Nidhamu katika taasisi yeyote ile ni jambo la msingi sana, iwe sehemu ya kazi iwe jeshini, kwenye biashara, pesa zako bila nidhamu huwezi kufanikiwa.
Kiongozi anapoenda kinyume na maamuzi halali ya taasisi ni aidha anajiuzulu au anafukuzwa. Halima Mdee amekiuka maamuzi halali ya Kamati Kuu hence ya Chama, awe amefanya kwa kushinikizwa au kwa tamaa zake, kwa kitendo kile hana uhalali tena wa kuendelea kuongoza kitengo cha BAWACHA.
Mbali na kukiuka msimamo wa Chama Mdee kaonyesha tamaa na ubinafsi wa hali ya juu, kajiteua yeye wa kwanza bila aibu badala ya kuwatafuta wanawake vijana wengine ndani ya chama nje ya BAWACHA nao wakapate ujuzi bungeni kama yeye.
1. Halima Mdee - M’kiti BAWACHA Taifa
2. Hawa Mwaifunga - Makamu M’kiti BAWACHA.
3. Grace Tendega - Katibu BAWACHA.
4. Jesca Kishoa - Naibu Katibu Mkuu BAWACHA.
5. Asia Mohamed - Naibu Katibu BAWACHA.
6. Agnester Kaiza - Mwenezi BAWACHA Taifa.
7. Ester Matiko- M’kiti kanda
8. Nusrat Hanje - Katibu BAVICHA
Juliana Shonza alikuwa Makamu M/kiti wa BAVICHA nakumbuka alileta vurugu kubwa ndani ya BAVICHA kiasi kwamba kuchelewa kwa chama kumfukuza ilikuwa al manusura akigawe chama, ilikuja kufahamika baadae kumbe Juliana hakuwa peke yake alikuwa ametangulizwa kama chambo, nyuma yake walikuwepo kina Zitto, Kitila, Mwigamba na wengineo.
Chama kimshukuru Mdee kwa kuijenga BAWACHA na yote aliyokifanyia chama lakini kitendo cha yeye kama kiongozi kukiuka maamuzi ya chama hakiwezi kuvumilika na chama kikiendelea kumlea anaweza kuambukiza mbegu ya uasi ndani ya chama na kuleta madhara makubwa ‘irreparable’ kwa sababu hatujui walio nyuma yake ndani na nje ya chama ni akina nani na wana nguvu kiasi gani.