kwenye karatasi baada ya kaz ya kunisaidia kulinda mnada mifugo isitoroshwe.
Usiogope kwa sababu kesi ipo pccp ugopa Kama ulikula kweli hiyo pesa? Kwenye ulimwengu sheria au sanaa ya sheria kitu kikubwa ni evidence hivyo basi kama unadoc zinazoonesha kuwa ulilipa watu lkn ulikuwa moral kuwalipa hata Kama taratibu ulizikiuka ziandae tu for more assistance nitafute
 
Pole Sana Kwa changamoto Kiongozi.
1. Malipo uliyoyafanya yalikuwa na maelekezo yoyote ya maandishi kutoka Kwa Mkurugenzi wa Halmshauri?
Najua umesema ulizitumia Kwa idhini ya Mkurugenzi lakini Je idhini hiyo ilikuwa Kwa Maandishi?
2. Unapokabidhiwa Pos ulikabidhiwa Kwa Mkataba maalum? Kama ni ndiyo, je kipengele cha baada ya makusanyo kinasemaje kuhusu utaratibu unaofuata Kwa fedha hizo?

Sasa
1. Endapo Kama ulikuwa na maandishi kutoka Kwa Mkurugenzi basi hiyo barua itunze itakusaidia huko PCCB au mahakamani.

2. Ila endapo Kama ulikiuka Mkataba wako ( Kama upo) maana najua kuna baadhi ya Halmshauri zinatoa PoS Kwa wahusika bila Mkataba. Basi kutakuwa na shida, itabidi ulipe tu ili uwe salama.

3. Lakini Kama pia haukuwa na Mkataba na Haukuwa na maandishi kutoka Kwa Mkurugenzi basi ulipe pia maana hii ni Tanzania Boss nadhani unanielewa.

4. Mwisho Siku nyingine hata Kama Mkurugenzi akikupa maandishi ya kutumia hizo fedha usikubali endapo Kama unaenda kinyume na Mkataba uliosaini unapokabidhiwa POS. Labda mpaka Huo Mkataba uvunjwe na kuwe na barua ya maelekezo na Nani atalipa fedha hizo zilizotumika, vinginevyo usijaribu.

Asante.
 
Kuna swali hapa hataki kulijibu na ndyo litaklo msaidia kuchomoka kwenye kesi hii

...MKURUGENZI ALIKUPAIDHINI YA KUTOA PESA KWA MAANDISHI AU MDOMO?
 
Nilikua nawalipa kwa kazi ya kukusanya ushuru mnadani ni watumishi waliokua wanalinda mnada ili mifugo inayonunuliwa isitoroshwe na wafugaj wasiopenda kulipia ushuru pindi wanaponunua mifugo mnadani ,,,hivyo pesa hizo zilitumika kwa matumizi hayo ya ulinzi na chakula kwa watumishi hao.
Unawalipaje watumishi hawana mshahara ?,hela mbichi ni IPI hiyo
 
Naomba unisaidie nikusaidie,
Je, hiyo idhini ya Mkurugenzi ipo au umeipoteza?
Sikupewa maandishi yoyote ila alikua anajua kuwa nawalipa hao wasaidizi wangu , mwishoni Ali sign dokezo nilipwe hiyo fedha ili nifute deni ila sikulipwa.
 
Back
Top Bottom