Haliniishi moyoni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haliniishi moyoni...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annina, Mar 12, 2010.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Habari za siku mingi wapendwa, nina wakati mgumu naomba mawazo yenu katika hili. Kwa kifupi shangazi yangu yaani dada wa baba yangu alitoka na boyfriend wangu wa kwanza. Hawakuwa wakifahamiana kabla, niliwatambulisha na sababu shangazi alikuwa kwa kiasi fulani karibu na mimi akazoeana na yule kijana. Ikatokea wakakutana SA wakaanza kuwasiliana na kutembeleana mwisho wa siku wakawa wapenzi! Waliporudi shangazi alijikausha, hakuniambia kwamba walikutana na kijana SA, kijana akaniambia walikutana briefly.

  Miezi 2 baadae kijana alitukutanisha mimi na shangazi na akaniambia hawezi kuvumilia tena maana nafsi yake inamsuta kwa hiyo inabidi aniambie ukweli kuwa walikutana na shangazi walipokuwa SA na wakafanya waliyoyafanya, anajutiana tendo hilo na anaomba nimsamehe. Alijitahidi sana kuonyesha kujutia na kuomba msamaha kwa njia na lugha zote lakini kwangu ilikuwa ngumu kusamehe na kusahau - pengine nilikuwa bado mdogo kipindi hicho kuweza kuhimili na kukabiliana na masuala (sio matukio!) mazito kiasi hiki. Na huo ulikuwa mwanzo wa mwisho wa mahusiano yangu na kijana niliempenda na kuamini ananipenda pia.

  Ni miaka 3 sasa toka tukio hili litokee, lakini kila mara nimejikuta narudia kuwaza na machungu yananijia upya... kimsingi nimewasemehe wote ingawa kwa huyu kijana bado siwezi hata kupokea salam yake... shangazi tumewahi kukutana mara moja kwenye kikao cha familia - aliniomba radhi na akaniomba yasifike kwa familia.

  Sasa shangazi amepata internship huku niliko, ameniandikia anaomba niwe mwenyeji wake nimhifadhi kwa miezi 9 atakayokuwa huku, nashindwa nimjibu nini maana bado sijasahau yaliyotokea, nahofia anaweza kufanya jambo jingine hata kama sio kutoka na mchumba wangu maana anaonyesha kutojali masilahi ya wengine. Nabaki najiuliza nifumbe macho nimpokee? Nitaweza kuzuia hisia zangu kwake kwa kipindi chote hicho? Ushauri tafadhali.

  Asanteni sana,

  Annina
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Im speechless
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Follow your heart to the very end
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Annina pole shost, jamani aunt huyu mhhhhhhhhhhh!!
  Je huyo aunt yako kiumri mnaringana? Au yeye mtu mzima kuzidi wewe?

  Kama sehemu unayoishi sasa hivi mpo pamoja na mchumba wako tafadhali usikubali kumkaribisha hapo atakunyanganya tonge mdomoni huyo aunt.
   
 5. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,356
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Mwambie hakuna nafasi, utakaribishaje kitu kilichokuumiza huko nyuma? akirudia utafanyaje? think twice!
   
 6. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante sana Pretty, shangazi ananizidi umri kwa zaidi ya miaka 10. Mchumba yupo mji mwingine lakini tunakuwa pamoja mara nyingi. Kwa kweli huyu shangazi ananipa wakati mgumu, sijui yeye kasahau au ndio ameona yamepita tugange yajayo, au ndio njia ya kurudisha amani hata sielewi!

  Asante sana,

  Annina
   
 7. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Achana naye huyo shangazi yako. Mwambie unaishi na rafiki yako so utamtafutia pa kukaa kwa mda huo. Then mtafutie chumba kwa mwanaume ambaye ni single akakae huko...nyege zikimzidia watamalizana wenyewe. Na kwako usimuonyeshe hata kidogo. Mpige kiswahili mpaka mda wake utakapoisha wakukaa hapo...yn hata kama utaweza kutunga safari za hp na pale poa tuu. Mijitu mingine haina mishipa ya aibu ilishaga katikia tumboni mwa mama zao.
   
