Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Muda mfupi kabla Kamati kuu CHADEMA kuwahoji wanachama wake walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, wanachama hao wamesisitiza kutotokea mbele ya kamati kuu wakidai kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wakihofia usalama endapo watafika ofisi za chama hicho.
--
Awali Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) leo waliandamana katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, kushinikiza kutowahitaji wabunge Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine walioapishwa viti maalum.


Updates

PICHA: Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wakiendelea na kikao hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam cha kuwajadili Halima Mdee na wenzake 18 wanaotuhumiwa kwa usaliti wa chama kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum. #MwanaHALISIDigital https:View attachment 1635850View attachment 1635851View attachment 1635852View attachment 1635854
Mzee alisema ukiona unasifiwa fisiwa na aliyekuwa mkali wako basi kutafakari zaidi ya mara kumi na mbili kisha chukua hatua stahiki!! Na ukiona mtoto anakuvamia na kukipiga kifi jua baba yake yupo karibu... Take care na weka pembeni kwa namna yoyote...
Pili ikifuatwa katiba hakuna wa kulaumu hapo sisi hatutegemei busara tunategemea maelekezo ya kikatiba ndani ya chama...
 
Wakifukuzwa tu, watakimbilia Mahakamani, Korti itazuia Bunge kuwatimua, Speaker atatii kwa furaha kabisa, watadunda Ubunge mpaka June 2025 huku kesi ikirushwa

Humu katikati Dec 2020 - June 2025 hawa 19 na Kamati kuu watayajenga na kusameheana ili maisha yawe rahisi kwa kila mtu

Hizi ndizo siasa za Tanzania
Iwe hivyo, chama kitakuwa kimetimiza wajibu wake. Watasalia kuwa wabunge wa Mahakama/CCM/Serikali, maana serikali ndiyo inawahitaji zaidi
 
Halima Mdee ni mwanamke shujaa, msomi na mwanasheria, anaijua katiba ya Chadema, na vikao vya mamlaka ya nidhamu ni kama ifuatavyo...
  • Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
  • Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
  • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
  • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili litafanyika?.
  • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?.
Halima na genge lake they are very right, Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!.

P
Hakuna kisiki chochote ni upuuzi tu, kwa mujibu wa Katibu Mkuu John Mnyika alieleza kwamba kwa ile katiba yao ya Chadema ni kwamba inaweza ikawaita kuwapa nafasi ya kujitetea lakini pia wanaweza wasiwaite na maamuzi watakayotoa pia ni sahihi.

Nafkiri kama leo hawakuja kwenye wito wafukuziliwe mbali tujenge chama chetu. Kama Dr Slaa he was good for northig, lowassa, Mashinji itakuwa mdee
 
yaani unaonyesha kiwango cha wivu ulionao! Wa Mpanda alifanya kampeni ya kushindwa? mara paap akashunda au? bila kupambania katiba! Haya ni maigizo tuu. Serikali na nchi wala havitasimama, waacheni hao walau tupata hadhira ya kupaza sauti !

Hii uliyoandika nini? Very disappointing
 
Halima Mdee anaogopa kwenda kujitetea ,niliwaambia jana humu mpaka wapewe maelekezo na Jiwe na tiss yake ndio watafika au kutofika . Halima Mdee njoo utoe ushahidi Mbowe alikuruhusu kama ulivyosema bungeni wakati wa kuapishwa . Acha chenga Mbowe ndio huwa anaruhusu kwenda bungeni ? Au kamati kuu ? Njoo na ushahidi wa maandishi kwamba Mbowe alikuruhusu? Chama kinaendeshwa kwa vikao kikao kipi kirikuruhusu we Pimbi ? Fukuza haraka hawana cha kujitetea hao wakawe wabunge wa viti maalum vya Ndugai .
 
Hadi sasa haieleweki kama kikao hicho kitafanyika ama la kadhalika uhakika wa akidi kutimia unatia shaka.

Ufipa hali ni shwari na kuna vijana wachache wa BAVICHA ambao kimsingi hawatoi taarifa kama kikao kitakuwepo na kitafanyikia wapi zaidi ya kuwataka wanachama wawe na subira.

Ngoja tuone muda ndio msema kweli.

Maendeleo hayana vyama
Uko dunia ya wapi mkuu?
 
Mnyika na Kamati Kuu kazi nyepesi fukuza.
MImi nawashangaa sana CCM MWENYEKITI WAO KAFUKUZA WATU KAZI KWA VYETI BANDIA ETI WANASHABIKIA KUWA NAWABUNGE WAKUFORGE SAHIHI TUACHE KUWA NDUMI FUKUZA WAHUNI HAWA TUKIWAACHA WATAUWA CHAMA
 
Halima Mdee anaogopa kwenda kujitetea ,niliwaambia jana humu mpaka wapewe maelekezo na Jiwe na tiss yake ndio watafika au kutofika . Halima Mdee njoo utoe ushahidi Mbowe alikuruhusu kama ulivyosema bungeni wakati wa kuapishwa . Acha chenga Mbowe ndio huwa anaruhusu kwenda bungeni ? Au kamati kuu ? Njoo na ushahidi wa maandishi kwamba Mbowe alikuruhusu? Chama kinaendeshwa kwa vikao kikao kipi kirikuruhusu we Pimbi ? Fukuza haraka hawana cha kujitetea hao wakawe wabunge wa viti maalum vya Ndugai .
Kikao kinafanyika sa ngap ?? Mpak sasa alasiri near to down but nothing new , in short hakuna kikao , na Mnyika kafyata mkia ..... Nimekiri wazi perhaps Mbowe engineering all the speculation...Tangu sa mbili , ooh fukuza fukuza ...wanashindwa nn kutoa tamko issue iburst into flames.... Hakuna kikao hapo na Mbowe ndo mastermind of the game
 
MaCCM mmemuona kiboko yenu Mbowe kwenye kikao cha kamati kuu CHADEMA.
Semeni lingine sasa, waunga juhudi tunawapa hao, sie hatuishi na wasaliti nyumba moja. FUKUZAAA..!
 
Nasikia hii mianamke mikaidi na misaliti inataka Jumatatu kuamkia mahakamani ili wasifukuzwe uanachama kwa miaka mitano na wala wasijadiliwe
Vipi wakienda mahakamani kupinga wasifukuzwe,hizo trillion mbili zitatolewa na wafadhili.
 
Mimi bado naamini Mdee na wenzake hawajajipeleka wenyewe. Huu mchezo ni highly calculated. Haya yanayotokea yalishafahamika.

Tafuteni pesa mtengeneze future zenu. Msiwekeze miili na mioyo yenu kwa wanasiasa.
 
Mimi bado naamini Mdee na wenzake hawajajipeleka wenyewe. Huu mchezo ni highly calculated. Haya yanayotokea yalishafahamika.

Tafuteni pesa mtengeneze future zenu. Msiwekeze miili na mioyo yenu kwa wanasiasa.
Umeongea point
Inawezekana viongozi wamezidiana kwenye mgao
Lakini mnyika anajua yote
Mbona mpaka muda huu wako kimya
 
Back
Top Bottom