Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Wiki hii, wakati mjadala wa bunge unaendelea, Mbunge wa Kawe Halima Mdee alionyesha tabia za ajabu kabisa.
Alikuwa mkaidi na mwenye kufanya dhihaka zisizo na sababu Wakati waziri mmoja ambaye ni mwanamama mwenzake aliposimama kutaka kuchangia, Halima Mdee akaongea chini chini akisema "huyu naye mmbeya". Alidhani yale maneno hayatasikika, akasahau kuwa kipaza sauti chake hakikuwa kimezimwa.
Halim Mdee una wawakilisha wananchi wa Kawe, jimbo ambalo limejaa watu wenye kuheshimiwa nchini. Haifai kuendeleza tabia za wanafunzi wa darasa la saba au form one, wakati wewe umekwenda bungeni kwa ridhaa ya wanakawe.
Kiburi, dharau kwa watu wanaokizidi umri kama waziri Mwakyembe na wengine wengi, ni muendelezo wa tabia ambazo personally zinaharibu wasifu wako. Utoto wa mjini sehemu yake ni nje ya ukumbi wa bunge, ukiwa ndani ya ukumbi wewe ni mtu muhimu sana, mwenye wajibu wa kutunza heshima na muonekano wa kila mwanakawe.
Punguza siasa za kiuanaharakati, jikite katika siasa za utatuzi wa matatizo ya msingi. Jitahidi uonekane mnyenyekevu hata kama unadhani labda unaonewa au unaishi ndani ya uonevu wakati ukiwa bungeni. Jaribu kuwa mstaarabu, punguza arrogance, punguza majivuno ya kimjini, utapendwa na wengi kama utaondoa ile hali ya wewe kuonekana kila siku upo katika ugomvi na watu fulani. Be friendly and everyone will appreciate your soul