Halima Mdee: Niko imara kuliko jana

Ujasiri walionao viongozi wa CHADEMA ni kwasababu wanafanya kazi ya alie juu(yeye ndio huwapa nguvu na ujasiri-sisi wanadamu sio rahisi kuona/kuelewa hili).

Kupitia CHADEMA,Watanzania mtakombolewa kutoka tawala za CCM.

Mkumbuke hata Yesu aliteswa ili sisi wanadamu tuokolewe.

Hata baada ya Yesu,Mungu ameendelea kutumia wanadamu kusaidia/kuokoa wanadamu wengine.

Ujasiri walionao viongozi wa CHADEMA na viburi walivyonavyo wakubwa,yote haya ni mpango wa Mungu ili alilopanga litimie.

Kumbukeni ya Musa na Farao katika kuwatoa wana wa Israeli kutoka utumwani nchini Misri.

Ni swala la muda tu.
 
Kaandika hivi kupitia mtandao wa twitter:

Niko HEWANI tena.... nimepata SIMU zangu USIKU HUU ...... hakuna NENO la Shukran ninaloweza kulisema....zaidi ya ASANTE!!!!!! kwa wema,ukarimu na upendo wenu!!! Sina cha kuwalipa. Niwahakikishie.....niko IMARA KULIKO JANA.
salimie sana hiyo mama mwambie sisi jimboni tunasema bye bye kwa yeye penda kesi ya jinai, oktoba tunachagua bunge nyingine .
 
Halima Mdee, a name with special meaning to our nation.

Nitajitahidi, nimwone Dada huyu ana kwa ana. Akina Dada wa namna hii hawapo wengi Duniani.

Pole sana Halima, pole sana kwa mateso yote. Waliokutenda wasamehe. Kuna wakati unaweza kutaka kwenda kumwokoa mbuzi aliyejiviriga kwa kamba ambayo inaweza kumwua, lakini kwa ujinga wake mbuzi, akakupiga mateke na kukuvunja taya. Mbuzi wa namna hiyo utamfanya nini? Utamsamehe kwa kuwa unajua kaumbwa aishi na upumbavu.
 
Kaandika hivi kupitia mtandao wa twitter:

Niko HEWANI tena.... nimepata SIMU zangu USIKU HUU ...... hakuna NENO la Shukran ninaloweza kulisema....zaidi ya ASANTE!!!!!! kwa wema,ukarimu na upendo wenu!!! Sina cha kuwalipa. Niwahakikishie.....niko IMARA KULIKO JANA.
Dah...sauti ya zege...dah

Sent using Beretta ARX 160
 
Kaandika hivi kupitia mtandao wa twitter:

Niko HEWANI tena.... nimepata SIMU zangu USIKU HUU ...... hakuna NENO la Shukran ninaloweza kulisema....zaidi ya ASANTE!!!!!! kwa wema,ukarimu na upendo wenu!!! Sina cha kuwalipa. Niwahakikishie.....niko IMARA KULIKO JANA.
Maneno ya kishujaa kabisa. May God Bless You Halima.Mdee.
 
Usipotii sheria bila shuruti, utashurutishwa kuitii sheria. Na wenye taaluma hiyo wapo na wamefundishwa na pia wameongezewa vitendea kazi vinavyonunuliwa kwa kodi ya Wananchi.

Amelia kama Bia/Soda kwenye CHUMA isipo kizibo.Ukizitikisa tu vimiminika vitafoka na kumwagika.Si mmeejaribu na mmeona.

"Kina cha maji ziwani hakipimwi kwa unyayo"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja / ccm ni chama cha watu wavijijin wasio na umeme wala maji.
Hapana.

Wewe ndiye unawauza huko bila ya ridhaa yao.

Watafute. Nenda huko vijijini ukazungumze nao, waelimishe pale ambapo hawana ufahamu napo.

Baada ya kufanya hivyo, na wakiendelea na kuing'ang'ania CCM, hapo utakuwa na haki ya kuandika uliyoandika hapo juu.
 
Usipotii sheria bila shuruti, utashurutishwa kuitii sheria. Na wenye taaluma hiyo wapo na wamefundishwa na pia wameongezewa vitendea kazi vinavyonunuliwa kwa kodi ya Wananchi.
Amelia kama Bia/Soda kwenye CHUMA isipo kizibo.Ukizitikisa tu vimiminika vitafoka na kumwagika.Si mmeejaribu na mmeona.
"Kina cha maji ziwani hakipimwi kwa unyayo"

Sent using Jamii Forums mobile app
Una ujinga mkubwa sana.

Ni mzigo mzito unaokuelemea. Itabidi tu uutue ukifika mahala.

Asiyetii sheria inajulikana ni wapi anapotakiwa kupelekwa ili aone sheria ambayo hakuitii.

Asiyetii sheria ni wewe na kundi lako lote mnaochukua sheria mkononi, na siku yenu itafika tu siku moja.
 
Salary Slip, p
Kila mara huwa nasema mmeshindwa kuwa na mikakati ya kujenga Chama ili atleast watu warudishe ile imani waliyokuwa nayo kwenu,lakini mmebaki kuwa na propaganda za kipumbavu(lack of intelligence).Habari za kumlinganisha Yesu na wanasisa matapeli zinatoka wapi?

Leo hii waha matapeli watamkomboa nani? Na Tanzania inahitaji kukombolewa toka kwenye matatizo yapi? Kama ufisadi umedhibitiwa,kama zahanati na hospital zimejengwa, barabara na madaraja yanendelea kujengwa Sgr JNHHP n.k. Unajua mmefeli mpaka mnadhani huruma toka kwa wananchi ndio solution.
 
Back
Top Bottom