Halima Mdee: Rais Magufuli, Serikali yako imechafuka, chutama uweze kujisitiri

Halima Mdee

New Member
Feb 5, 2012
4
172
RAIS MAGUFULI, SERIKALI YAKO IMECHAFUKA,CHUTAMA UWEZE KUJISITIRI!

NDUGU RAIS naona Trillion 1.5 imekutoa mafichoni, CAG ameivua nguo SERIKALI yako! CHUTAMA uweze kujisitiri !! USITISHE WATU!

Nasema na wewe nikiwa nina kumbukumbu ya kukamatwa na vyombo vyako vya usalama SAA TISA ALFAJIRI (31/3/2018) na kuwekwa ‘lock up’ kwa SIKU TATU nikiwa nimetoka kwenye MATIBABU! Naandika nikifahamu vyombo vyako vya DOLA vitakuja ‘kunikamata’ tena kwa kuwa MTUKUFU umetoa AMRI kwamba yeyote atakayezungumzia suala la shilingi Trillion 1.5 kama lilivyoainishwa kwenye ripoti ya CAG akamatwe na afungwe!! Ngoja tuseme ili utukamate na kutufunga vizuri!!

Nimekusikia JANA kupitia vyombo vya habari ukinukuliwa ukisema “ kuna ugonjwa tumeupata sisi watanzania wa kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli,sasa sijui huu ugonjwa umetoka wapi,lakini ni kwa sababu hii itandao hatuicontrol sisi….ndio maana mkienda katika nchi kam China sina uhakika kama wana google na whatsApp kama tulizonazo sisi” mwisho wa kunukuu!! Ndugu Rais hapa sitajadili kama CHINA wana GOOGLE au whatsApp’ nikitambua kwamba toka umetangazwa na Tume ta Taifa ya uchaguzi kama ‘mshindi halali’ wa Urais umegoma kabisa kusafiri kwenda NJE YA MIPAKA YA AFRIKA MASHARIKI na Kati..ukidai unaiNYOOSHA NCHI.

Kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu sana kwako kujua kama China ‘wana GOOGLE au WHATSAPP’ Mara ya kwanza nilidhani husafiri kwa sababu ya gharama, nikaja nikagundua kwamba gharama ilikuwa ni POROJO pale ulipoamua kumtuma MAKAMU WAKO WA Rais akuwakilishe kwenye mikutano mbalimbali ya KIMATAIFA inayokutaka wewe kama MKUU wa Nchi kukutana na wakuu wa Nchi wenzako kujadili mambo MAZITO yatakayoiletea neema Nchi yetu!

Ndugu Rais natambua hasira zako dhidi ya ‘Google na whatsapp’…nadhani hapa ulikuwa una maanisha ‘mitandao ya kijamii’! kutokana na ukweli kwamba umeshindwa kuvidhibiti kama ambavyo umefanikiwa kuvidhibiti vyombo vikuu vya habari! Huku kwenye mitandao ya kijamii watu wako huru, hawataki kulishwa matango pori ambayo wewe unatamani watanzania walishwe! Kwa lugha nyingine watanzania wanataka kujiepusha na ugonjwa wa kuamini kila SERIKALI yako inachokisema..

Jana tumekushuhudia ukimsimamisha CAG na kumuuliza kama kwenye ripoti yake kuna pahala ameandika kuna shilingi trillion 1.5 zilizoibiwa , kisha ukamuuliza na MTOTO wako Katibu Mkuu wa wizara ya FEDHA kama NCHI imeibiwa …. NAE akakupa jibu “hapana Mheshimiwa” ….SIJUI ULITARAJIA MTOTO atampa jibu gani BABA….

NDUGU RAIS NINA MAMBO 8 AMBAYO NATAKA UYASOME NA KUYAELEWA..KISHA UTAJIJIBU MWENYEWE KAMA UMEFANIKIWA KUINYOOSHA NCHI….AU NCHI IMEKUNYOOSHA….

1. Alichokisema CAG kwenye ukurasa wake wa 34 ,nanukuu “ Kati ya shilingi bilioni 25,307.8 zilizokusanywa , shilingi bilioni 23.792 zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi , matumizi mengine ,matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatokananayo na amana za serikali pamoja na riba’ CAG hawezi sema pesa zimeibwa au la…anachotuambia SISI wananchi ni kwamba mpaka mwaka wa fedha unaisha 30 Juni 2017. Na mpaka anawasilisha ripoti yake kwako Mwezi Machi 2018 kulikuwa kuna bakaa la shilingi Trillion 1.5 ambalo halijulikani limefanya kazi gani !Mpaka sasa si wewe wala WASAIDIZI wako walioweza kujibu ,

Kwa kuwa taarifa imeshapita kwako na wewe ukatoa idhini iletwe mbele ya BUNGE, tunaomba MTUACHIE wabunge tufanye kazi yetu!! UMELIZIMA BUNGE….HUWEZI ZIMA FIKRA YAKINIFU

2. CAG anasema nchi imeshindwa kupata mapato ya kodi yenye thamani ya shilingi trillion 4.44 kutokana na ufanisi mdogo wa baraza la rufaa la kodi na Mahakama ya rufaa kutokana na upungufu wa makamu wenyeviti na wajumbe wa bodi zake hali inayopelekea kushindikana kufanya vikao vya kutosha hivyo serikali kukosa mapato!

3. CAG anasema TRA haikukusanya kodi yenye thamani ya shilingi 1,827,720,075,433.35 (Trillion 1.8 ) kutokana na mapingamizi ya kodi ambayo yalikwisha shughulikiwa na kukamilishwa. Hivi zile ziara zako za kushtukiza na za mara kwa mara TRA zimezaa matunda kweli??

4. CAG anatuambia serikali yako haifuati SHERIA ya Manunuzi ya UMMA na KANUNI zake wakati wa kufanya MANUNUZI, ameeleza wazi kabisa moja ya manunuzi yaliyofanyika bila kufuata sheria ya manunuzi , ni manunuzi ya ile ndege ya Q400 BOMBANDIER yenye thamani ya shilingi Bilioni 51.838 uliyoipigia upatu kwamba umelipa CASH kama vile unatoa fedha zako mfukoni !SISI WAKONGWE TUNAJUA mara nyingi DILI za NAMNA HII zina harufu za wizi na ufisadi

5. CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka kutoka shilingi (Bilioni 28.6 mpaka shilingi Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika kipindi cha UTAWALA wako matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe.Lissu mmegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!

Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”

6. CAG anatuambia kwamba SERIKALI yako ilikopa ndani zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa 10/08%. Kitendo hiki mbali na kuwa kinyume na sheria kina athari kubwa kwa wakopaji wengine(wafanyabiashara)kwani sehemu kubwa ya mtaji wa mabenki unakuwa umefungwa kwenye fedha walizokopesha Serikali kwa muda mfupi na muda mrefu. Matokeo yake , riba ya kukopesha kwa watu binafsi inakuwa kubwa na gharama ya maisha inakuwa juu!

7. CAG anatuambia kwamba Serikali IMEPORA akiba za mamilioni ya WASTAAFU waliotumia jasho na damu yao kulitumikia Taifai ! IMEKOPA MIFUKO ya HIFADHI shilingi bilioni 5,343 (Trillion 5.3) na kuamrisha ilipwe shilingi bilioni 3,183 (Trillion 3.1). Serikali ituambie ,shilingi bilioni 2,160 (Trillion 2.1) ziko wapi?huu WIZI?

8. CAG anatuambia kwamba Serikali yako ilikuwa inawadanganya watanzania kwamba TRA inakusanya mapato na kuvuka malengo !lakini tukiwaambia mtupe mchanganuo wa mapato husika , milikuwa mnapiga danadana…leo CAG amewaumbua na kutuambia kwamba mapitio ya hesabu jumuifu yalibainisha kwamba TRA iliwadanya WATANZANIA iliposema mapato ya kodi yamefikia kuwa shilingi 15,094,949,741,000 (Trillion 15). Ilhali ikijua kwamba Kiasi kinajumuisha kodi iliyokusanywa na TRA kwa niaba ya TAASISI nyingine shilingi 2,165,273,630,236 (Trillion 2.1)..

Mtukufu… UNAAMINI KWELI umeinyosha NCHI? Na hapa sijazungumzika kabisa DENI la TAIFA linalolitafuna TAIFA kimya kimya…Nikuhakikishie tu, waBUNGE , hata kama tutabaki 10 tutafanya kazi yetu ipasavyo! ….CHUTAMA….usitishe watu! HAKUNA mwenye HATIMILIKI YA Tanzania!! WATANZANIA AMKENI, USINGIZI WENU WA PONO unaligharimu TAIFA [HASHTAG]#RUDISHA[/HASHTAG] PESA YETU

HALIMA MDEE(MB)

MBUNGE -JIMBO LA KAWE

WAZIRI KIVULI : FEDHA NA MIPANGO

MWENYEKITI BAWACHA TAIFA
 
Attachments

  • HALIMA MDEE.pdf
    135.5 KB · Views: 85
uchambuzi mzuri sana, Sasa subiri video nyingine ya CAG wa Lumumba aliyepata ile ya kwanza kidato cha sita
Hahahaha mwambie asipotoshe report ya CAG
tapatalk_1524209741975.jpeg
 
Mdee mwambie Mwenyekiti pendwa achutame mtueleze 7 billion za ruzuku zimetumikaje maana kama unaongelea report ya CAG ajaacha kitu.

Tusipende kuchambua report ya CAG nusu nusu au sehemu ambazo mbaya kwa mwenzako. Kama kweli ulikuwa na nia ya dhati kuongelea kuhusu hii report ungetoa ushauri sehemu zote zilizoguswa kwenye report ya CAG.
 
CHADEMA katika ubora wao wa kutumia mitandao ya habari. Unapofika wakati wa uchaguzi wale wapiga kura huwa hawaangalii mwanasiasa katika kipindi cha miaka mitano ameandika makala ngapi kwenye facebook, Twitter au Instagram.

Wao wanapima maendeleo halisi, kwa kutazama kipi kipya kimeletwa na mbunge kwenye jimbo lao.

Halima Mdee anapoteza nguvu zake mbele ya keyboard, wapiga kura wa Kawe hatutazama amefungua uzi mara ngapi mitandaoni, awe muangalifu sana.
 
Duuh .majibu ya maswali haya ni mitandao kudhibitiwa .usajili umetangazwa rasmi .ghafla tunarudishwa mwaka 1958 napo ilikuwa heri
 
Tuige basi china wanavyopiga risasi mafisadi hadharani.

Natahadharisha tena, uchaguzi ujao, sioni jimbo lolote likirudi upinzani, kwa namna yeyote ile, kwa hila, halali, vita, nguvu, mabavu au namna yeyote ile.

Upinzani wabadili mtindo wa siasa zao. Tujikumbushe kwenye chaguzi za marudio na hii kamatakamata ya viongozi wa upinzani.

Inamaana hata hizi sheria za kutoza ada wamiliki wa blogs na online TV ni mwendelezo wa kuiga China.
 
NDUGU RAIS naona Trillion 1.5 imekutoa mafichoni, CAG ameivua nguo SERIKALI yako! CHUTAMA uweze kujisitiri !! USITISHE WATU! Nasema na wewe nikiwa nina kumbukumbu ya kukamatwa na vyombo vyako vya usalama SAA TISA ALFAJIRI (31/3/2018) na kuwekwa ‘lock up’ kwa SIKU TATU nikiwa nimetoka kwenye MATIBABU! Naandika nikifahamu vyombo vyako vya DOLA vitakuja ‘kunikamata’ tena kwa kuwa MTUKUFU umetoa AMRI kwamba yeyote atakayezungumzia suala la shilingi Trillion 1.5 kama lilivyoainishwa kwenye ripoti ya CAG akamatwe na afungwe!! Ngoja tuseme ili utukamate na kutufunga vizuri!!

Nimekusikia JANA kupitia vyombo vya habari ukinukuliwa ukisema “ kuna ugonjwa tumeupata sisi watanzania wa kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli,sasa sijui huu ugonjwa umetoka wapi,lakini ni kwa sababu hii itandao hatuicontrol sisi….ndio maana mkienda katika nchi kam China sina uhakika kama wana google na whatsApp kama tulizonazo sisi” mwisho wa kunukuu!! Ndugu Rais hapa sitajadili kama CHINA wana GOOGLE au whatsApp’ nikitambua kwamba toka umetangazwa na Tume ta Taifa ya uchaguzi kama ‘mshindi halali’ wa Urais umegoma kabisa kusafiri kwenda NJE YA MIPAKA YA AFRIKA MASHARIKI na Kati..ukidai unaiNYOOSHA NCHI.

Kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu sana kwako kujua kama China ‘wana GOOGLE au WHATSAPP’ Mara ya kwanza nilidhani husafiri kwa sababu ya gharama, nikaja nikagundua kwamba gharama ilikuwa ni POROJO pale ulipoamua kumtuma MAKAMU WAKO WA Rais akuwakilishe kwenye mikutano mbalimbali ya KIMATAIFA inayokutaka wewe kama MKUU wa Nchi kukutana na wakuu wa Nchi wenzako kujadili mambo MAZITO yatakayoiletea neema Nchi yetu!

Ndugu Rais natambua hasira zako dhidi ya ‘Google na whatsapp’…nadhani hapa ulikuwa una maanisha ‘mitandao ya kijamii’! kutokana na ukweli kwamba umeshindwa kuvidhibiti kama ambavyo umefanikiwa kuvidhibiti vyombo vikuu vya habari! Huku kwenye mitandao ya kijamii watu wako huru, hawataki kulishwa matango pori ambayo wewe unatamani watanzania walishwe! Kwa lugha nyingine watanzania wanataka kujiepusha na ugonjwa wa kuamini kila SERIKALI yako inachokisema..

Jana tumekushuhudia ukimsimamisha CAG na kumuuliza kama kwenye ripoti yake kuna pahala ameandika kuna shilingi trillion 1.5 zilizoibiwa , kisha ukamuuliza na MTOTO wako Katibu Mkuu wa wizara ya FEDHA kama NCHI imeibiwa …. NAE akakupa jibu “hapana Mheshimiwa” ….SIJUI ULITARAJIA MTOTO atampa jibu gani BABA….
Ndugu RAIS NINA mambo 8 ambayo nataka UYASOME na kuyaelewa..KISHA utajijibu mwenyewe kama UMEFANIKIWA kuinyoosha NCHI….au

NCHI Imekunyoosha….
Alichokisema CAG kwenye ukurasa wake wa 34 ,nanukuu “ Kati ya shilingi bilioni 25,307.8 zilizokusanywa , shilingi bilioni 23.792 zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi , matumizi mengine ,matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatokananayo na amana za serikali pamoja na riba’ CAG hawezi sema pesa zimeibwa au la…anachotuambia SISI wananchi ni kwamba mpaka mwaka wa fedha unaisha 30 Juni 2017. Na mpaka anawasilisha ripoti yake kwako Mwezi Machi 2018 kulikuwa kuna bakaa la shilingi Trillion 1.5 ambalo halijulikani limefanya kazi gani !Mpaka sasa si wewe wala WASAIDIZI wako walioweza kujibu ,

Kwa kuwa taarifa imeshapita kwako na wewe ukatoa idhini iletwe mbele ya BUNGE, tunaomba MTUACHIE wabunge tufanye kazi yetu!! UMELIZIMA BUNGE….HUWEZI ZIMA FIKRA YAKINIFU

CAG anasema nchi imeshindwa kupata mapato ya kodi yenye thamani ya shilingi trillion 4.44 kutokana na ufanisi mdogo wa baraza la rufaa la kodi na Mahakama ya rufaa kutokana na upungufu wa makamu wenyeviti na wajumbe wa bodi zake hali inayopelekea kushindikana kufanya vikao vya kutosha hivyo serikali kukosa mapato!

CAG anasema TRA haikukusanya kodi yenye thamani ya shilingi 1,827,720,075,433.35 (Trillion 1.8 ) kutokana na mapingamizi ya kodi ambayo yalikwisha shughulikiwa na kukamilishwa. Hivi zile ziara zako za kushtukiza na za mara kwa mara TRA zimezaa matunda kweli??

CAG anatuambia serikali yako haifuati SHERIA ya Manunuzi ya UMMA na KANUNI zake wakati wa kufanya MANUNUZI, ameeleza wazi kabisa moja ya manunuzi yaliyofanyika bila kufuata sheria ya manunuzi , ni manunuzi ya ile ndege ya Q400 BOMBANDIER yenye thamani ya shilingi Bilioni 51.838 uliyoipigia upatu kwamba umelipa CASH kama vile unatoa fedha zako mfukoni !SISI WAKONGWE TUNAJUA mara nyingi DILI za NAMNA HII zina harufu za wizi na ufisadi

CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka kutoka shilingi (Bilioni 28.6 mpaka shilingi Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika kipindi cha UTAWALA wako matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe.Lissu mmegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!

Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”

CAG anatuambia kwamba SERIKALI yako ilikopa ndani zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa 10/08%. Kitendo hiki mbali na kuwa kinyume na sheria kina athari kubwa kwa wakopaji wengine(wafanyabiashara)kwani sehemu kubwa ya mtaji wa mabenki unakuwa umefungwa kwenye fedha walizokopesha Serikali kwa muda mfupi na muda mrefu. Matokeo yake , riba ya kukopesha kwa watu binafsi inakuwa kubwa na gharama ya maisha inakuwa juu!

CAG anatuambia kwamba Serikali IMEPORA akiba za mamilioni ya WASTAAFU waliotumia jasho na damu yao kulitumikia Taifai ! IMEKOPA MIFUKO ya HIFADHI shilingi bilioni 5,343 (Trillion 5.3) na kuamrisha ilipwe shilingi bilioni 3,183 (Trillion 3.1). Serikali ituambie ,shilingi bilioni 2,160 (Trillion 2.1) ziko wapi?huu WIZI?

CAG anatuambia kwamba Serikali yako ilikuwa inawadanganya watanzania kwamba TRA inakusanya mapato na kuvuka malengo !lakini tukiwaambia mtupe mchanganuo wa mapato husika , milikuwa mnapiga danadana…leo CAG amewaumbua na kutuambia kwamba mapitio ya hesabu jumuifu yalibainisha kwamba TRA iliwadanya WATANZANIA iliposema mapato ya kodi yamefikia kuwa shilingi 15,094,949,741,000 (Trillion 15). Ilhali ikijua kwamba Kiasi kinajumuisha kodi iliyokusanywa na TRA kwa niaba ya TAASISI nyingine shilingi 2,165,273,630,236 (Trillion 2.1)..

Mtukufu… UNAAMINI KWELI umeinyosha NCHI? Na hapa sijazungumzika kabisa DENI la TAIFA linalolitafuna TAIFA kimya kimya…Nikuhakikishie tu, waBUNGE , hata kama tutabaki 10 tutafanya kazi yetu ipasavyo! ….CHUTAMA….usitishe watu! HAKUNA mwenye HATIMILIKI YA Tanzania!! WATANZANIA AMKENI, USINGIZI WENU WA PONO unaligharimu TAIFA [HASHTAG]#RUDISHA[/HASHTAG] PESA YETU

HALIMA MDEE(MB)
MBUNGE -JIMBO LA KAWE
WAZIRI KIVULI : FEDHA NA MIPANGO
MWENYEKITI BAWACHA TAIFA
mdee.jpg
 
Back
Top Bottom