Halleluja - Watu wa Libya wameamka na kufukuza wahalifu wanaojiita waislamu

Status
Not open for further replies.
kweli we kipala, nimekuuliza maana ya salafy hujui.
Ngoja nikurahisishie swali,
unajua maana ya ansar?
Tatizo umekurupuka, unaongozwa na chuki ndiomana hauwezi kujenga hoja.
Nani asiejua marekani ndio walowasaidia wanamgambo wa libwa kumuangusha gadafi?
Tena ngome yao ilikuwa benghazi?
Nani asiyejua walibya walivyokuwa na maisha bora kuliko raia wa nchi nyingine nyingi za dunia kutokana na usimamizi mzuri wa mapato wa gadafi?

Hakuna mtu mwenye akili timamu atakae waunga mkono walibwa kwa walichofanya.
Sasahivi wanamaisha magumu kuliko ilivyokuwa wakati wa gadafi, waliyachoka maisha bora, wakadanganywa na wamarekani kuwa demokrasia ndio muhimu zaidi kuliko unafuu wa maisha.
Sasa yanawatokea puani.
Waliiga misri na kwingineko wakasahau huko mambo ni tofauti sana na libya.

Mpendwa, nikielewa vema unapenda kutangaza kuwa wewe unajua maana ya ansar na salafi. Hongera sana. Nadhani mimi najua pia. Je tuulizane maana ya maneno hapa ? (ansar: msaidizi; salaf: mzee, mtangulizi...)

Sasa hapa si mahala pa kujadili maana ya maneno haya katika upeo wa dini (kwa hiyo tuende uwanja wa dini) bali harakati ya kidini-kisiasa inayotajwa kimataifa kama wanajihadi-Salafiya; wenyewe mara nyingi wanatumia majina mengine lakini kuna pia vikundi vya mkondo huu kama vile Groupe Salafiste pour la Prédication et le Combat
الجماعة السلفية للدعوة والقتال.

Ni hao wanaojisikia kuwa na wito kuchukua silaha na kufanya vita dhidi ya waislamu wanaoona hawafuati mweleko "sahihi" au kile wanachoona kama athira ya magharibi na wakala wake.

Ni haohao waliojaribu kutumia habari za video ile ya kashfa kwa mashambulizi dhidi ya polisi (Pakistan, vifo 12 au zaidi) au balozi za Marekani (Misri, Libia, vifo 4).

Kwa jumla wale walioandamana kwa kutumia mawe, moto na silaha walikuwa wachache; lakini hao wachache wanazidi kuongeza ugumu katika maelewano na majidiliano kati ya tamaduni na dini duniani. Huko Libia walishambulia pia mapadre na masista wakatoliki waliowahi kuishi kule tangu miaka mingi kwa utulivu na kutoa huduma za afya kwa watu maskini.

Sasa nimesikia habari za Bengazi ninafurahia ya kwamba wananchi wengi sana walikata shauri kumaliza fujo la hao wachache na kuwaondoa. Sishangai sana ya kwamba wenyewe waliona hali yao chini ya Gadhafi tofauti na wewe.

Mpendwa umeona vema kunitambia eti najaa chuki.Kumbe lakini hapo sina habari. Naomba unisaidie umeona "chuki" katika maneno gani?


 
What does Hallelujah means? I am not here for 9/11, grow up dude. How can you talk about Islam and said it is not religious? Define the word "islam"?

Hi Dude!!
1. Halleluja = Alhamdulillah!

2. Tunashukuru sisi sote, bila shaka

3. Unataka kutuambia wewe umeshakuwa mtu mzima? Asante sana!

4. Naweza kwa kufungua mdomo na kutumia lugha. Hasa ikihusu mambo ya historia, siasa, uchumi na kadalika katika upeo wa watu Waislamu.

5. Ukihitaji kujua naomba ufungue thread katika uwanja wa dini. Utahudumiwa karibuni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom