Halima Mdee: Naona aibu Prof. Kabudi kuwa mwalimu wangu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,506
mdee+kabudi+pic.jpg

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma. Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee amesema anaona aibu kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kuwa mwalimu wake kwa sababu ameshindwa kulieleza Bunge kuhusu Sh424 trilioni ambazo Serikali ilidai zitalipwa na Mgodi wa Acacia kama kodi waliyokwepa.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2018/19, Mdee amesema wakati Profesa Kabudi akizungumza bungeni alisema hawatasema tena kiasi wanachodai kwa makampuni hayo kwa sababu kuna watu wanaibuka kuidai nchi.

“Tuliwahi kusema kuwa shida si Acacia, shida ni Serikali. Naona aibu kusema kuwa Kabudi ni mwalimu wangu, waziri anasema kuwa hawezi kutamka kiasi gani kimelipwa kwasababu watakuja watu wanaotudai,’’amesema.

Hata hivyo, alikatizwa na maombi ya taarifa kutoka kwa wabunge wa CCM na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) na hivyo muda wake wa kuchangia kuisha.

Chanzo: Mwananchi
 
View attachment 794767

Kwani uwaziri unasomewa?!!
 
Hawezi kutangaza kwakuwa watu wanaodai wataibuka!!!
Kwahyo serikali haitaki kulipa madeni inayodaiwa?
Mbona yenyewe inapodai inatumia mabavu!!?
Watu wamepoteza makontena yao kwa kudaiwa na serikali!!
Watu wamefungiwa biashara zao kwa kudaiwa na serikali!!
Kweli nyani haoni kundule!!
 
Unaachaje kuona aibu kwa viongozi wa aina hii.
Ni zuzu tu ndio anaweza kumuona Kabudi yupo sawa .Huyu mzee ameingizwa mkenge bila kujua, sasa ataongozwa na kina Bashite, Lusinde, Msukuma bila hata kupenda kwani CCM kwanza akili baadae.
 
Back
Top Bottom