MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,194
Jana katika tukio liliofanyika makao makuu ya CHADEMA, Mheshimiwa Halima Mdoe alikaririwa akitamka serikali imezifunga akaunti zote za benki za Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa Mbowe kwa vile walitarajiwa yeye akiwa na ukwasi mkubwa wa pesa ataweza kulipa faini kwa wote, hivyo muafaka ni kuzifunga akaunti zake pamoja na M-PESA.
Kimsingi sina tatizo na ukwasi wa Mheshimiwa Mbowe, lakini kizungumkuti ni pale Mheshimiwa Halima Mdee alipotutangazia umma ya kuwa yeye binafsi na waheshimiwa wengine Bulaya, Esther Matiko, Mnyika, Msingwa na Heche ambao wote ni wabunge kwenye akaunti zao zina pesa chini ya shilingi milioni moja.
Kwa kifupi serikali ilijua waheshimiwa husika watashindwa kulipa faini na hatimaye kuishia magerezani hatahivyo wananchi wamefanikisha kutoa michango ya kuwalipia wao.
ULAGHAI wa Mheshimiwa Halima Mdee unakuja pale anapoomba michango ya pesa kutoka kwa walala hoi huku waheshimiwa wabunge wakiwa na pato kubwa wao wenyewe hata akaunti zao za benki na raslimali wanazomiliki zina thamani zaidi ya milioni 200 kwa kila mmoja.
Waheshimiwa wabunge wa CHADEMA msitumie umbumbumbu wa wananchi kuwaibia kidogo walichonacho ili kulipia faini zenu, wakati waheshimiwa mna ukwasi mkubwa na pia chama chenu kinapata ruzuku kubwa kila mwezi.
Wananchi wa Tanzania tuachane na michango ya kilaghai badala yake tuwahoji kwanini wao wenye kiasi kikubwa cha pesa leo hii wanalazimisha sisi walalahoi kuwachangia faini kwa wao ambao wana kipato kikubwa kuliko walalahoi!!!