Halima Mdee na wenzake 18 watatoboa Mahakamani kwa kutumia hoja hizi?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,192
25,493
Nawasalimu waungwana wa JF,

Kama ilivyo ada yangu, nianze kwa kutamka kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa hapa Tanzania au kwingineko. Daima, nimekuwa nikijenga hoja; kukosoa kwa staha; kushauri au kuunga mkono hoja yoyote ya kisiasa au ya kitaifa kumhusu yeyote yule. Sibagui chama chochote au mtu yeyote wa kumhusisha na hoja yangu. Pamoja na yote yanayojulikana kwenye sakata zima za akina Halima Mdee, nawiwa kusema neno katika maeneo mawili: ubunge wao na taratibu za kinidhamu zilizofuatwa dhidi yao.

Nikiri kuwa nimeziona na kuzisoma nyaraka zilizowasilishwa na akina Halima Mdee Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la kutekelezwa kwa uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA dhidi yao pamoja na kuondolewa kwa ubunge wao. Sitaki na wala siko tayari kujadili kwa kina kuhusu nyaraka husika (kwakuwa si sahihi na hairuhusiwi kujadili jambo ambalo liko mahakamani). Mpira uko kwa Jaji Mgeta kwasasa na yeye anaucheza katika kutoa haki kwa anayestahili. Unaweza kuziona hapa: Nyaraka za kesi iliyofunguliwa na Halima Mdee na Wabunge wenzake dhidi ya CHADEMA

Hatahivyo, nisamehewe kwa kufanya hivyo, nitatumia kauli mbili za kwenye Kiapo cha Halima James Mdee alichokiwasilisha Mahakama Kuu ya Tanzania katika shauri lao. Aya husika ni ya 2 na 18 ya Kiapo hicho. Kwanini ni Halima Mdee? Ndiye anayetajwa na kuonekana kama kiongozi wa wahusika 19 waliofukuzwa uanachama na CHADEMA. Hata kesi yao imeanza na jina lake. Kwanini Kiapo? Kisheria na kiuhalisia, Kiapo ni ushahidi. Katika Kipo tajwa kunapatikana mambo yangu mawili.

Kuhusu ubunge wao, Halima Mdee (kwenye aya ya 2 ya Kiapo chake) anasema kuwa wao waliteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kudhaminiwa na CHADEMA. Yaweza kuwa makusudi au bahati mbaya, Mdee amekwepa kusema kuwa walipendekezwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kwakuwa wao wanaamini kuwa ni Wabunge halali wa VIti Maalum wa CHADEMA, walipaswa kupendekezwa na kudhaminiwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kuacha hoja hii ya kupendekezwa na CHADEMA kama takwa la kikatiba na kisheria, ni kuuteteresha ukuta wao wa kuwakinga.

Kuhusu taratibu za kinidhamu zilizofuatwa kwenye kufukuzwa kwao uanachama na CHADEMA, kwenye aya ya 18 ya kiapo chake, Halima Mdee analeta hoja ya kuwa wanachama ambao pia ni 'Wabunge' wana taratibu za kipekee katika kushughulikiwa kinidhamu tofauti na wanachama wa kawaida. Tena, taratibu hizo za kipekee kwa wanachama walio 'Wabunge' hazikufuatwa. Yawezekana ni kwa makusudi au bahati mbaya, Halima Mdee hakuelewa mantiki ya hoja yake mwenyewe na hoja ya CHADEMA katika jambo lao-la jinsi walivyoteuliwa kuwa Wabunge.

Tangu mwanzo, CHADEMA imekuwa inapinga uhalali wa kuteuliwa kwa akina Halima Mdee. Kwakuwa wamekuwa wakipinga uhalali wa kuteuliwa kwao, ni wazi kuwa CHADEMA haikuwahi kuwatambua akina Mdee kama Wabunge wao wa Viti Maalum baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Hivyobasi, akina Halima Mdee walishughulikiwa kinidhamu kama wanachama wengine wa kawaida na hakukuwa na sababu za kushughulikiwa kama 'Wabunge' kwakuwa wao si 'Wabunge' kwenye macho ya CHADEMA. Ndiyo kusema, taratibu za kipekee za kuwashughulikia kinidhamu wanachama walio Wabunge za CHADEMA 'hazikuwahusu akina Halima Mdee.

Taarifa ya kufukuzwa uanachama imewasilishwa Bungeni ili kuwaondoa kwenye Ubunge wote wanaotajwa kama Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalum. Kutokana na hayo mambo mawili na mengineyo, nauona ukuta wanaoutumia akina Halima Mdee kujikinga na kuhalalisha ubunge wao kama dhaifu na usio na msaada kwao. Lakini, kwakuwa jambo hili lipo mahakamani, tusubiri matokeo yake. Haya yabaki kama maoni yangu tu.
 
nani kasema sheria zinafatwa tena nchi hii? siku hizi ni kusikilizia maagizo toka juu..hao hata wakitoboa waki drill , wakae huko hadi 2050 wapewe na vyumba hapo bungeni , shauri zao na hao wanaowalea ILA ISSUE KUBWA NI KWAMBA SIYO WANA CHADEMA watafutiwe chama haraka
 
Kwamba CCM Wana utaalam wa kufuata sheria za jinsi ya kufukuzwa uanachama wanachama wao au ni kuwa wanachama wao wakifukuzwa huwa wapole?
 
Nakubaliana na wewe

Hata CCM hupendekeza majina zaidi y 100 halafu NEC huteuwa kulngana na idadi inayohitajika.

Cha ajabu Chadema walipeleka exactly.majina 19!

CDM hawakupeleka hayo majina hata Halima Mdee mwenyewe anakiri hilo. Kasema waliteuliwa na NEC na kudhaminiwa na CDM, yaani kaeleza njisi alivyoaanza kuvaa sketi/suruali kabla hajavaa taiti
 
CDM hawakupeleka hayo majina hata Halima Mdee mwenyewe anakiri hilo. Kasema waliteuliwa na NEC na kudhaminiwa na CDM, yaani kaeleza njisi alivyoaanza sketi/suruali kabla hajavaa taiti
NEC wakimteua vipi bila kupokea majina kutoka CHADEMA? ulitaka aseme NEC walipewa majina na CHADEMA kwani ye inamhusu? NEC watajibu waliyatoa wapi majina ndo sababu na wenyewe ni washtakiwa kwenye kesi hii.
 
Wansheria wa hivyo kama wewe naye unakuja na kelele zako huku

Ussr
ujinga wako ni pale unapowaita watu wenye akili wa hovyo bila kuelezea uhovyo wao tu kwasababu wameandika ukweli usiopenda kuusikia.
je tukisema wewe ni wa hovyo zaidi yao utakanusha?
hoja hujibiwa kwa hoja siyo vijembe na taarabu za bi khadija kopa ka hizo zako
 
NEC wakimteua vipi bila kupokea majina kutoka CHADEMA? ulitaka aseme NEC walipewa majina na CHADEMA kwani ye inamhusu? NEC watajibu waliyatoa wapi majina ndo sababu na wenyewe ni washtakiwa kwenye kesi hii.
Sawa mkuu tusubiri, lile swali letu la nani aliandaa majina na kuweka saini ya Mnyika sasa litapata jibu
 
Nimesoma hoja za Kibatala na Mtobesya naona kama ni hojo nzuri..lakini kwa nini huwa nashindwa kwenye mapingamizi anayoweka? mahakama huwa zinafanya kusudi au ni kweli huwa na hoja dhaifu kisheria?
 
Nawasalimu waungwana wa JF,

Kama ilivyo ada yangu, nianze kwa kutamka kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa hapa Tanzania au kwingineko. Daima, nimekuwa nikijenga hoja; kukosoa kwa staha; kushauri au kuunga mkono hoja yoyote ya kisiasa au ya kitaifa kumhusu yeyote yule. Sibagui chama chochote au mtu yeyote wa kumhusisha na hoja yangu. Pamoja na yote yanayojulikana kwenye sakata zima za akina Halima Mdee, nawiwa kusema neno katika maeneo mawili: ubunge wao na taratibu za kinidhamu zilizofuatwa dhidi yao.

Nikiri kuwa nimeziona na kuzisoma nyaraka zilizowasilishwa na akina Halima Mdee Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la kutekelezwa kwa uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA dhidi yao pamoja na kuondolewa kwa ubunge wao. Sitaki na wala siko tayari kujadili kwa kina kuhusu nyaraka husika (kwakuwa si sahihi na hairuhusiwi kujadili jambo ambalo liko mahakamani). Mpira uko kwa Jaji Mgeta kwasasa na yeye anaucheza katika kutoa haki kwa anayestahili. Unaweza kuziona hapa: Nyaraka za kesi iliyofunguliwa na Halima Mdee na Wabunge wenzake dhidi ya CHADEMA

Hatahivyo, nisamehewe kwa kufanya hivyo, nitatumia kauli mbili za kwenye Kiapo cha Halima James Mdee alichokiwasilisha Mahakama Kuu ya Tanzania katika shauri lao. Aya husika ni ya 2 na 18 ya Kiapo hicho. Kwanini ni Halima Mdee? Ndiye anayetajwa na kuonekana kama kiongozi wa wahusika 19 waliofukuzwa uanachama na CHADEMA. Hata kesi yao imeanza na jina lake. Kwanini Kiapo? Kisheria na kiuhalisia, Kiapo ni ushahidi. Katika Kipo tajwa kunapatikana mambo yangu mawili.

Kuhusu ubunge wao, Halima Mdee (kwenye aya ya 2 ya Kiapo chake) anasema kuwa wao waliteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kudhaminiwa na CHADEMA. Yaweza kuwa makusudi au bahati mbaya, Mdee amekwepa kusema kuwa walipendekezwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kwakuwa wao wanaamini kuwa ni Wabunge halali wa VIti Maalum wa CHADEMA, walipaswa kupendekezwa na kudhaminiwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kuacha hoja hii ya kupendekezwa na CHADEMA kama takwa la kikatiba na kisheria, ni kuuteteresha ukuta wao wa kuwakinga.

Kuhusu taratibu za kinidhamu zilizofuatwa kwenye kufukuzwa kwao uanachama na CHADEMA, kwenye aya ya 18 ya kiapo chake, Halima Mdee analeta hoja ya kuwa wanachama ambao pia ni 'Wabunge' wana taratibu za kipekee katika kushughulikiwa kinidhamu tofauti na wanachama wa kawaida. Tena, taratibu hizo za kipekee kwa wanachama walio 'Wabunge' hazikufuatwa. Yawezekana ni kwa makusudi au bahati mbaya, Halima Mdee hakuelewa mantiki ya hoja yake mwenyewe na hoja ya CHADEMA katika jambo lao-la jinsi walivyoteuliwa kuwa Wabunge.

Tangu mwanzo, CHADEMA imekuwa inapinga uhalali wa kuteuliwa kwa akina Halima Mdee. Kwakuwa wamekuwa wakipinga uhalali wa kuteuliwa kwao, ni wazi kuwa CHADEMA haikuwahi kuwatambua akina Mdee kama Wabunge wao wa Viti Maalum baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Hivyobasi, akina Halima Mdee walishughulikiwa kinidhamu kama wanachama wengine wa kawaida na hakukuwa na sababu za kushughulikiwa kama 'Wabunge' kwakuwa wao si 'Wabunge' kwenye macho ya CHADEMA. Ndiyo kusema, taratibu za kipekee za kuwashughulikia kinidhamu wanachama walio Wabunge za CHADEMA 'hazikuwahusu akina Halima Mdee.

Taarifa ya kufukuzwa uanachama imewasilishwa Bungeni ili kuwaondoa kwenye Ubunge wote wanaotajwa kama Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalum. Kutokana na hayo mambo mawili na mengineyo, nauona ukuta wanaoutumia akina Halima Mdee kujikinga na kuhalalisha ubunge wao kama dhaifu na usio na msaada kwao. Lakini, kwakuwa jambo hili lipo mahakamani, tusubiri matokeo yake. Haya yabaki kama maoni yangu tu.
Kama mbowe alikutwa ana kesi ya kujibu kwa ushahidi ule wa kina afande Urio..usishangae Mdee et al wakashinda kesi hiii kwa hoja hizi hizi!
 
Back
Top Bottom