Halima Mdee: Rais Magufuli, Serikali yako imechafuka, chutama uweze kujisitiri

CHADEMA katika ubora wao wa kutumia mitandao ya habari. Unapofika wakati wa uchaguzi wale wapiga kura huwa hawaangalii mwanasiasa katika kipindi cha miaka mitano ameandika makala ngapi kwenye facebook, Twitter au Instagram.

Wao wanapima maendeleo halisi, kwa kutazama kipi kipya kimeletwa na mbunge kwenye jimbo lao.

Halima Mdee anapoteza nguvu zake mbele ya keyboard, wapiga kura wa Kawe hatutazama amefungua uzi mara ngapi mitandaoni, awe muangalifu sana.
Binafsi mm sio mwana siasa ,mm ni mwalim na huwa sishabikii chama chochote na angalia mtu nikimuelewa napiga kura.Ila kwa elim yangu ndogo nilio nayo rais wetu mambo mengi anaharibu kwa sababu ya ubabe.Mm naangalia huku nilipo kwenye elim mambo yameharibika mnoo pesa ni ndogo mnoo anayoitoa,walianzisha sera ya wanafunzi waishie drs la sita hawajawah kuleta vitabu wanasema fanya vyovyote masomo yafunishwe.

Leo huku mitihani ya wilaya na mikoa tunaandika ubaoni,wastaafu wengi wanadai mafao yao,kibaya zaidi wanakuja kutulisha viapo eti ole wetu watoto wafeli tutakiona.Kwakweli mm nilioko huku nikiona mtu anatetea hii serikali najua yeye kashiba lakini hajui kuna mtoto wa shangazi,mjomba au mdogo wake.

Wengne tulikuwa na moyo wakijitolea kuwa wazalendo tukiiamini mungu atatulipa tunafundisha mpaka basi ili watoto waende vipaj na wengne wafaulu vzri ila shahd ni Allah tumekataa tamaa mpaka basi.Rais abadilike bwana hata mungu hampendi mtu jeuri na mwenye kibri akubali kusikiliza ushauri wa watu jamani.
 
RAIS MAGUFULI, SERIKALI YAKO IMECHAFUKA,CHUTAMA UWEZE KUJISITIRI!

NDUGU RAIS naona Trillion 1.5 imekutoa mafichoni, CAG ameivua nguo SERIKALI yako! CHUTAMA uweze kujisitiri !! USITISHE WATU!

Nasema na wewe nikiwa nina kumbukumbu ya kukamatwa na vyombo vyako vya usalama SAA TISA ALFAJIRI (31/3/2018) na kuwekwa ‘lock up’ kwa SIKU TATU nikiwa nimetoka kwenye MATIBABU! Naandika nikifahamu vyombo vyako vya DOLA vitakuja ‘kunikamata’ tena kwa kuwa MTUKUFU umetoa AMRI kwamba yeyote atakayezungumzia suala la shilingi Trillion 1.5 kama lilivyoainishwa kwenye ripoti ya CAG akamatwe na afungwe!! Ngoja tuseme ili utukamate na kutufunga vizuri!!

Nimekusikia JANA kupitia vyombo vya habari ukinukuliwa ukisema “ kuna ugonjwa tumeupata sisi watanzania wa kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli,sasa sijui huu ugonjwa umetoka wapi,lakini ni kwa sababu hii itandao hatuicontrol sisi….ndio maana mkienda katika nchi kam China sina uhakika kama wana google na whatsApp kama tulizonazo sisi” mwisho wa kunukuu!! Ndugu Rais hapa sitajadili kama CHINA wana GOOGLE au whatsApp’ nikitambua kwamba toka umetangazwa na Tume ta Taifa ya uchaguzi kama ‘mshindi halali’ wa Urais umegoma kabisa kusafiri kwenda NJE YA MIPAKA YA AFRIKA MASHARIKI na Kati..ukidai unaiNYOOSHA NCHI.

Kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu sana kwako kujua kama China ‘wana GOOGLE au WHATSAPP’ Mara ya kwanza nilidhani husafiri kwa sababu ya gharama, nikaja nikagundua kwamba gharama ilikuwa ni POROJO pale ulipoamua kumtuma MAKAMU WAKO WA Rais akuwakilishe kwenye mikutano mbalimbali ya KIMATAIFA inayokutaka wewe kama MKUU wa Nchi kukutana na wakuu wa Nchi wenzako kujadili mambo MAZITO yatakayoiletea neema Nchi yetu!

Ndugu Rais natambua hasira zako dhidi ya ‘Google na whatsapp’…nadhani hapa ulikuwa una maanisha ‘mitandao ya kijamii’! kutokana na ukweli kwamba umeshindwa kuvidhibiti kama ambavyo umefanikiwa kuvidhibiti vyombo vikuu vya habari! Huku kwenye mitandao ya kijamii watu wako huru, hawataki kulishwa matango pori ambayo wewe unatamani watanzania walishwe! Kwa lugha nyingine watanzania wanataka kujiepusha na ugonjwa wa kuamini kila SERIKALI yako inachokisema..

Jana tumekushuhudia ukimsimamisha CAG na kumuuliza kama kwenye ripoti yake kuna pahala ameandika kuna shilingi trillion 1.5 zilizoibiwa , kisha ukamuuliza na MTOTO wako Katibu Mkuu wa wizara ya FEDHA kama NCHI imeibiwa …. NAE akakupa jibu “hapana Mheshimiwa” ….SIJUI ULITARAJIA MTOTO atampa jibu gani BABA….

NDUGU RAIS NINA MAMBO 8 AMBAYO NATAKA UYASOME NA KUYAELEWA..KISHA UTAJIJIBU MWENYEWE KAMA UMEFANIKIWA KUINYOOSHA NCHI….AU NCHI IMEKUNYOOSHA….

1. Alichokisema CAG kwenye ukurasa wake wa 34 ,nanukuu “ Kati ya shilingi bilioni 25,307.8 zilizokusanywa , shilingi bilioni 23.792 zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi , matumizi mengine ,matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatokananayo na amana za serikali pamoja na riba’ CAG hawezi sema pesa zimeibwa au la…anachotuambia SISI wananchi ni kwamba mpaka mwaka wa fedha unaisha 30 Juni 2017. Na mpaka anawasilisha ripoti yake kwako Mwezi Machi 2018 kulikuwa kuna bakaa la shilingi Trillion 1.5 ambalo halijulikani limefanya kazi gani !Mpaka sasa si wewe wala WASAIDIZI wako walioweza kujibu ,

Kwa kuwa taarifa imeshapita kwako na wewe ukatoa idhini iletwe mbele ya BUNGE, tunaomba MTUACHIE wabunge tufanye kazi yetu!! UMELIZIMA BUNGE….HUWEZI ZIMA FIKRA YAKINIFU

2. CAG anasema nchi imeshindwa kupata mapato ya kodi yenye thamani ya shilingi trillion 4.44 kutokana na ufanisi mdogo wa baraza la rufaa la kodi na Mahakama ya rufaa kutokana na upungufu wa makamu wenyeviti na wajumbe wa bodi zake hali inayopelekea kushindikana kufanya vikao vya kutosha hivyo serikali kukosa mapato!

3. CAG anasema TRA haikukusanya kodi yenye thamani ya shilingi 1,827,720,075,433.35 (Trillion 1.8 ) kutokana na mapingamizi ya kodi ambayo yalikwisha shughulikiwa na kukamilishwa. Hivi zile ziara zako za kushtukiza na za mara kwa mara TRA zimezaa matunda kweli??

4. CAG anatuambia serikali yako haifuati SHERIA ya Manunuzi ya UMMA na KANUNI zake wakati wa kufanya MANUNUZI, ameeleza wazi kabisa moja ya manunuzi yaliyofanyika bila kufuata sheria ya manunuzi , ni manunuzi ya ile ndege ya Q400 BOMBANDIER yenye thamani ya shilingi Bilioni 51.838 uliyoipigia upatu kwamba umelipa CASH kama vile unatoa fedha zako mfukoni !SISI WAKONGWE TUNAJUA mara nyingi DILI za NAMNA HII zina harufu za wizi na ufisadi

5. CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka kutoka shilingi (Bilioni 28.6 mpaka shilingi Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika kipindi cha UTAWALA wako matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe.Lissu mmegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!

Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”

6. CAG anatuambia kwamba SERIKALI yako ilikopa ndani zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa 10/08%. Kitendo hiki mbali na kuwa kinyume na sheria kina athari kubwa kwa wakopaji wengine(wafanyabiashara)kwani sehemu kubwa ya mtaji wa mabenki unakuwa umefungwa kwenye fedha walizokopesha Serikali kwa muda mfupi na muda mrefu. Matokeo yake , riba ya kukopesha kwa watu binafsi inakuwa kubwa na gharama ya maisha inakuwa juu!

7. CAG anatuambia kwamba Serikali IMEPORA akiba za mamilioni ya WASTAAFU waliotumia jasho na damu yao kulitumikia Taifai ! IMEKOPA MIFUKO ya HIFADHI shilingi bilioni 5,343 (Trillion 5.3) na kuamrisha ilipwe shilingi bilioni 3,183 (Trillion 3.1). Serikali ituambie ,shilingi bilioni 2,160 (Trillion 2.1) ziko wapi?huu WIZI?

8. CAG anatuambia kwamba Serikali yako ilikuwa inawadanganya watanzania kwamba TRA inakusanya mapato na kuvuka malengo !lakini tukiwaambia mtupe mchanganuo wa mapato husika , milikuwa mnapiga danadana…leo CAG amewaumbua na kutuambia kwamba mapitio ya hesabu jumuifu yalibainisha kwamba TRA iliwadanya WATANZANIA iliposema mapato ya kodi yamefikia kuwa shilingi 15,094,949,741,000 (Trillion 15). Ilhali ikijua kwamba Kiasi kinajumuisha kodi iliyokusanywa na TRA kwa niaba ya TAASISI nyingine shilingi 2,165,273,630,236 (Trillion 2.1)..

Mtukufu… UNAAMINI KWELI umeinyosha NCHI? Na hapa sijazungumzika kabisa DENI la TAIFA linalolitafuna TAIFA kimya kimya…Nikuhakikishie tu, waBUNGE , hata kama tutabaki 10 tutafanya kazi yetu ipasavyo! ….CHUTAMA….usitishe watu! HAKUNA mwenye HATIMILIKI YA Tanzania!! WATANZANIA AMKENI, USINGIZI WENU WA PONO unaligharimu TAIFA [HASHTAG]#RUDISHA[/HASHTAG] PESA YETU

HALIMA MDEE(MB)

MBUNGE -JIMBO LA KAWE

WAZIRI KIVULI : FEDHA NA MIPANGO

MWENYEKITI BAWACHA TAIFA
Kama Mbunge wa upinzani, umefanyakazi nzuri, tatizo ni lugha ya uandishi. Kwa wadhifa wa mbunge, ulitakiwa utumie lugha ya 'citicism' tatizo kubwa ni lugha ya kuzomea. Yako wapi, mbona umeshindwa, serikali yako iko wapi, nk. Hii inapelekea suala hili liwe ni la kisiasa badala ya kitaalamu. Ukishazomea, rais na watu wake wanazomea, sisi wa pembeni tufanye nini?

Maoni yangu ingekuwa ni kuwa positive. Kwa mfano unapoeleza juu ya matumizi ktk matibabu, ulitakiwa ueleze na kutoa pendekezo. Pendekeza waliohusika wachukuliwe hatua. Badala yake unamzomea rais kwa kusema umeinyoosha nchi kweli? Kwa maana nyingine unataka ainyooshe nchi. Ktk lengo hilo la kuinyoosha nchi, rais huyu sasa anaweza akainyoosha hasa na kuanzia hata kwenu ambao munazomeana. Akifanya hayo kilio tena!

Kwa ujumla nionavyo; ninyi wabunge na wanasiasa wengine munadhani kuinyoosha nchi ni kupambana wengine na siyo ninyi wanasiasa. Wizi wenu hamzungumzii. Malipo muliyojilipa miaka mingi bungeni kwa kuchukuwa posho za vikao na zile za kujikimu kwa kila siku na kamati zenu hamtaki kusema ni wizi, bahasha za wizara mulizopokea miaka mingi hamzungumzii. Tulioko pembeni hata ninyi kwetu ni shida na manufaa yenu hayaendani na faida kwa mwananchi. Siasa isiwe ni taaluma, ifanyeni iwe wito kama ambavyo mumewaambia waalimu, madaktari na mananesi.
 
