Halleluja - Watu wa Libya wameamka na kufukuza wahalifu wanaojiita waislamu

Status
Not open for further replies.

Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,763
699
Taarifa imefika ya kwamba watu wa Benghazi (ambako juzi kundi dogo lilishambilia ubalozi wa Marekani na kumwua balozi wa nchi hii kwa maelezo ya kupinga video iliyomkashifu mtume Muhamad) waliandamana leo kwa wengi na kufukuza kundi la "Ansar al-Shariah" mjini. Katika majengo ya kundi hili watu walioshambulia ubalozi waliwahi kukutana.

Mimi (nikiwa Mkristo) nafurahi kwa sababu tukio la leo inaonyesha si Waislamu wengi walio tayari kuleta fujo na kuonekana kama vichaa - kinyume chake watu wa Benghazi 30,000 (wote waislamu maana hakuna wasio waislamu huko) waliandamana bila silaha na kuwalazimisha wanamigambo wa "Ansar al-Shariah" kukimbia mjini.

(MODS: HII SI MCHANGO KUHUSU DINI NA SI SAHIHI KAMA MNASUKUMA KILA POST YENYE NENO "UISLAMU" KWENYE KONA YA UWANJA WA DINI".

Basi someni taarifa:

"BENGHAZI, Libya - Hundreds of protesters stormed the compound of one of Libya's strongest armed Islamic extremist groups Friday, evicting militiamen and setting fire to their building as the attack that killed the U.S. ambassador and four other Americans sparked a public backlash against armed groups that run rampant in the country and defy the country's new, post-Moammar Gadhafi leadership. Armed men at the administrative center for the Ansar al-Shariah militia, suspected to have led the Sept. 11 attack on the U.S. Benghazi consulate, first fired in the air to disperse the crowd, but eventually withdrew from the site with their weapons and vehicles after it was surrounded by waves of protesters shouting "No to militias." .....

Some 30,000 people filled a broad boulevard as they marched along a lake in central Benghazi on Friday to the gates of the headquarters of Ansar al-Shariah.

"No, no, to militias," the crowd chanted, filling a broad boulevard. They carried banners and signs demanding that militias disband and that the government build up police to take their place in keeping security. "Benghazi is in a trap," signs read. "Where is the army, where is the police?"

Other signs mourned the killing of U.S. Amb. Chris Stevens, reading, "The ambassador was Libya's friend" and "Libya lost a friend." (Chanzo: Libyans storm militia building after giant protest in wake of attack on US consulate - The Washington Post)




Someni pia taarifa juu ya tukio hilihilo kwa Protesters seek to disband Libya militias - Africa - Al Jazeera English
 
Sasa kilichokufurahisha nini hapa?au na wewe ndio mmoja wa wanaofurahia ile film?
 
Sasa kilichokufurahisha nini hapa?au na wewe ndio mmoja wa wanaofurahia ile film?
1. Kilichonifurahisha nilitaja juu. Naona ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo ni muhimu kwa ajili ya amani na maendeleo duniani. Tukiwa tofauti katika imani tunaweza kufikia mengi kwa njia ya maadili mema ya pamoja. Wahalifu na wakoroga chuki ni hatari kila upande.
Siku za nyuma zilisikitisha maana picha ya Waislamu ilikuwa picha ya watu wenye fujo wanaotema chuki - na kuua (Wamarekani 4 Libia, Waislamu Wapakistani 12 leo hii huko Karachi...). Lakini hali halisi Waislamu wengi kabisa ni watu wanaopenda amani ilhali hawapendi kusikia matusi juu ya imani yao.

Furaha yangu ni Waislamu wapenda amani waliamua kutonyamaza lakini kuwaondoa wanaoleta fujo na kurejesha nchi yao nyuma. Hongera na mbarikiwe!

2. Hapa, sifurahi filamu baya kwa jumla na hasa siwezi kurahia filamu inayolenga kuchafusha imani ya watu.
 
.. This thread is religious ad infinitum.
"finita" gani??
Mpendwa kwa sababu unazotaja kila majadiliano kuhusu 9/11 yapelekwe "Dini" maana huewzi kuiandika bila kutumia neno "uislamu"?

Uenezaji wa harakati kali za Salafiya na jibu katika nchi za magharibu ni kati ya matatizo makubwa kwa amani ya kimataifa duniani.

# Salafiya wakali kama Al Qaeda wanalenga kuwaondoa athira ya Marekani katika Uarabuni kwa njia ya ugaidi
# walisababisha vita ya Afghanistan na uharibufu zaidi katika nchi hii
# Salafiya walijaribu kutwaa mamlaka katika Misri kwa njia ya uchaguzi na hadi sasa wako kundi wenye kura nyingi kwa nafasi ya pili; hao SI magaidi lakini inaonekana wana watu ndani yao walio tayari kutumia mbinu hizi
# vikundi vya salafiya wanaendelea kuua Iraq na Pakistan
# vikundi vya Salafiya walichukua nafasi ya video ya kashfa kujificha kati ya waislamu wengine na kushambulia balozi za Marekani (Libiy, Misri, Sudan) au wanapolisi (walio Waislamu pia katika huduma ya serikali isiyo Kisalafi kam Pakistan)

Nafasi hii ya Wasalafi wakali inalisha chuki upande wa nchi za magharibi (waliotangulia kulisha hasira kati ya Waislamu kwa siasa yao Uarabuni na Palestina...)

Pia mashambulio ya Wasalafiya wakali inaleta picha baya kati ya tamaduni na hasa kwa watu waliohamia katika nchi za magharibi amabko wanaona ubaguzi wao unaongezeka kwa kila kitendo cha kigaidi.

Hapa naona hatua ya watu wa Bengazi ni muhimu! Kuwafukuza kundi la wasalafiya inayosisitiza haki ya kubeba / kutumia silaha kwa madai eti ni watetezi wa imani ya kweli....
Hapa wananchi wengi wa mji huu walionyesha ya kwamba hawakubali maelezo bandia yale.
 
" Kikundi cha wahuni wachache, wasio na elimu yoyote wanaofanya kazi za kuwarubuni watu"
 
hivi unajua maana ya salafy au unaongea tu?
We ungeleta habari tu ingetosha, sio unaleta habari na kutoa ufafanuzi na hukumu wakati hakuna unachokijua juu ya uislam.
 
cha ajabu unawatetea wamarekani wanao ua watu waso na hatia kila kukicha, wanatesa watu, wanabaka na kudhalilisha hasa waislamu duniani kote.
Mkuu hujui unachoongea na kama unajua basi unapotosha kwa maksudi.

Nani leo asojua unyama na ukatili wa hali ya juu ya marekani na washirika wake?
Nani kawapa kazi ya upolisi wa dunia?
Wanajidai wanapambana na ugaidi wakati ndo wanaendelea kuzalisha magaidi zaidi?
Imagin wewe familia yako yote imeuliwa ktk vita vinavyoendeshwa na wamarekani.
U mdogo ki umri, kila uliekuwa unamtegemea ameuwawa au kama yupo ni kilema.
Je utasita kulipa kisasi kwa walomfanyia hivyo?
Hiyo ndo tafsri ya wanayoyafanya marekani na washirika wao.
Wanadhani wanapambana na ugaidi kumbe ndo wanazidi kuongeza maadui.
 
hivi unajua maana ya salafy au unaongea tu?
We ungeleta habari tu ingetosha, sio unaleta habari na kutoa ufafanuzi na hukumu wakati hakuna unachokijua juu ya uislam.
Asante kwa kunijua kimakini!!

Je una habari kuwa wanamigambo wa "Ansar al-Shariah" wa Libia wasihesabiwe kati ya mikondo ya Wasalafiya?
 
cha ajabu unawatetea wamarekani wanao ua watu waso na hatia kila kukicha, wanatesa watu, wanabaka na kudhalilisha hasa waislamu duniani kote.
Mkuu hujui unachoongea na kama unajua basi unapotosha kwa maksudi.

Nani leo asojua unyama na ukatili wa hali ya juu ya marekani na washirika wake?
Nani kawapa kazi ya upolisi wa dunia?
Wanajidai wanapambana na ugaidi wakati ndo wanaendelea kuzalisha magaidi zaidi?
Imagin wewe familia yako yote imeuliwa ktk vita vinavyoendeshwa na wamarekani.
U mdogo ki umri, kila uliekuwa unamtegemea ameuwawa au kama yupo ni kilema.
Je utasita kulipa kisasi kwa walomfanyia hivyo?
Hiyo ndo tafsri ya wanayoyafanya marekani na washirika wao.
Wanadhani wanapambana na ugaidi kumbe ndo wanazidi kuongeza maadui.
Kaka una picha yako ya Marekani kichwani - pamoja na habari nyingi zisizoweza kukanwa.

Ila tu picha hii haikuacha nafasi kuona dunia halisi kama hailingani na picha yako.

Tafakari: ni nini inayoweza kuhamaasisha watu wa mji mkubwa wa pili nchini Libia kuandamana barabarani dhidi ya wanamigambo wenye silaha? Kuingia katika hatari maana hao walianza kufyarulia risasi? na kuendelea hadi waliweza kuwafukuza?

Ulisema tu "cha ajabu" maana tukio halilingani na picha kichwani mwako.
Kumbe sasa nini ibadilike: kichwa au dunia?
 
Siku za waarabu kuisumbua dunia kupitia imani ya dini zinahesabika,

"TUTAHAMISHIA NGUVU ZA KIUCHUMI MIKONONI MWA ADUI ZAO"

Mafuta yatakuwa ni bidhaa inayopatikana kila nchi! udhibiti wa bei unaoratibiwa na Opec utakoma, bei ya vyakula itapanda maradufu kuliko ilivyo mafuta leo, mfano hai, msumbiji, malawi, sudan, kenya, uganda, tanzania, kongo kishasa, kongo brazavile listi inaendelea.

Tutabadili teknolojia ya usafiri isitegemee mafuta isipokuwa 25% hali hiyo itaporomosha bei ya mafuta, Mfano hapa ni msisitizo wa viwanda ulaya kutengeneza magari yanayotumia battery, ambapo mafanikio ni makubwa sana kwani ishatengenezwa gari inakwenda karibu 1000km kabla ya kurecharge battery na havitofautiani sana kwa speed na magari yatumiayo damu ya mwarabu!

ukijumlisha na soko lisilo na udhibiti nchi zinazotegemea pato la mafuta kuendesha bajeti yake zitaamua ama ziendelee kushinda kwenye nyumba za ibada ama kwa kuokoa maisha yao na wananchi wake, wamtafune "Nguruwe" kukidhi maelekezo ya kuruani kinyume chake wafe njaa.

Mafuta na gesi tutakuwa navyo kama wao, chakula tutakuwa nacho wao hawana, maji tuanayo, tutaendelea kuwa nayo wao mtihani. MUOMBE MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU USHUHUDIE HAYA.
 
Libia ndio nn mkuu...?!!hii propaganda ya Marekani..balozi aliuwawa kama ambavyo Marekani inaua watu wengine wengi Duniani..
 
Libia ndio nn mkuu...?!!hii propaganda ya Marekani..balozi aliuwawa kama ambavyo Marekani inaua watu wengine wengi Duniani..

Napendelea kujadili dunia halisi si ndoto. Balozi aliuawa na watu waliotoka majengo ya "Ansar al-Shariah" mjini Benghazi waliojiunga na umati wa watu mamia kadhaa walioandamana mbele ya ubalozi.

Jana watu 30.000 wa Benghazi waliandamana kuwafukuza
"Ansar al-Shariah" na wengine wao walibeba tangazo la kusikitika kifo cha balozi na kumwita "Rafiki wa watu wa Libia".

Kama ni propagansa wa Marekani - basi soma taarifa ya Aljazeera.com (ni shirika la habari ambayo ofisi yao ilibomolewa na mabomu ya Marekani wakati wa vita ya Iraq kwa sababu majenerali Waamerika walichukia taarifa zake...)


 
Napendelea kujadili dunia halisi si ndoto. Balozi aliuawa na watu waliotoka majengo ya "Ansar al-Shariah" mjini Benghazi waliojiunga na umati wa watu mamia kadhaa walioandamana mbele ya ubalozi.

Jana watu 30.000 wa Benghazi waliandamana kuwafukuza
"Ansar al-Shariah" na wengine wao walibeba tangazo la kusikitika kifo cha balozi na kumwita "Rafiki wa watu wa Libia".

Kama ni propagansa wa Marekani - basi soma taarifa ya Aljazeera.com (ni shirika la habari ambayo ofisi yao ilibomolewa na mabomu ya Marekani wakati wa vita ya Iraq kwa sababu majenerali Waamerika walichukia taarifa zake...)



Kama hujui hao Al jazeera ni sawa tu na BBC au CNN, wote ni pro America na wao wako kusaidia kusambaza ulongo kila pahala kwa amri ya US...ukumbuke wmiliki wa Al jazeera ni Quatar ambao ni kituo kikuu cha kusambazia silaha kuingia Libya kumpindua Ghadafi na Kumuua, pia hao hao vibaraka w Us ndio wanaoshiriki kwenye vita ya Syria, watch out watu 30 elf walikua wapi wasimsaidie balozi alipovamiwa?!!

Je Libya ni salama? jibu ni kwamba ni sehemu hatari sana sasa a hakuna serikali pale ni magenge tu yenye silaha hata hao Vibaraka wanaoitwa viongozi wanapiga picha wakiwa Quatar wanasema wako Tripoli...
 
kweli we kipala, nimekuuliza maana ya salafy hujui.
Ngoja nikurahisishie swali,
unajua maana ya ansar?
Tatizo umekurupuka, unaongozwa na chuki ndiomana hauwezi kujenga hoja.
Nani asiejua marekani ndio walowasaidia wanamgambo wa libwa kumuangusha gadafi?
Tena ngome yao ilikuwa benghazi?
Nani asiyejua walibya walivyokuwa na maisha bora kuliko raia wa nchi nyingine nyingi za dunia kutokana na usimamizi mzuri wa mapato wa gadafi?

Hakuna mtu mwenye akili timamu atakae waunga mkono walibwa kwa walichofanya.
Sasahivi wanamaisha magumu kuliko ilivyokuwa wakati wa gadafi, waliyachoka maisha bora, wakadanganywa na wamarekani kuwa demokrasia ndio muhimu zaidi kuliko unafuu wa maisha.
Sasa yanawatokea puani.
Waliiga misri na kwingineko wakasahau huko mambo ni tofauti sana na libya.
 
Asante kwa kunijua kimakini!!

Je una habari kuwa wanamigambo wa "Ansar al-Shariah" wa Libia wasihesabiwe kati ya mikondo ya Wasalafiya?

eleza kwanza maana ya salafy na ansar, sio unapiga porojo tu. Hujui unachoongea ila chuki zako ndo zinakupelekesha.
 
mkuu Somoche, kipala hajui anachoongea. Ana muhemko wa chuki ndo unaomsumbua.
Watu kama hawa tumesha wazoea.
 
Kama hujui hao Al jazeera ni sawa tu na BBC au CNN, wote ni pro America na wao wako kusaidia kusambaza ulongo kila pahala kwa amri ya US...ukumbuke wmiliki wa Al jazeera ni Quatar ambao ni kituo kikuu cha kusambazia silaha kuingia Libya kumpindua Ghadafi na Kumuua, pia hao hao vibaraka w Us ndio wanaoshiriki kwenye vita ya Syria, watch out watu 30 elf walikua wapi wasimsaidie balozi alipovamiwa?!! ..

Habari hupendi? Pole sana!

Unapendelea kuepukana nayo kwa kujadili wale wanaoleta habari badala ya habari yenyewe? Mjanja we!

Jaribu habari hapa kwa Xinhua (huduma ya serikali ya China): Pro-government demonstrators storm militia compound in eastern Libya - Xinhua | English.news.cn

Na hao wamenunuliwa na Marekani ?

Au labda hii?
Libyan demonstrators wreck militia compound in Benghazi
 
"finita" gani??
Mpendwa kwa sababu unazotaja kila majadiliano kuhusu 9/11 yapelekwe "Dini" maana huewzi kuiandika bila kutumia neno "uislamu"?

.

What does Hallelujah means? I am not here for 9/11, grow up dude. How can you talk about Islam and said it is not religious? Define the word "islam"?

God-Jesus bless ISRAEL :israel:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom