Halima Mdee: Naona aibu Prof. Kabudi kuwa mwalimu wangu

Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee amesema anaona aibu kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kuwa mwalimu wake kwa sababu ameshindwa kulieleza Bunge kuhusu Sh424 trilioni ambazo Serikali ilidai zitalipwa na Mgodi wa Acacia kama kodi waliyokwepa.
duuuuuhhhh . . . . . . . . kweli ni aibu, maana hili sakata limeshageuka kigugumizi
 
Pole Halima.. Ila yakupasa kujua kuwa huo uongo ndio uliompa hiyo nafac.. Hivyo ni lazima ajidefend kwa njia hiyo-hiyo ya uongo..
 
Jiwe nae angeacha kutangaza kwamva tuna hela nyinhi sana, tupo pazuriii na tutembee kifua mbele maana hii pia inachangia watu kwenda kudai fidia. Maprofesa waliopo CCM akili zao zimepigwa sindano ya ganzi.

Yaani wanachekesha mbaya! Mzee mwenyewe anasema tuna pesa nyingi sana ndio maana tunanunua mpaka ndege keshi, hamna haja ya kuwa wanyonge tutembee kifua mbele tako nyuma likitingishika!

Lakini tukilipwa pesa iwe siri maana wanaotudai wakijua watakuja kutudai. Hapo which is which bwana Kabudi? au ulikuwa teee kama Kitwanga? maana majibu mengine yanaweza kuwa mchanganyiko wa K-vant na Konyagi pori imekuzingua na supu Profesa hujanywa!
 
Angekuwa wa hovyo angeongoza kamati itakayotuletea matrilioni ya dola..?? Ya makanikia...??? Wewe ndio wa hovyo kabisa..shwain
Hivi kumbe kuna wapuuzi kama Wewe unategemea wale wanaume walipe hayo matrillion!
 
Hivi kumbe kuna wapuuzi kama Wewe unategemea wale wanaume walipe hayo matrillion!
Khaaaa...!! Hivi ungekuwa wewe ungekubali kuendelea kuibiwa kama vile sio...?? Nchi ikiwana watu kama wewe walahi haitakaa iendelee...wale wanaume kwani sisi ni wanawake..?????.khaaaaaa...sijui mtapevuka lini akili wajameni
 
Mbona maprofessor wamekubali kutawaliwa na dr ambaye hajui kuandika hata sentensi moja ya kiingereza ?
Kwa hiyo sentensi ya kiingereza ndio inaonyesha umesoma sana au..????.kweli kazi ipo nchi hii..unataka kutuambia nchi zooote duniani kiingereza ndio key factor ya werevu..??
 
Yaani wanachekesha mbaya! Mzee mwenyewe anasema tuna pesa nyingi sana ndio maana tunanunua mpaka ndege keshi, hamna haja ya kuwa wanyonge tutembee kifua mbele tako nyuma likitingishika!
Lakini tukilipwa pesa iwe siri maana wanaotudai wakijua watakuja kutudai. Hapo which is which bwana Kabudi? au ulikuwa teee kama Kitwanga? maana majibu mengine yanaweza kuwa mchanganyiko wa K-vant na Konyagi pori imekuzingua na supu Profesa hujanywa!
Issue hapa ilikuwa kutaja amount wajameni mbona vichwa vyenu vigumu mno
 
Kama kweli maneno haya yamesemwa kama inavyodaiwa basi tuna tatizo kubwa zaidi kuliko huyo aliyesema maneno hayo. Kama serikali haitaki kutangaza mapato yake kuna wasiwasi hata matumizi yake pia haitataka yatangazwe. Hii inaleta tafsiri ya ajabu sana na inaweza kuleta athari. Siku zote serikali inawasisitiza wananchi wawe wawazi kwenye mapato yao ili yenyewe iweze kukusanya kodi stahiki kutoka kwao, sasa inapotangaza kwamba inaficha mapato yake kisa isidaiwe (!?) inatoa ujumbe gani kwa wananchi wa kawaida hasa walipa kodi? Serikali inapaswa iwe mfano kwa kuwa wazi katika mapato na matumizi yake ili wananchi nao waige mfano huo, lakini hapa wananchi wataiga nini kutoka serikalini?
Wewe lipa kodi inayotakiwa unataka kuigaiga nini..?? Mtu mmoja unataka kufanana na serikali kivipi..hivi unadhani nchi kubwa dunianihuwa zinaweka wazi kila kitu..lazima kunakuwa na policy ya kutunza baadhi ya siri nyeti na hasa haya mambo ya uchumi wa dunia..ni vitaa..sio kujianikaanika tu kama kuku wa kienyeji mitaani..hata nyumbani kwako kuna vitu vya siri huwezi toa nje mitaani eti watu waige..you have got to be selective on some issues.
 
Khaaaa...!! Hivi ungekuwa wewe ungekubali kuendelea kuibiwa kama vile sio...?? Nchi ikiwana watu kama wewe walahi haitakaa iendelee...wale wanaume kwani sisi ni wanawake..?????.khaaaaaa...sijui mtapevuka lini akili wajameni
Ndio wale wanaume! Labda kama umeamua upingane na maneno ya rais wetu aliyewaita hivyo
 
wanachaguwa wasomi ili iweje na wakati hawatumii usomi wao hao wasomi wenyewe? Si huwa wanawachaguwa ili kupunguza hoja zenye makali za kupingana na sera mbovu mbovu za serikali? Msomi kazi yake inabadilika kutetea ubadhirifu. Mwishowe inaonekana mara mia hata ya asiye msomi.

Sasa sijui tumlaumu nani hapa zaidi ya serikali ya ccm?
 
Back
Top Bottom