Halmashari wilaya zaamka - elimu ya uraia Chadema inafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halmashari wilaya zaamka - elimu ya uraia Chadema inafanyakazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Afisa utumishi wilaya ya Luddewa Bw. Juma Ally


  BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe (Iringa) limemsimamisha kazi kuanzia afisa utumishi mkuu wa Halmashauri hiyo Juma Ally kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kutoelewana na watumishi wenzake, upotevu wa Tshs mil 54 ambao aliufanya kwa njia ya kujiongezea mshahara pamoja na kushindwa kusimamia miradi na fedha za umma.

  Uamuzi wa kumsimamisha kazi afisa utumishi huyo ulitolewa juzi kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo wakati kikao cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa mbali mbali za robo mwaka tangu madiwani hao walipoingia madarakani mwaka 2010,kilichohudhuriwa na mbunge Filikunjombe.

  Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, amewaonya watumishi wengine wa Halmashauri hiyo ya Ludewa kuacha tabia hiyo mara moja akisema kuwa, “Ludewa sio shamba la bibi” na kuwa wakati umefika kwa watumishi wasiowajibika kuvuliwa magamba kwamba hatapenda kuona wilaya ya Ludewa inakwamishwa kusonga mbele kimaendeleo na watumishi hao.

  Kabla ya kusimamishwa kwa afisa utumishi huyo madiwani wote zaidi ya 33 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na diwani mmoja wa Chama cha TLP walipiga kura ya ndio ya kugoma kuendelea na ajenda mpya za kikao wakati zile maagizo na mipango mbali mbali iliyopangwa kufanyika kusimama utekelezaji wake kutokana na ufanisi duni wa wakuu wa idara katika Halmashauri hiyo.

  Kutokana na madiwani hao kugoma kuendelea na ajenda mpya ilimlazimu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Matei Kongo kusimama na kutoa maazimio ya madiwani wa CCM yaliyotolewa siku moja kabla ya kikao hicho dhidi ya afisa utumishi huyo baada ya kikao cha chama kuwahoji watumishi wawili wa Halmashauri hiyo akiwemo mkurugenzi wa Halmashauri na afisa utumishi huyo.

  Mwenyekiti huyo wa Halmashauri alisema kuwa kutokana na afisa utumishi huyo kuendelea kuwa na ugomvi na watumishi wenzake kasi ya maendeleo katika wilaya ya Ludewa imeendelea kuyumba na kuwa toka madiwani walipoingia madarakani wamekuwa wakitoa maagizo mbali mbali ya kimaendeleo bila kutekelezwa kwa wakati.

  Alisema kutokana na afisa utumishi huyo kukutwa na makosa ya kukwamisha maendeleo ya wilaya ya Ludewa, kujiongezea mshahara yeye mwenyewe, kujipandisha cheo yeye mwenyewe na rafiki zake wanne pamoja na kukataa kufanya kazi na baraza hilo la madiwani uamuzi ambao umefikiwa ni huo wa ulifikiwa ni wa kusimamishwa kazi kwa muda usiojulikana. Juma Ally pia anatuhumiwa kuongezea mishahara watuimshi wengine 65 kinyemela baada ya kupokea rushwa kutoka kwao.

  Uamuzi wa kusimamishwa kazi kwa afisa utumishi huyo umeungwa mkono na mbunge wa Jimbo hilo Deo Filikunjombe, madiwani wote wa CCM na TLP, Juma Ally mwenyewe akisema kuwa kikao cha madiwani hakiwezi kumfanya chochote kwani wao si mamlaka waliomteua.

  “Kilichokuwa kinachofanywa (kujiongezea mshahara) na Mtumishi huyu ni sawa na wizi,” alisema Deo Filikunjombe na kwamba kwamba uamuzi kama huo wa baraza la madiwani ni uamuzi ambao utampata mtumishi yeyote atakeyeshindwa kuwajibika ipasavyo katika Halmashauri.
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Duuuh! masikini chinga boy, imekula kwake! Ila jamaa ni jeuri kwa asili yake. Hata alipokuwa Wilaya ya Chamwino alikuwa na hako katabia ka ujeuri kwa watumishi wenzake, mweeeeh!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umenishtua kidogo, kumbe jamaa kaanza mbali. Mlamba asali haishi kuitamani kila aiendako.
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Badili kichwa cha habari ili kiendane na maudhui ya habari.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Maudhui ya kichwa cha habari haiko mbali sana na mada iliyoletwa kwa vile baraza la madiwani halmashauri ya huko kunakosemwa wameamka na kumwekea kigingi afisa utumishi kwa ubadhilifu. Kama kusingekuwa na mwamko wa uraia wangeendelea na dhana ya kufunikana.
   
Loading...