Halima Mdee sasa aukana uchumba wake na Joshua Nassari...

kuna mahali niliona kuwa ana katabia kabaya,
atakuwa ameshanogea hawezi kuolewa tena

Is not fair. Kwani mangapi Jukwaani yamepotoshwa? Mbona kwa uwazi ilionekana si kweli, the age difference. Joshua ametoka kwenye familia ya kichungaji, Halima ni mtoto wa kijiweni, muhuni kwa mavazi, ongea, sijui mengine.
 
Ningeshangaa kijana wa miaka 26 kufunga ndoa na huyu Bi kizee. Nasari si ana miaka 26?
Afu Halima Mdee nini kimempata mbona anaongea pumba sana siku hizi?:doh:
 
0.jpg


MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.


“Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo,” alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia.

Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni.

“Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili,” alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu’.

Chadema ina idadi kubwa ya wabunge vijana ambao hawajaoa, ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’; wa Ubungo, John Mnyika; wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na sasa Nassari.
Zitto Kabwe kumbe nae hajaoa, mbona nilisikia kuwa alimuoa mwalimu wake aka lecturer wake?? au nipo wrong plz!!!!!
 
tama umenipa raha,km maneno yangelikuwa sumu yangeutoa uhai wao,km yangekuwa tindikali yangebabua ngozi zao lkn ah hayana risas wla hayababaish
 

images
images


MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari. “Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo,” alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.
“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia. Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa. Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni. “Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili,” alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu’.

Chadema ina idadi kubwa ya wabunge vijana ambao hawajaoa, ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’; wa Ubungo, John Mnyika; wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na sasa Nassari. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ametaka wananchi kutoa maoni ya Katiba mpya ili walete mabadiliko mwaka 2015. Aidha, amewasihi kuacha kutopiga kura, kwa kuwa katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki waliojitokeza walikuwa wachache.

Aliwasihi vijana kujitokeza Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakapotolewa kwa ajili ya kuboresha taarifa zao na wengine kujiandikisha upya. Alisema hayo katika mkutano huo na kumsifu Nassari ambaye alidai ni kijana atakayeleta mabadiliko ndani ya jimbo hilo ingawa baadhi ya watu walihoji umri na mambo mengine. Mbowe alisema chama hicho kitatumia njia ya miguu, magari hata helikopta nchi nzima, kufikia wananchi ili watoe maoni yao juu ya mchakato wa Katiba mpya.

Alitoa rai kwa Polisi kuacha kupiga mabomu, kutumia risasi na nguvu zaidi, nyakati za uchaguzi kwani vijana wanaoumia ndio watakaokuwa viongozi wa baadaye. "Nawashukuru kwa kunipa kijana mjanja, yaani Nassari namkabidhi Lema (Godbless) ili aje naye mjengoni (bungeni) na sisi wabunge wa Chadema tutampokea na wananchi. “Lakini nawapasha ninyi vijana, kunapotokea suala la uamuzi wenu kwa ajili ya maendeleo, pigeni kura na natoa rai, tumieni marekebisho ya Daftari mjiandikishe na kulinda kadi zenu, ili tulete maendeleo, kwani ushindi wa Chadema ndiyo safari ya CCM mwaka 2015 na kila wanapotupiga mabomu tunashinda," alidai Mbowe.

Mbunge wa Arusha Mjini, Lema alishukuru wananchi hao na kusema watuhumiwa wa rushwa wakae chonjo, kwani baada ya Chadema kushinda Arusha Mjini na Arumeru Mashariki maendeleo yatapatikana. Aliomba wananchi kuondoa itikadi zao za vyama na kumpa ushirikiano Nassari kwa kuwa yeye ndiye mbunge atakayewaletea maendeleo. Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa, alisema ushindi huo ni wa kishindo, kwani walimtanguliza Mungu na kutoa angalizo kuwa jimbo la Monduli nalo wanakaribia kulichukua.

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alisema yeye si mtu wa ahadi hewa, hivyo atashirikiana na Nassari kuchimba visima viwili na kuongeza kuwa mfadhili wa chama hicho, Mustapha Sabodo, amejitolea kuchimba vinne ili kuondoa kero ya maji jimboni humo. Wabunge majeruhi Hali za wabunge wawili wa Chadema walioshambuliwa mwishoni mwa wiki Mwanza na kujeruhiwa wanaendelea vizuri.

Wabunge hao wa Ilemela, Highness Kiwia na wa Ukerewe, Salvatory Machemli, wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakiendelea na matibabu baada ya kupata rufaa kutoka Hospitali ya Bugando, Mwanza. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Machemli alisema bado wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na hali zao zinaendelea kuimarika. Alisema Kiwia bado hajafanyiwa kipimo cha MRI ili kuangalia usalama wa kichwa, kutokana na majeraha kichwani.
 
Makinda agusia ndoa ya Nassari, Halima Mdee

SUALA la ndoa kati ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) leo limeibukia bungeni baada ya Spika Anne Makinda kuwatania na kusababisha washangiliwe walipoinuka wakati mmoja wakitaka kuuliza maswali.

Mdee na Nassari walitaka kuuliza maswali ya nyongeza katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Betty Machangu (CCM) kuhusu mikataba isiyokuwa na tija iliyoingiwa kati ya wawekezaji wa mashamba 41 ya kahawa mkoani Kilimanjaro na Vyama vya Ushirika.

Baada ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe kulijibu akikiri kuwepo upungufu mkubwa katika uwekezaji huo, Mdee, Nassari pamoja na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe walisimama wakitaka kuuliza swali la nyongeza.

"Nassari na Mdee, lakini kwa kuwa hawajafunga ndoa, namuita Kiongozi wa Upinzani," alitania Spika Makinda na kusababisha kicheko na kushangilia kutoka kwa wabunge.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Halima alisema, sasa yupo tayari kufunga ndoa na Mbunge wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

"Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo," alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa Chadema.

Alisema, yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo hilo ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

"Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi," alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia.

Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake kuhusu useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa. Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni.

"Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili," alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu'.

Hivi karibuni, Halima alikaririwa akisema kuwa, suala la yeye kuolewa na Nassari halipo, na kwamba, alizungumzia jambo hilo hadharani kwa utani tu wa kisiasa.
 
Kitu ambacho nimegundua kwa mtoa mada hii na wachangiaji wengi ni wadada,ndiyo maana majibu yao
ni ya kimbeakimbea,na inaonyesha wengi wenu hamjaolewa ndiyo maana mmeshabikia sana kwa sababu
ya nature ya kawivu.Na wanaume walioshabikia hili pia wanatia mashaka maana inakuwaje wanaume
wazima muwe na tabia za umbea!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom