Halima Mdee na Esther Bulaya watakiwa kujieleza kwanini walienda Afrika ya Kusini bila kibali cha Mahakama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,803
Hakimu Thomas Simba ameahirisha kesi ya viongozi wa CHADEMA ili kutoa muda kwa wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya pamoja na wadhamini wao kujieleza kwanini wasifutiwe dhamana baada ya kusafiri nje ya nchi bila ruhusa ya mahakama.

Mdee amesema alienda Afrika Kusini kupata matibabu baada ya kupewa barua na Hospitali ya Aga khan, katika safari hiyo ya kitabibu Halima alisindikizwa na Bulaya.

Chanzo: ITV habari!
 
Hawa wapinzani kweli wamebanwa, hawako huru kabisa,yaani ni kesi juu ya kesi, hakuna kutoa mguu nje ya nchi bila kuomba kibali cha mahakama, yaani ni kama wafungwa fulani walioko uraiani ndani ya nchi yao; this is not fair.

Hii yote ni kwasababu ya kesi iliyotengenezwa kwasababu walikwenda kudai kiapo, halafu eti huyo muhusika aliyechelewesha kutoa hicho kiapo bado yupo ofisini mpaka leo!, hivi ni nani mwenye kosa kati ya hao watu?! eti nyie mnaojiita wapenda kusema ukweli wapenzi wa Mungu? hebu acheni kuona wengine wajinga, wapeni uhuru wao hao watu, kuwa upinzani sio dhambi wala kosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakimu Thomas Simba ameahirisha kesi ya viongozi wa Chadema ili kutoa muda kwa wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya pamoja na wadhamini wao kujieleza kwanini wasifutiwe dhamana baada ya kusafiri nje ya nchi bila ruhusa ya mahakama.

Mdee amesema alienda Afrika kusini kupata matibabu baada ya kupewa barua na Hospitali ya Aga khan, katika safari hiyo ya kitabibu Halima alisindikizwa na Bulaya.

Source ITV habari!
Hivi hawa ni mme na mke nini?? Mbona wanafuatana sana?
 
Back
Top Bottom