Halima Mdee na wenzake 18 hawana nguvu yoyote ya kimaamuzi Bungeni, wanaburuzika tu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Unaweza ukajiuliza uwepo wa wapinzani kiduchu bungeni una faida gani iwapo maamuzi yote muhimu yanafanywa na kamati kuu ya CCM?

Kiukweli Tanzania hatuna mfumo wa vyama vingi tuna kiini macho tu.

Na katika hili hayati Magufuli hakumung'unya maneno.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mbona mzee Mgaya unakuwa na ufinyu wa kufikiri.

Bunge la sasa ni matokeo ya Uchaguzi wa 2020 na ulisimamiwa na Magufuli mwenyewe.

Tunakumbuka walivyokatwa watu, hata kina Chenge na kura za mabegi.

Matokeo yakikuwa so smooth kiasi kwamba wapinzani hawakupenyeza hata sindano.

Kazi nzuri ya Magufuli!

Tukajikuta tuna bunge ka CCM watupu isipokuwa mbunge mmoja nafikiri Katavi huko.

Tatizo sasa kuna nafasi kikatiba lazima zishikiliwe na wapinzani.

Forgeries zikaanza kati ya Tume ya Uchaguzi na Ndugai.

Wakaingizwa kimpango mpango hao 19 wa CDM, kina Mdee.

Halima Mdee si wa upinzani, naye anajua hilo.

Yeye ni zao la Magufuli.

Sasa ataongea nini cha maana watu wamwelewe.

Sasa Magufuli angekemea vipi kazi yake?
 
Kwa hiyo nguvu ya kina Mdee bungeni ilishikiliwa na Magufuli?

Wale watu 19 wapo tu kuleta uwiano na si kuwa wanaweza pambana na idadi kubwa ya wabunge wa CCM...
 
Back
Top Bottom