Halima Mdee: Naona aibu Prof. Kabudi kuwa mwalimu wangu

Ni haki yake kuona aibu. Hata mimi huyu Karamaganda Kabundi niliyemtegemea siyo huyu. Amekuwa mtupu kichwani kuliko alivokuwa kabla hajaupata huo uwaziri

Wallah ukiteuliwa na sisonje anakuharibu kwanza ubongo ufanane na wake, huyu Kalamaganda alikuwa anaheshimika, akiunguruma kwenye makongamano watu walipigwa ganzi kumsikiliza na povu lake mdomoni, ila sasa huwezi jua kala maharage na kuvimbiwa au ubongo kachukua sisonje kauhifadhi gambushi kwao
 
Kwahiyo hizo fedha hazitakuwa documented ktk kitabu cha mapato...
Hizo zitapigwa kama zile za EPA ambazo nazo walidai kuna waliorudisha lakini haijulikani nani alirudisha na ni sh ngapi. Walipomaliza kuzipiga zile wakageukia kapu la Esrow. Mpaka leo waliobeba kwenye mabox, lumbesa na mifuko ya sandalusi "hawajulikani" lakini wale ambao miamala yao ilipitia bank ndio wanajulikana. Hata kujulikana kwao hakusaidii kitu kwani wako huru wanakula pesa bila jasho na wengine ni viongozi bungeni. Hizo anazosema kabudi nazo zitabebwa kama za Escrow kwakuwa wanazipokea kwa siri na watazibeba kwa siri. Kwani mpaka sasa trilioni 1.5 iko wapi? Tuombe watokee akina Lisu wengine watakaofichua siri kama zile za ndege. Tumbili ambaye alikomalia Escrow naye kageuka kuwa ngedere baada ya kuona anapiga kelele lakini wenzake wanafaidi kwa kumaliza mahindi shambani akaona ni bora ajiunge nao angalau naye atafune hata magunzi
 
Kabudi alivyosema "when the president was the president and the law was the law" tu, nikajua waziri tumempata.

Hiyo ni kauli ambayo mtu anayejitambua aliyepewa dhamana kuwa waziri wa sheria na rais kwa sasa hatakiwi kuisema.

Kwa sababu ni kama kusema sasa hatuna sheria na rais wetu ni boya.

Nikaona huyu jamaa anaweza kuwa na uzuri wake, lakini hana kina cha fikira wala uwezo wa kuchuja maneno.
 
Nilikutana na mwalimu wangu Kabudi majuzi kati pale Mlimani City.. tuliteta kidogo na alikiri kwamba aliteuliwa kwa shinikizo na alitishwa..na mengi anayojibu ni kwa maagizo. Hivyo anapaswa kusamehewa
 
Nilikutana na mwalimu wangu Kabudi majuzi kati pale Mlimani City.. tuliteta kidogo na alikiri kwamba aliteuliwa kwa shinikizo na alitishwa..na mengi anayojibu ni kwa maagizo. Hivyo anapaswa kusamehewa
Kama ni kweli -we have no way of verifying- then he is not only not an intellectual, he fails a basic test of integrity.

He is a coward.

Ni bora mtu anayekosea kwa kusimamia anachokiamini, kuliko mtu anayejua haya maamuzi mabaya, nafanya kwa kushinikizwa, halafu akakubali kufanya maamuzi hayo.
 
Ili kuendelea kuheshimika ukiwa kama msomi ni kuyakataa tu hayo mavyeo ya Jiwe.Hayana maana zaidi ya kujidhalilisha tu!
 
Vitu vingine mnaimbishwa kama kasuku tuu, DJ DJ!
Huyo DJ umsemaye baba yenu jiwe kamvulia kofia, sio PM wala waziri au kiongozi yeyote ambaye anaweza kuendelea kunywa chai akisikia Mbowe anaongea! Wote ni attention tuu.
Sasa nyie msio na hata anuani ndio mnaimbishwa Mbowe, Mbowe na kama mazuzu mnaitikia kwa nguvu kiitikio huku walio watuma wako pembeni uzwazwa wamewaachia
Pole sana mkuu Chakaza. Mkija kujitambua mtakuwa tayari ni wazee wa miaka 80, mnatembea kwa kutumia fimbo.
 
Ni haki yake kuona aibu. Hata mimi huyu Karamaganda Kabundi niliyemtegemea siyo huyu. Amekuwa mtupu kichwani kuliko alivokuwa kabla hajaupata huo uwaziri
Tatizo mliowengi mpaka sasa bado hamjamjua Adui namba moja wa Nchi hii...ni CCM hata akija Obama kutawala kupitia hiyo taka taka mambo yatakuwa Yale yale
 
financial statements za ACACIA zitaonesha kama watalipa msiwe na wasiwasi
wazungu hawana akili ndogo kama haya maccm
hivi na nyinyi mnamuamini vipi mtu mwenye kadi ya ccm!!!
 
Mbona Wewe halima haujaona aibu kuongozwa na Mwenyekiti wako Wa chama aliyepata Division Zero form six
 
Jiwe nae angeacha kutangaza kwamba tuna hela nyingi sana, tupo pazuriii na tutembee kifua mbele maana hii pia inachangia watu kwenda kudai fidia. Maprofesa waliopo CCM akili zao zimepigwa sindano ya ganzi.
 
Ukifanya kazi ya kuitetea CCM lazima akili irudi nyuma 50%
Hii si afadhali...embu jaribu kazi ya kuitetea chadema kwa sasa kama utaweza...lazima akili irudi nyuma 0%.. hivi chama cha mafisadi unaanzaje kukitetea...tuambiane ukweli...LIST OF SHAME imefichiliwa mbali kisa...! Eti mzee kaja.....pyuuuuusssss.....
 
Kama kweli maneno haya yamesemwa kama inavyodaiwa basi tuna tatizo kubwa zaidi kuliko huyo aliyesema maneno hayo. Kama serikali haitaki kutangaza mapato yake kuna wasiwasi hata matumizi yake pia haitataka yatangazwe. Hii inaleta tafsiri ya ajabu sana na inaweza kuleta athari. Siku zote serikali inawasisitiza wananchi wawe wawazi kwenye mapato yao ili yenyewe iweze kukusanya kodi stahiki kutoka kwao, sasa inapotangaza kwamba inaficha mapato yake kisa isidaiwe (!?) inatoa ujumbe gani kwa wananchi wa kawaida hasa walipa kodi? Serikali inapaswa iwe mfano kwa kuwa wazi katika mapato na matumizi yake ili wananchi nao waige mfano huo, lakini hapa wananchi wataiga nini kutoka serikalini?
 
Back
Top Bottom