Halmashauri nchini zinawatumia wataalamu ngazi ya kata na vijiji kukusanya mapato badala ya kusimamia taaluma zao

tatamajuva

Member
Sep 11, 2019
74
83
Hili la wataalamu mbalimbali ngazi. Ya kata na Kijiji Kama afisa maendeleo, mifugo,kilimo,ustawi wa jamii wame base katika kukusanya mapato kwa maelekezo ya wakurugenzi wa miji,halmashauri,manispaa na majiji.

Kwasasa hawatekelezi majukumu yao waliyosomea na kusababisha kurudisha nyuma maendeleo ya sekta mbalimbali .

Wakulima,wafugaji,vikundi vya ujasiriamali havitembelewi /hawatembelewi na wataalamu hao.

Kwasasa Hali ni mbaya katika sekta mbalimbali kwani ukisimamia sekta moja nyengine zinakufa.

Chondechonde serikali iweke agents au iweze kuajiri maafisa biashara katika Kila kata kwa ajili ya kukusanya ushuru.

Maafisa hawakai maofisini na hawatembelei wananchi wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali.

Tutakusanya mapato lakini tutarudi nyuma sana,kwani watu watalima kienyeji,watafuga kienyeji.

Jamani hata katika masika hii hawatembelei wananchi.

Fanyeni utafiti mtagundua Hilo.
 
Umeongea kinafiki Sana.wafuate uwaambie shida zako za kilimo au ufugaji.ukiona hawajakusaidia nends kawashitaki,ni haki yako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom