Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha (UPDP) imemvua uenyekiti Fahmi Dovutwa kwa kufanya kosa la kukisemea chama hicho kinyume na Katiba

Wanamuonea bure kumtimua Dovutwa kwa kujitoa uchaguzi wa serikali za mitaa, kwasababu kujitoa huko kwa UPDP ni just saving faces, kuna vyama havina the capacity and resources za kushiriki uchaguzi, viko hoi, dholfu, hoi bin taaban, hivyo kutangaza kujitoa ni nusura yake, chama tangu kuundwa hakijawahi kushinda hata mtaa mmoja, unategemea nini?.

P
 
Hizi akili wangekuwa nazo chadema nchi ingesonga mbele ,wao wamekuwa misukule tu hata mbele hawaoni

Hongereni kwa uamuzi wa busara


State agent
Nimeamini wewe una mahaba ya dhati kabisa na chadema.
Kila post we uko na chadema tu!
 
Mwenyekiti wa People's Democratic Party amepoteza uwenyekiti wake baada ya kusaliti chama na kuwaunga mkono Chadema kujitoa kwenye uchaguzi wa serkali za mitaa kinyume cha sheria.

Fahmi Dovutwa ambaye tayari amepoteza muelekeo wa kisiasa kutokana na kuunga mkono tamko batili la Chadema hajui hatma yake kisiasa.

My take:
Chadema mlimdanganya huyu Mzee sasa mmemuacha peke yake hiyo sio fair. Mpeni hata nafasi awe makamu mwenyekiti wa chadema Taifa la sivyo huyu mzee atachanganyikiwa

Vyama vingine viache kuwasikiliza Chadema vitapotea kama Fahmi alivyopotezwa
 
Mbowe naye alitakiwa kufukuzwa sema anaongoza malofa yanamrudisha kinyume na katiba ,CCM wakisema jpm aongezewe muda wanachukia


State agent
 
Mbowe naye alitakiwa kufukuzwa sema anaongoza malofa yanamrudisha kinyume na katiba ,CCM wakisema jpm aongezewe muda wanachukia


State agent
Kuna watu wana umri, elimu, vyeo, uzoefu na hela vile vile kuliko wewe. Lugha yako siyo utamaduni wa watanzania wala misingi ya siasa za vyama vingi nchini.

Ukiona huna la kuchangia tuza basi heshima za wenzio mkuu wote ni wa TZ !!!!!!!!!!!!!!!!!!!111
 
Hizi akili wangekuwa nazo chadema nchi ingesonga mbele ,wao wamekuwa misukule tu hata mbele hawaoni

Hongereni kwa uamuzi wa busara


State agent
Acha ujinga wewe kama chadema ni Dhaifu kama huko CCM B Mbona kutwa kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi kwenye chaguzi mbalimbali kutumia mabilioni ya pesa za walipa kodi kuwanunua madiwani wabunge wenyeviti wa chadema,
 
Wanamuonea bure kumtimua Dovutwa kwa kujitoa uchaguzi wa serikali za mitaa, kwasababu kujitoa huko kwa UPDP ni just saving faces, kuna vyama havina the capacity and resources za kushiriki uchaguzi, viko hoi, dholfu, hoi bin taaban, hivyo kutangaza kujitoa ni nusura yake, chama tangu kuundwa hakijawahi kushinda hata mtaa mmoja, unategemea nini?.

P
Dovutwa katolewa kafara kuna sinema zinatengenezwa na CCM zipo njiani zinakuja
 
Mbona wakati ule wa uchaguzi mlikuwa mnakioorodhesha hicho chama ili mabwana zenu waone kuna vyama vingi havikutendewa haki? Sasa mnamkimbia Dovutwa!!
Ukiona hivyo ujue Dovutwa kagoma kuunga mkono Juhudi za mtukufu
 
Chama cha UPDP kimemvua madaraka Mwenyekiti wake mzee Dovutwa baada ya kuvunja katiba ya chama hicho.

Dovutwa aliungana na Mbowe wa Chadema kujitoa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ilhali katiba ya UPDP haina kipengere kinachoruhusu chama chao kujitoa kwenye uchaguzi wowote.

Dovutwa atabakia kuwa mwanachama wa kawaida.

Chanzo: Star tv habari

Maendeleo hayana vyama!

=====


Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha United People's Democratic Party (UPDP) imemvua uenyekiti Fahmi Dovutwa baada ya kubainika kufanya kosa la kukisemea chama hicho kinyume na katiba.

Uamuzi huo ulitangazwa jana Jumapili Desemba 2, 2019 Mjini Unguja, Zanzibar na Kaimu Mwenyekiti wa UPDP Taifa, Abdalla Mohammed Khamis akisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao hicho kujadili kwa kina makosa alioyafanya Dovutwa.

Alisema kosa kuu lililopelekea kuvuliwa kwa wadhifa wake ni kukisema chama hicho kuwa hakitoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa uchaguzi uliofanyika Novemba 24, 2019 Tanzania Bara kitendo ambacho alikifanya bila kuagizwa wala kupata ridhaa ya uongozi wa chama hicho.

"Alichokifanya Fahmi ni kukiuka katiba ya chama chake kwani hakupaswa kabisa kukisemea, uhalali wa kushirikiana au kutoshiriki uchaguzi huo na tunafanya hivi ili iwe ni funzo kwa viongozi wengine waliomo ndani ya chama na wanaokuja," alisema Kaimu mwenyekiti huyo.

Alisema suala la chama hicho kutoingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa imekiathiri kwani utekelezaji wa agizo alilotoa Dovutwa limesababisha chama kukosa wenyeviti wa serikali hizo ambao wataweza kuwakilisha chama.

Khamis alisema Dovutwa anaweza kukata rufaa endapo atahisi amevunjiwa haki yake kisheria na kikatiba na kwa sasa atabaki kuwa mwanachama wa kawaida.

Pia, alisema kikao hicho kilimteua Twalibu Ibrahim Kadege kuwa naibu Katibu mkuu, ambapo kabla ya uteuzi nafasi hiyo ilikuwa wazi.

Mwananchi limemtafuta Dovutwa amesema atafutwe baadaye kwani yuko safarini kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam.

Itakumbukwa, UPDP ilikuwa miongoni mwa vyama sita vilivyosusia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24, 2019.

Vyama vingine ni; Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, Chaumma na ACT-Wazalendo.


Chanzo: Mwananchi
Kwani Chama Chao hakina demokrasia? Kujitoa nako ni demokrasia.
 
Back
Top Bottom