 8. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,821
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  amlete kwangu annina atakaa bila taabu mpaka amalize shughuli yake
   
 9. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2010
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante Dada penny ,Hivi ndivyo ninavyokupendea Humwachi Mtu na Kinyesi (Mav)
   
 10. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Unaambiwa kwamba kutenda kosa sio kosa ila kurudia kosa ni kosa,Mpe chance nyingine
   
 11. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
   
 12. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mijitu mingine jama haina second chance...yn ukiteleza tuu tayari inakula kwako tena maana anakuona kama **** fulani. Bora alisha mjuaga tabia yake so sioni sababu ya yeye kutumia tuu oblongata yake vizuri akamueka kwapani na kumfungia huko. Prevention is better than cure!. Ama?
   
 13. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante sana Penny, ni kweli kinga ni bora kuliko tiba, ingekuwa mimi wala nisingethubutu kumuomba nikakae kwake baada ya tukio lile, ndio maana najiuliza ni kweli amesahau na kujirekebisha au ananijaribu?


  Annina
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,442
  Trophy Points: 280
  Annina, Maisha ni mafupi hapa duniani. Binadamu wote hatuko perfect tunafanya makosa mbali mbali ingawaje makosa mengine yanakuwa na uzito mkubwa kwa ndugu na jamaa na hata kuweza kuwatenganisha ndugu wa karibu kabisa. Ili kuwa na amani ndani ya roho yako msamehe Shangazi yako na pia kama haitakuwa na ugumu kwako kumhifadhi kwa kipindi hicho cha miezi tisa basi mimi kwa maoni yangu sioni kwanini usifanye hivyo na hili litamdhihirishia kwamba umemsamehe kwa upumbavu wale alioufanya. Kila la heri Annina.
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,201
  Trophy Points: 280
  Annina unajua maana ya kusamehe?
  Kama unajua maana yake na kweli umemsamehe basi mkaribishe shangazi yako.

  Annina unamwamini mchumba wako?
  Kama unamwamini mchumba wako basi mkaribishe shangazi yako.
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  majambo hayakuishi?
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Pole sana Annina..Pole kwa kuumizwa hivyo, imenigusa sana moyoni rafiki yangu.

  Nadhani jambo la msingi, kama ulimsamehe kikweli, mkaribishe nyumbani, lakini umwambie b/f wako asije nyumbani muda wote huo, maana anaweza kumnyakua huyo!

  Bora muwe mnakutania kwa b/f wako kuliko hapo kwako.Lakini katika kukaa nae usikumbushe yaliyopita, we kaa kimya kama kobe anaetunga sheria, na akianzisha maneno hayo we nyamaza tu!

  Miezi 9 si mingi, atamaliza na kuchapa zake mwendo, na atakuachia amani yako.

  Lakini pia kama ana akili, kweli anaweza kurudia kosa ZITO NAMNA HIYO?

  All in all, you forgave, then forget!
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu hiki kitakuwa Kifungo cha Nyumbani kwake sasa, Namshauri Annina aufuate moyo wake unamwambiaje kama Bado ana Kinyongo atafute Njia Nzuri ya Kumpotezea, mojawapo ni kumwambia ninaishi Chumba kimoja na B/F
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nimekusamehe LAKINI SITASAHAU:D:D
   
 20. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  My dia najua jinsi inavyouma hasa kusalitiwa na mpz,mm naona msamehe maadam ulihsasamehe,mkaribishe nyumbani kwako na na ikiwezekana na mpz wako pia mwambie aje!Imay sound stange to some pple but ol I knw is kama Mungu kapanga ulie nae sasa awe wako atakuwa tu.ktk maisha hutakiwi kuwa na wasiwasi kama digidigi!cha muhimu ni ww kujiamini,then utawaamini wengine,kama litatokea lolote tena usife moyo,he wasnt ment for u!God will make a way
   
Loading...