Halmashauri Hai yapewa siku saba kusafisha Soko la Kwa Sadala

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,764
2,000
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Hai limetoa siku saba kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuondoa taka zilizopo kwenye soko la walaji la Kwa Sadala ili kunusuru afya za walaji.

Pia wamewataka kuziba shimo kubwa lililopo katika soko hilo ambalo ni hatari kwa wananchi wa maeneo hayo. Agizo hilo limetolewa mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha kawaida cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Madiwani hao wamesema kuwa wamepiga kelele kwa muda mrefu kuhusu uchafu katika soko hilo bila mafanikio

Diwani wa Kata ya Masama Magharibi, Harsoni Masakia, amesema baada ya kutembelea soko hilo na kukuta wafanyabiashara wakiuzia bidhaa chini huku pembeni yao kukiwa na uchafu wa mabaki ya mazao yaliyooza na kutoa harufu.

Amesema kwa muda mrefu pamoja na soko hilo kukabiliwa na changamoto ya usafi pia soko hilo linakabiliwa na ubovu wa miundombinu iliyopo katika eneo hilo na kuitaka halmashauri kuirekebisha ili iwe katika hali bora itakayowawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao katika mazingira salama.mwananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom