Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi, tunaomba mnusuru mpasuko unaoletwa na Viongozi wa CCM Mkoa wa Tabora

Nyasa Girl

Member
Jul 11, 2017
10
19
Nikiwa kama mwanachama wa muda mrefu naandika kwa masikitiko makubwa sana, mambo yanayofanywa na uongozi wa CCM mkoa wa Tabora wakiongozwa na katibu wa CCM mkoa.

Naamini jukwaa hili ndio njia pekee ya kufikisha malalmiko ambayo yataweza kufika kwa urahisi kwenye uongozi wa CCM Taifa na hatimaye hatua stahiki zichukuliwe katika kukinusuru chama mkoani Tabora hasa, jimbo la Tabora mjini na halmashauri yake.

Nikiwa mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya wilaya ya Tabora ,nimeshuhudia mengi sana ambayo kimsingi chama kinatakiwa kuchukua hatua madhubuti, mchakato wa kupata wawakilishi ndani ya CCM watakaokwenda kushindana na wagombea wa vyama vingine katika uchaguzi mkuu ulikuwa na mambo mengi sana.

Mimi nitayataja mambo ambayo wanachama wengi na mimi nikiwamo tuliyoyashuhudia na yaliyotusikitisha na ambayo yamesababishwa na viongozi wa CCM mkoa wa Tabora

Mambo hayo ni yafuatayo:
  • Katibu wa CCM mkoa , ndugu Solomon Kasaba kuwa na mgombea wake kabla ya uchaguzi ambaye ni ndugu ADEN RAGE na AMINA KABOYONGA, ambaye pia alikamatwa na TAKUKURU.
  • Katibu wa CCM mkoa , mwenezi wa ccm mkoa, ndugu Majaliwa Majaliwa na Mjumbe wa kamati ya siasa mkoa ,ndugu Maimuna Abasi , kuwa wapiga kampeni za ADEN RAGE na AMINA KABOYONGA.
  • Uongozi wa ccm mkoa kuanza kumuandaa mwenyekiti mpya wa halmashauri na kumkata diwani ambaye alikuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Tabora, ambaye ndiye kashinda kiti cha udiwani.
  • Uongozi wote CCM mkoa , kuwa wapiga kampeni wa baadhi ya madiwani baada ya kuwalazimisha kuwapa rushwa ya pesa kwa wanaume na rushwa ya ngono kwa viti maalum.
  • Uongozi wa CCM mkoa kuwapitisha madiwani na wabunge ambao hawajashinda uchaguzi na ambao hawakubaliki kwa sababu wameshaongwa pesa
  • Uongozi wa CCM mkoa, kumpitisha AMINA KABOYONGA ambaye amepata kura 1, kwa sababu ameshawanunua viongozi wa mkoa na kuwaacha washindi wote wa nafasi za awali ambao kimsingi ndio wanakubalika na wana CCM pamoja na kwa wana Tabora mjini wote
Sisi wafia chama ambao ndio tunapata taabu za kuwanadi wagombea wetu,hatuwezi kukubali kubadilishiwa wagombea kwa nafasi za udiwani na ubunge kwa wale washindi, kwani kufanya hivyo wanakigawa chama na kuacha maumivu makali kwa wana CCM jimbo la Tabora Mjini

Tatizo kubwa ni uongozi mzima wa CCM mkoa ambao tayari wameshakula pesa za wagombea wao ambao wameshashindwa kwenye kura za maoni na hivyo kulazimisha wawe wagombea

Tunaamini malalamiko yetu yatakifikia chama cha mapinduzi na kuhakikisha wananusuru mgawanyiko unaoletwa na viongozi wa CCM mkoa kwa kulazimisha wagombea wao na kuacha kufuata machaguo ya wajumbe ambao ni wawakilishi wa wanachama walio wengi.

Tunaomba chama taifa, chukueni hatua madhubuti kwani uongozi wa CCM mkoa hawakitakii mema chama cha mapinduzi mkoani Tabora, tunaomba machaguo yetu kuanzia ngazi ya udiwani na wabunge yazingatiwe kwani ndio machaguo yetu na ndio yanayouzika na kukubalika kwa wananchi.

Ndimi,
NYASA MALEMBEKA
Mwakilishi wa wajumbe, Wilaya ya Tabora
 
CCM naona wamesahau ya 2010, walipoteza majimbo kwa sababu kama hizi.
 
Nyasa Malembeka, njoo Oxygen upate ya baridi upoze asila.
 
Mimi nashukuru kura za maoni za CCM na TAKUKURU kutokuwa meno,kwani nimelipwa deni la 4.6 Milioni nililokuwa namdai mdogo wangu tangu 2017.
Mdogo wangu huyo ni Katibu wa CCM wa Mkoa fulani. Napongeza sana kwa rushwa kushamiri huko maana hatimaye haki yangu nimeipata.
CCM hoyeeee..
TAKUKURU hoyee.
 
PONGEZI ZA SHUKRANI KWA KATIBU MKUU WA CCM, DR. BASHIRU ALLY

Tarehe 11/08/2020 ,nilishusha bandiko hili kwa kuomba chama cha mapinduzi kiingilie kati suala la washindi wa kura za maoni ,ndani ya CCM, kwani ilionekana tayari mambo si mambo hasa kwa washindi ambao walikuwa hawaivi na viongozi wa ccm mkoa wa Tabora katika nafasi ya udiwani, kumbe hili tatizo lilikuwa la nchi nzima, baada ya viongozi wa halmashauri kuu za mikoa kufanya yao kwa kuwakata washindi halali na kuwarudisha wasio wasio washindi, ilileta mvurugano sana na hatimaye chama kupitia katibu mkuu kutoa waraka wa kunusuru na kurudisha haki zilizoporwa.

Pia naomba niishukuru Jamii forum kwani bila jukwaa hili malalamiko yetu naamini yasingefika na yasingefanyiwa kazi, kwani Jamii forum imesaidia taarifa kufika na kufanyiwa kazi

Kwa niaba ya Wajumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Tabora tunasema asante CCM makao makuu na Asante sana Jamii forum kwa kufikisha taarifa

Wenu,
NYASA MALEMEBEKA
Mjumbe mkutano mkuu wa CCM,, wilaya ya Tabora
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom