Halima Mdee: ⁦⁦Rais Magufuli hivi unajua ⁩biashara ya wabunge wa Ukonga na Monduli tu iligharimu taifa Shilingi 12,449,659,588.00 ?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,916
2,000
Hizo zingeenda ujenzi wa madarasa watoto wangeshindwa leo kuanza kidato cha kwanza kwa kukosa madarasa? Juha kwa kukosa akili anaweza kulazimika kutembea Dar to Moro kwa sababu 20,000/ yake ya nauli kaitumia kunywea pombe Bar ili kutaka walevi wamsifu.
Hii serikali inapenda sifa Kama za majuha
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,274
2,000
⁦⁦@Magufuli JP hivi unajua ⁩ BIASHARA ya wabunge wa UKONGA na Monduli TU!!ililagharimu TAIFA shilingi 12,449,659,588.00 ?
Duh! Hapa ndipo mtu unabaki unajiuliza maswali yasiyo na majibu. Idadi ya Wabunge wa CCM ndani ya Bunge la Ndugai na Tulia inawawezesha kupitisha sheria yoyote ile hata ikiwa ya hovyo namna gani. Sasa lengo la kutumia mihela yote hiyo kuongeza idadi ya Wabunge wa aina hiyo hiyo ni nini kama si kuhalalisha ufisadi na kuimarisha udikteta?

Hata kwa akili ya wastani tu, utagundua kuwa lengo ni kuhakikisha hakuna sauti zitakazohoji hili gari letu bovu linatupeleka wapi?Tumeshuhudia wale watundu wasiokubali kuuza nafsi zao kwa kipande cha fedha wakimiminiwa risasi zisizo idadi na wengine kubambikiziwa kesi zisizo na miguu wala kichwa. Je kwa staili hii, wananchi tutegemee nini?
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,124
2,000
Mwenzenu yupo ulaya na america anapigia chapuo demokrasia..ndio demokrasia ilivyo..kwani enzi za jk si mlimpiga chini zitto kabwe..mlidhani asingeenda mahakamani jimbo lake lingefutwa au usingefanyika tena uchaguzi?mbona hamkushtakiwa kwa kutaka kuingiza taifa kwenye hasara..
Ni nyie chadema ndio mliondoka mkagomea mchakato wa katiba mpya huku tayari zikiwa zimeidhinishwa na watu kulipwa billions of shillings, hali iliyopelekea mchakato kusimama...mbona nyie hamkushtakiwa au kama mliona hamtafikia muafaka kwa nini hamkumshauri jk asipitishe mlipokuwa mnaenda ikulu kunywa juisi.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
2,636
2,000
Ina maana kila uchaguzi umetucost kama nchi 4 point kadhaa bilioni kugharamikia chaguzi hizo ambazo kimsingi hazikuwa na sababu iwapo tungekuwa na sheria ya mtu akihama ahame na ubunge wake au kutokuwa na uchaguzi wowote mpk muda wa uchaguzi ufike hata kama mbunge akihama. Nadhani tunahitajika kuliangalia hili kwa umakini kuepusha hasara hii.

Maana kwa idadi ya wabunge waliohama nadhani billion za kutosha zimepotea ambazo kama zingeelekezwa kwenye kununua vifaa vya hospital maisha ya wengi yangeokolewa, kama zingeenda kuboresha elimu wadogo zetu wangesoma Vizuri na kuongeza ufaulu, kama zingeenda kununua vifaa vya uokoaji maisha ya watz wenzetu yasingepotea Kwa excuse ya giza nk
 
Ndio gharama ya demokrasia ndugu..bahati imeback fire upande mmoja ndio maana vilio vingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom