Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,984
2,000
Hii ndio kazi Magufuli anayoweza kufanya, yeye maendeleo ni usanii tu wa kwenye majukwaa.

Atamaliza miaka yake kumi ya ukora nchi ikirudi nyuma kimaendeleo kama treni ya Godegode. Very useless dictator.
"Makamanda nchi nzima, tulieni! Tumekuja hapa leo ili kuapa, tuweze kuendeleza harakati za mapambano. Mwenyekiti wetu anajua. Na kazi yangu mnaifahamu siku zote!" ~ HJM (Mb).
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,825
2,000
Bulaya mtoe kwenye hiyo list, maana alimfuata Mdee na sio chama. Labda Mdee ndio tumjadili. Ili waseme ni kwanini wamechukua hayo maamuzi, ndio hao wameitwa kwenye kikao wanyooshe maelezo lakini wamegoma.
Habari hii ni ya kushangaza sana. Hata ni ngumu kuamini kwamba Mdee angekuwa mmoja kati ya hao watu. Ni ajabu sana!
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,825
2,000
Umeuliza kama mimi naweza kununuliwa hasa baada ya Mdee kujiuza , kwa kifupi nikujibu tu kwamba mimi siwezi kununuliwa kwa sababu sifanyi siasa ya kujikimu , mimi na wachache kama Mbowe tuliingia kwenye siasa tukiwa na hela nyingi kwa lengo la kusaidia utawala wa haki na demokrasia nchini Tanzania .
Kama sio kununuliwa, yaani hamna bei, huoni mtatafutiwa njia nyingine msiyoweza kuikataa?

Elewa kwamba tuna mtu wa ajabu sana aqnayefanya mambo usiyotegemea kwamba binaadam anaweza akayafanya. Huyu kwake hakuna lisiloweza kufanyika.
Hebu angalia Mbowe alivyohangaishwa hadi hapa tulipofikia! Mwishowe na yeye atasema, mateso yote haya ya nini wakati anaowaongoza kila mara hawaoni usumbufu anaopitia kumbe wao wapo kukidhi mahitaji yao tu, kama akina Mdee?
Bado siamini kabisa kuwa Mdee ni mmoja wao!
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,825
2,000
Kumbe unaogopa kuuliwa basi kaa utulie sio unaanza kuwaita watu wasaliti watu ambao hawakuogopa kuuliwa katika harakati za kudai haki walizidai hadharani tofauti na wewe uliyejificha humu JF unaogopa hata kuandamana,si ajabu nawe unakula keki ya taifa vizuri tu ila humu mnakuja kuleta unafki na ndio maana hamuwezi kuandamana kudai haki mnajificha.
Ni wapi uliposoma nimeandika "naogopa kuuliwa"?

Basi furahia hiyo "keki ya taifa" huku ukitafuta damu za waTanzania.
Nimekupa heshima usiyostahiri kwa kukujibu hapa; kwani wewe ni mpuuzi mmoja nisiyekuwa na muda wa kupoteza kujibishana naye.

Haya endelea kushangilia, na huenda mkaipata hiyo damu mnayoitafuta kwa udi na ubani. Na hata mkishaipata, hamtaridhika, bado roho zenu zitaendelea kuhangaika tu hadi mwisho wenu utakapowadia.
 

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,592
2,000
Siku zote vyama vya upinzani vikiwa kwenye mgogoro lawama zote huenda kwa dola na CCM.
Kwani kwa mfano mdogo tu ulishawahi ona wapi AG anawatetea wabunge wateule wa Chadema? au uliwahi ona wapi mtu yuko mahabusu anapata fursa ya kusainishwa kuwa mbunge mteule wakati alinyimwa nafasi ya kujaza fomu ya kugombea ubunge makusudi hapo awali? au unataka kusema ni Repablican au Democratic wanaosabibisha mgogoro wa vyama vya upinzani
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,776
2,000
Kama sio kununuliwa, yaani hamna bei, huoni mtatafutiwa njia nyingine msiyoweza kuikataa?

Elewa kwamba tuna mtu wa ajabu sana aqnayefanya mambo usiyotegemea kwamba binaadam anaweza akayafanya. Huyu kwake hakuna lisiloweza kufanyika.
Hebu angalia Mbowe alivyohangaishwa hadi hapa tulipofikia! Mwishowe na yeye atasema, mateso yote haya ya nini wakati anaowaongoza kila mara hawaoni usumbufu anaopitia kumbe wao wapo kukidhi mahitaji yao tu, kama akina Mdee?
Bado siamini kabisa kuwa Mdee ni mmoja wao!
Labda kuuawa , lakini kununuliwa haipo , after all hii ccm wanayohamia wengine leo haina maisha marefu , maisha yake ni mafupi mno ! hii ni sawa na raia wa Zimbabwe leo hii ajiunge ZANU PF , ni lazima atakuwa karogwa
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,463
2,000
Muda mfupi kabla Kamati kuu CHADEMA kuwahoji wanachama wake walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, wanachama hao wamesisitiza kutotokea mbele ya kamati kuu wakidai kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wakihofia usalama endapo watafika ofisi za chama hicho.
--
Awali Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) leo waliandamana katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, kushinikiza kutowahitaji wabunge Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine walioapishwa viti maalum.


Updates

PICHA: Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wakiendelea na kikao hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam cha kuwajadili Halima Mdee na wenzake 18 wanaotuhumiwa kwa usaliti wa chama kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum. #MwanaHALISIDigital https: View attachment 1635850 View attachment 1635851 View attachment 1635852 View attachment 1635854
Kuna watu wana bahati Sana.
1) Chama kinaweka msimamo wa kutotambua matokeo wao wanakiuka msimamo huo.

2) Waanitwa kwenye kikao kujieleza wanaamua kukacha pia.
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
6,791
2,000
Kuwafukuza hawa kuna hasara kwa CHADEMA zaidi ya faida. Basically hawa haiwezekani tena kuwaondoa bungeni kwa muda huu.

Regardless wamekwendaje kule, CHADEMA inapaswa kumaximize uwepo wao Bungeni. Ndani ya chama bila shaka kuna kiongozi mmoja au wawili wamewezesha hili kufanyika baada ya kupiga hesabu kali. Mbowe yu wapi?

Tukiacha ushabiki wa kwenye social media, kuna maisha baada ya uchaguzi na lazima chama kiendelee kuwepo - financially

Kabla hujapost na kudai wafukuzwe tu ili “kuleta heshima” jiulize maswali haya

1) Unapenda CHADEMA pia ikatae Ruzuku kwa kuwa zitakuwa ni zao la tunda haramu?
2) Wakifukuzwa ila Bunge/Mahakama ikawalinda, CHADEMA isiwatambue na ikate pia kupokea ile michango kutoka kwenye salary ya kila mbunge?
3) Wewe binafsi umeshawahi kuichangia CHADEMA shilingi ngapi?
Nasikia wameshawasamehe tayari.
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
6,791
2,000
Labda kuuawa , lakini kununuliwa haipo , after all hii ccm wanayohamia wengine leo haina maisha marefu , maisha yake ni mafupi mno ! hii ni sawa na raia wa Zimbabwe leo hii ajiunge ZANU PF , ni lazima atakuwa karogwa
Vipi hii hapa chini
IMG-20201127-WA0028.jpg
IMG-20201127-WA0027.jpg
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,825
2,000
Sasa si wangewasiliana na IGP Sirro ili awape ulinzi wanapokuwa wanapokuwa wanaelekea kwenye kikao kujitetea?

Kutishiwa usalama wao Hakupo Bali ni kisingizio tu...

Ukweli ni kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa na chama chao (ambayo obviously ni kuvuliwa uanachama), dola imewahakikishia kuwa wataendelea kuwa wabunge tu...!

Andiko la Yericko Nyerere lina maana sana. CHADEMA waendelee mbele. Hakuna sababu ya kulea watovu wa nidhamu ndani ya chama wanaouza utu wao kwa fedha..


Bahati mbaya kwa dola ni kuwa, CHADEMA wakisimama kwenye msimamo wao na kua - bide ktk principles za uendeshaji wa chama, lengo la Magufuli na CCM litagonga mwamba spectacularly..

Mwafaka hapa ni kukaa mezani tu kwa ajili ya mwafaka...
Nimekusoma na kukuelewa vizuri mkuu 'The Palm Tree' katika mistari yote huko juu, isipokuwa huo mstari uliouweka mwisho kabisa.

Unajua dhahiri kwamba hapa tulipofikia hapawezi kamwe kuwepo na hicho kitu unachokiita "Mwafaka".

Mwafaka utoke wapi wakati mporaji ameridhika uporaji wake umefanikiwa? Iliyobaki sasa hivi ni kuwashughulikia kwa njia mbali mbali wote wasiokubali uporaji uliofanyika. Inashangaza kidogo kuona kwamba bado kuna watu wenye matumaini, wewe ukiwa mmoja wao.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,163
2,000
Leo Makamanda waliopigania chama zaudi yako unawaita "mianamke".
Ukome kabisa na matusi yako
Walipigania chama dhidi ya nani? Dhidi yenu?

Waliopigania chama dhidi yenu leo wamegeuka rafiki zako? Tusianzie hapo kushangaa?
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,345
2,000
mbowe aseme ukweli asitake kuremba maneno kwa aiji ya kuutetea uenyekiti wake. la sivyo ajibu maneno/tuhuma aliyo yatamka mdee mara baada ya kula kiapo, mdee sio mjinga amsingizie Mbowe.
yaani kweli watu wote tunaonekana hatuwezi kufikiria kisa kumlinda mtu mmoja?! kwani huwezi kuachia nafasi kwa heshima tu kuliko kuumbuka ?!
mambo yamevurugika na wewe ndio kiongozi step down kwa heshima pisha wengine warudishe heshima ya chama na imani ya wanachama
Vuvuzela tu, umesha muhukumu Mbowe kisa Mdee katamka!.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom