Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kukutana Desemba 18, 2021

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,862
930

HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA ITAKUTANA TAREHE 18 DESEMBA, 2021

TAARIFA KWA UMMA

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa itakutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu, Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho kitatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuanzia Desemba 15, 2021.

Vikao vyote ni vya kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la Mwaka 2020 ibara ya 108 (2). Ambavyo vitafanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma ambapo maandalizi ya vikao hivyo yamekamilika.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

SHAKA HAMDU SHAKA
KATIBU WA HALMASHAURI KUU
YA CCM TAIFA ITIKADI NA UENEZI.
14 DESEMBA, 2021.

IMG-20211214-WA0112.jpg

IMG-20211214-WA0120.jpg
 
Bwana Kiroboto naomba utafute kazi nyingine, wenye Chama wana Kikao tarehe 18.
 
Here we go, wahuni na kiroboto nani zaidi?

Kiroboto alidhani anaijuwa ccm kumbe haijui, amuulize vizuri Lowasa ambaye alikuwa na influence kubwa lakini alitulizwa, sembuse hii takataka Kiroboto?
 
HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA ITAKUTANA TAREHE 18 DESEMBA, 2021

TAARIFA KWA UMMA

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa itakutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu, Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho kitatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuanzia Desemba 15, 2021.

Vikao vyote ni vya kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la Mwaka 2020 ibara ya 108 (2). Ambavyo vitafanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma ambapo maandalizi ya vikao hivyo yamekamilika.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

SHAKA HAMDU SHAKA
KATIBU WA HALMASHAURI KUU
YA CCM TAIFA ITIKADI NA UENEZI.
14 DESEMBA, 2021.

View attachment 2043745

View attachment 2043746
Vikao ni vya kawaida, ila tusisahau jambo moja muhimu kwenye mengineyo (AOB) nalo ni hili

- Majibizano Wanachama na Viongozi Waandamizi wastaafu wa CCM, jinsi yanavyoweza kukigawa Chama, na kujenga hisia kwamba ndani ya Chama kuna watu wasioguswa. Halmashauri Kuu ipitishe azimio ndaniya kikao hiki
 
Hiyo ndio itakuwa agenda kuu na ndio itachukua muda wao mwingi.

Baada ya kikao, wataalika media huku wakiimba: "CCM,CCM, CCM" huku rohoni kila mtu na lake.
 
hoja yoyote ya kumchukulia hatua Polepole tunagawana milango na madirisha.
 
V
Hiyo ndio itakuwa agenda kuu na ndio itachukua muda wao mwingi.

Baada ya kikao, wataalika media huku wakiimba: "CCM,CCM, CCM" huku rohoni kila mtu na lake.
Usidhani vikao vya CCM ni sawa na CHADEMA! Polepole wala hana impact ya CCM kumweka kwenye ajenda za vikao muhimu kama CC na NEC!
Kama kuna jambo kumhusu basi angekuwa ameshaitwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo baada ya kumsikiliza na kumjadili basi kikao hicho kingepeleka mapendekezo kwa CC na baadaye NEC ingefanya maamuzi ! CCM ni level nyingine kabisa!
 
Back
Top Bottom