Binafsi mm sio mwana siasa ,mm ni mwalim na huwa sishabikii chama chochote na angalia mtu nikimuelewa napiga kura.Ila kwa elim yangu ndogo nilio nayo rais wetu mambo mengi anaharibu kwa sababu ya ubabe.Mm naangalia huku nilipo kwenye elim mambo yameharibika mnoo pesa ni ndogo mnoo anayoitoa,walianzisha sera ya wanafunzi waishie drs la sita hawajawah kuleta vitabu wanasema fanya vyovyote masomo yafunishwe.

Leo huku mitihani ya wilaya na mikoa tunaandika ubaoni,wastaafu wengi wanadai mafao yao,kibaya zaidi wanakuja kutulisha viapo eti ole wetu watoto wafeli tutakiona.Kwakweli mm nilioko huku nikiona mtu anatetea hii serikali najua yeye kashiba lakini hajui kuna mtoto wa shangazi,mjomba au mdogo wake.

Wengne tulikuwa na moyo wakijitolea kuwa wazalendo tukiiamini mungu atatulipa tunafundisha mpaka basi ili watoto waende vipaj na wengne wafaulu vzri ila shahd ni Allah tumekataa tamaa mpaka basi.Rais abadilike bwana hata mungu hampendi mtu jeuri na mwenye kibri akubali kusikiliza ushauri wa watu jamani.
Sijui unafundisha ngazi gani, nami naelewa elimu kuna tatizo. Lakini kuna tatizo pia upande wa waalimu na viongozi wenu. Waalimu ni moja ya kada inayotumika ktk usimamizi wa kupiga kura. Rais aliyepita aliwahi kusema hata kura zenu (wafanyakazi) hazihitaji! Bado wafanyakazi hao hao walitoa kura. Elimu shuleni ilianza kwenda hovyo siku nyingi na kwa sasa muelekeo ulikuwa ni kama kila shule ina sera yake. Watu binafsi wanaamua kukusanya makaratasi na kuyaita vitabu. Wizara ilikuwepo, kimya!! Mashuleni mukaendesha michango ya lazima baadhi wakashindwa kwenda shule kwa kukosa hata mchango wa kumuandikisha mtoto.

Siasa zetu mbovu na tabia yetu mbovu vyote vinachangia. Angalia hicho chama chenu munachoita chama cha waalimu. Miaka yote ni wizi tu. Chama cha waalimu kimegeuka kuwa ni chama cha waalimu Dar tu! Kila kiongozi anahamia Dar, vitega uchumi ni Dar! Utetezi wa waalimu, zero, sifuri. Tunageukana.
 
RAIS MAGUFULI, SERIKALI YAKO IMECHAFUKA,CHUTAMA UWEZE KUJISITIRI!

NDUGU RAIS naona Trillion 1.5 imekutoa mafichoni, CAG ameivua nguo SERIKALI yako! CHUTAMA uweze kujisitiri !! USITISHE WATU!

Nasema na wewe nikiwa nina kumbukumbu ya kukamatwa na vyombo vyako vya usalama SAA TISA ALFAJIRI (31/3/2018) na kuwekwa ‘lock up’ kwa SIKU TATU nikiwa nimetoka kwenye MATIBABU! Naandika nikifahamu vyombo vyako vya DOLA vitakuja ‘kunikamata’ tena kwa kuwa MTUKUFU umetoa AMRI kwamba yeyote atakayezungumzia suala la shilingi Trillion 1.5 kama lilivyoainishwa kwenye ripoti ya CAG akamatwe na afungwe!! Ngoja tuseme ili utukamate na kutufunga vizuri!!

Nimekusikia JANA kupitia vyombo vya habari ukinukuliwa ukisema “ kuna ugonjwa tumeupata sisi watanzania wa kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli,sasa sijui huu ugonjwa umetoka wapi,lakini ni kwa sababu hii itandao hatuicontrol sisi….ndio maana mkienda katika nchi kam China sina uhakika kama wana google na whatsApp kama tulizonazo sisi” mwisho wa kunukuu!! Ndugu Rais hapa sitajadili kama CHINA wana GOOGLE au whatsApp’ nikitambua kwamba toka umetangazwa na Tume ta Taifa ya uchaguzi kama ‘mshindi halali’ wa Urais umegoma kabisa kusafiri kwenda NJE YA MIPAKA YA AFRIKA MASHARIKI na Kati..ukidai unaiNYOOSHA NCHI.

Kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu sana kwako kujua kama China ‘wana GOOGLE au WHATSAPP’ Mara ya kwanza nilidhani husafiri kwa sababu ya gharama, nikaja nikagundua kwamba gharama ilikuwa ni POROJO pale ulipoamua kumtuma MAKAMU WAKO WA Rais akuwakilishe kwenye mikutano mbalimbali ya KIMATAIFA inayokutaka wewe kama MKUU wa Nchi kukutana na wakuu wa Nchi wenzako kujadili mambo MAZITO yatakayoiletea neema Nchi yetu!

Ndugu Rais natambua hasira zako dhidi ya ‘Google na whatsapp’…nadhani hapa ulikuwa una maanisha ‘mitandao ya kijamii’! kutokana na ukweli kwamba umeshindwa kuvidhibiti kama ambavyo umefanikiwa kuvidhibiti vyombo vikuu vya habari! Huku kwenye mitandao ya kijamii watu wako huru, hawataki kulishwa matango pori ambayo wewe unatamani watanzania walishwe! Kwa lugha nyingine watanzania wanataka kujiepusha na ugonjwa wa kuamini kila SERIKALI yako inachokisema..

Jana tumekushuhudia ukimsimamisha CAG na kumuuliza kama kwenye ripoti yake kuna pahala ameandika kuna shilingi trillion 1.5 zilizoibiwa , kisha ukamuuliza na MTOTO wako Katibu Mkuu wa wizara ya FEDHA kama NCHI imeibiwa …. NAE akakupa jibu “hapana Mheshimiwa” ….SIJUI ULITARAJIA MTOTO atampa jibu gani BABA….

NDUGU RAIS NINA MAMBO 8 AMBAYO NATAKA UYASOME NA KUYAELEWA..KISHA UTAJIJIBU MWENYEWE KAMA UMEFANIKIWA KUINYOOSHA NCHI….AU NCHI IMEKUNYOOSHA….

1. Alichokisema CAG kwenye ukurasa wake wa 34 ,nanukuu “ Kati ya shilingi bilioni 25,307.8 zilizokusanywa , shilingi bilioni 23.792 zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi , matumizi mengine ,matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatokananayo na amana za serikali pamoja na riba’ CAG hawezi sema pesa zimeibwa au la…anachotuambia SISI wananchi ni kwamba mpaka mwaka wa fedha unaisha 30 Juni 2017. Na mpaka anawasilisha ripoti yake kwako Mwezi Machi 2018 kulikuwa kuna bakaa la shilingi Trillion 1.5 ambalo halijulikani limefanya kazi gani !Mpaka sasa si wewe wala WASAIDIZI wako walioweza kujibu ,

Kwa kuwa taarifa imeshapita kwako na wewe ukatoa idhini iletwe mbele ya BUNGE, tunaomba MTUACHIE wabunge tufanye kazi yetu!! UMELIZIMA BUNGE….HUWEZI ZIMA FIKRA YAKINIFU

2. CAG anasema nchi imeshindwa kupata mapato ya kodi yenye thamani ya shilingi trillion 4.44 kutokana na ufanisi mdogo wa baraza la rufaa la kodi na Mahakama ya rufaa kutokana na upungufu wa makamu wenyeviti na wajumbe wa bodi zake hali inayopelekea kushindikana kufanya vikao vya kutosha hivyo serikali kukosa mapato!

3. CAG anasema TRA haikukusanya kodi yenye thamani ya shilingi 1,827,720,075,433.35 (Trillion 1.8 ) kutokana na mapingamizi ya kodi ambayo yalikwisha shughulikiwa na kukamilishwa. Hivi zile ziara zako za kushtukiza na za mara kwa mara TRA zimezaa matunda kweli??

4. CAG anatuambia serikali yako haifuati SHERIA ya Manunuzi ya UMMA na KANUNI zake wakati wa kufanya MANUNUZI, ameeleza wazi kabisa moja ya manunuzi yaliyofanyika bila kufuata sheria ya manunuzi , ni manunuzi ya ile ndege ya Q400 BOMBANDIER yenye thamani ya shilingi Bilioni 51.838 uliyoipigia upatu kwamba umelipa CASH kama vile unatoa fedha zako mfukoni !SISI WAKONGWE TUNAJUA mara nyingi DILI za NAMNA HII zina harufu za wizi na ufisadi

5. CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka kutoka shilingi (Bilioni 28.6 mpaka shilingi Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika kipindi cha UTAWALA wako matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe.Lissu mmegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!

Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”

6. CAG anatuambia kwamba SERIKALI yako ilikopa ndani zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa 10/08%. Kitendo hiki mbali na kuwa kinyume na sheria kina athari kubwa kwa wakopaji wengine(wafanyabiashara)kwani sehemu kubwa ya mtaji wa mabenki unakuwa umefungwa kwenye fedha walizokopesha Serikali kwa muda mfupi na muda mrefu. Matokeo yake , riba ya kukopesha kwa watu binafsi inakuwa kubwa na gharama ya maisha inakuwa juu!

7. CAG anatuambia kwamba Serikali IMEPORA akiba za mamilioni ya WASTAAFU waliotumia jasho na damu yao kulitumikia Taifai ! IMEKOPA MIFUKO ya HIFADHI shilingi bilioni 5,343 (Trillion 5.3) na kuamrisha ilipwe shilingi bilioni 3,183 (Trillion 3.1). Serikali ituambie ,shilingi bilioni 2,160 (Trillion 2.1) ziko wapi?huu WIZI?

8. CAG anatuambia kwamba Serikali yako ilikuwa inawadanganya watanzania kwamba TRA inakusanya mapato na kuvuka malengo !lakini tukiwaambia mtupe mchanganuo wa mapato husika , milikuwa mnapiga danadana…leo CAG amewaumbua na kutuambia kwamba mapitio ya hesabu jumuifu yalibainisha kwamba TRA iliwadanya WATANZANIA iliposema mapato ya kodi yamefikia kuwa shilingi 15,094,949,741,000 (Trillion 15). Ilhali ikijua kwamba Kiasi kinajumuisha kodi iliyokusanywa na TRA kwa niaba ya TAASISI nyingine shilingi 2,165,273,630,236 (Trillion 2.1)..

Mtukufu… UNAAMINI KWELI umeinyosha NCHI? Na hapa sijazungumzika kabisa DENI la TAIFA linalolitafuna TAIFA kimya kimya…Nikuhakikishie tu, waBUNGE , hata kama tutabaki 10 tutafanya kazi yetu ipasavyo! ….CHUTAMA….usitishe watu! HAKUNA mwenye HATIMILIKI YA Tanzania!! WATANZANIA AMKENI, USINGIZI WENU WA PONO unaligharimu TAIFA [HASHTAG]#RUDISHA[/HASHTAG] PESA YETU

HALIMA MDEE(MB)

MBUNGE -JIMBO LA KAWE

WAZIRI KIVULI : FEDHA NA MIPANGO

MWENYEKITI BAWACHA TAIFA

Hivi wapiga kura wa Kawe wanajisikiaje mbunge wao anatukanana matusi ya nguoni na Rais? What is chutama? Kama CAG anasema serkali imekusanya 100 jmetumia 80, kwa nini useme 20 zimeibiwa badala ya kusema bado tu hazijatumika? CAG akisema TRA imekusan6a 10, zikiwama 3 za TANROADS, kuna ubaya gani, si wamekusanya? Hizo za matibabu CAG amesema zimetumika, kuna ubaya gani, si wametibiwa Watanzania kina Ndugai kina James Mbatiya kina Professor Mwandosya? Kwa nini inakuuma? Wewe mwenyewe ulienda kutibiwa Afrika ya Kusini kama nawe ungeenda India si gjarama ingekuwa kubwa zaifi? Mbona hukudai haki yako ya kibunge ulipiwe?
 
Tatizo la wabunge wote wa upinzani na chama tawala imekuwa ni imani kwamba wao ni watu muhimu sana ktk nchi hii. Wanaamini kila wasemalo tunafuata. Imani za aina hiyo ziko hadi juu kwa mawaziri. Mtu akishakuwa waziri anaamini sasa anaelewa kila kitu kuliko yeyote. Sasas hivi wanalazimisha kutushirikisha ripoti ya CAG wakati sisi hatuna nafasi ya kuisoma, kwa nini watusomee wao? hebu tuombe iwekwe mtandaoni ili nasi tuisome mbona wabunge wengi muko chini ya kiwango chetu?

Itakuwa ni bahati mbaya kuendelea kuwategemea wabunge kutusimulia mambo ambayo hata sisi tunaweza kuyaelewa wenyewe.
 
Ktk manunuzi ya wapinzani hili lilitegemewa kuwa kuna mahali fedha zinatoka na ilisemwa ni 'jambo la muda tu' sasa ndio yanaanza kutoka moja baada ya jingine.
 
Mkuu unafahamu kwamba bado kutakuwa na kikao kati ya CAG pamoja na wabunge kuhusiana na masuala ya hizi fedha?.

Yaani unataka serikali ifanye kazi kwa taratibu za akili za mtu binafsi!!!?. Hakuna kitu kama hicho duniani.

Ukiishi kwa kuendekeza udaku lazima udaku huo ulete athari hata kwenye mitazamo yako.

nyie ndio mnataka mambo yafanywe kienyeji, mbona mnageuza mambo?
 
Nimeishia darasa la kawaida

UK wa 34, unaonesha mapato yaliyokusanywa na yaliyotumika , lakini haioneshi ambacho hakionekani kimeenda wapi ?

Yaani , maelezo ya kuwa yameenda wapi na serikali imejibu maana wao ndio walikuwa wakaguliwa

Wewe , mwenye taarifa pesa zilipo naomba utusaidie maana Serikali imeshatoa majibu yake basi yapinge kwa kuonesha sivyo
Serikali haikuwa na majibu wakati wa ukaguzi na hata walipopewa 21 days za kutoa majibu either hawakuwa na majibu au hayakuwa yanaridhisha na ndio maana report ikaandikwa bila hizo 1.5 Tr kuwa na maelezo ya matumizi yake. Majibu ya leo ya serikali yalipaswa kuwasilishwa kabla ya kuandika report hii ili yafanyiwe audit. Kwa hiyo majibu ya serikali sio audited ni bla bla tu.

Bado shule ndio tatizo, sio kitu kingine.
 
Mdee mwambie Mwenyekiti pendwa achutame mtueleze 7 billion za ruzuku zimetumikaje maana kama unaongelea report ya CAG ajaacha kitu.

Tusipende kuchambua report ya CAG nusu nusu au sehemu ambazo mbaya kwa mwenzako. Kama kweli ulikuwa na nia ya dhati kuongelea kuhusu hii report ungetoa ushauri sehemu zote zilizoguswa kwenye report ya CAG.
Hapo hawawezi kupazungumzia hata kidogo.
 
Hakim a hakuna cha maana ulichoandika japo wapo wanaokushabikia.
Kuhusu kukamatwa ukifanya makosa lazima utakamatwa tuu sidhani eti kutoa taarifa in advance Kama mbinu kitakusaidia.
JPM ni jembe na Watanzania wengi wanamjubali.
Pole
 
Hivi wapiga kura wa Kawe wanajisikiaje mbunge wao anatukanana matusi ya nguoni na Rais? What is chutama? Kama CAG anasema serkali imekusanya 100 jmetumia 80, kwa nini useme 20 zimeibiwa badala ya kusema bado tu hazijatumika? CAG akisema TRA imekusan6a 10, zikiwama 3 za TANROADS, kuna ubaya gani, si wamekusanya? Hizo za matibabu CAG amesema zimetumika, kuna ubaya gani, si wametibiwa Watanzania kina Ndugai kina James Mbatiya kina Professor Mwandosya? Kwa nini inakuuma? Wewe mwenyewe ulienda kutibiwa Afrika ya Kusini kama nawe ungeenda India si gjarama ingekuwa kubwa zaifi? Mbona hukudai haki yako ya kibunge ulipiwe?
Mkuu WILLIAM, akili za mheshimiwa ndio zile zile za bangi na viroba.

Ila awamu ya tano haitaki ujinga, aliwahi huyo kutukana halafu akakamatwa na mkuu wa wilaya tu, haikuhitajika kauli ya RC.
 
Taratibu mleta mda unaanza kueleweka.Mpaka 2020 tunaweza kujitathmini vizuri
 
Back
Top Bottom