Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA aidha ajiuzulu au aondolewe haraka kabla hajaleta madhara kwa Chama

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Nidhamu katika taasisi yeyote ile ni jambo la msingi sana, iwe sehemu ya kazi iwe jeshini, kwenye biashara, pesa zako bila nidhamu huwezi kufanikiwa.

Kiongozi anapoenda kinyume na maamuzi halali ya taasisi ni aidha anajiuzulu au anafukuzwa. Halima Mdee amekiuka maamuzi halali ya Kamati Kuu hence ya Chama, awe amefanya kwa kushinikizwa au kwa tamaa zake, kwa kitendo kile hana uhalali tena wa kuendelea kuongoza kitengo cha BAWACHA.

Mbali na kukiuka msimamo wa Chama Mdee kaonyesha tamaa na ubinafsi wa hali ya juu, kajiteua yeye wa kwanza bila aibu badala ya kuwatafuta wanawake vijana wengine ndani ya chama nje ya BAWACHA nao wakapate ujuzi bungeni kama yeye.

1. Halima Mdee - M’kiti BAWACHA Taifa
2. Hawa Mwaifunga - Makamu M’kiti BAWACHA.
3. Grace Tendega - Katibu BAWACHA.
4. Jesca Kishoa - Naibu Katibu Mkuu BAWACHA.
5. Asia Mohamed - Naibu Katibu BAWACHA.
6. Agnester Kaiza - Mwenezi BAWACHA Taifa.
7. Ester Matiko- M’kiti kanda
8. Nusrat Hanje - Katibu BAVICHA

Juliana Shonza alikuwa Makamu M/kiti wa BAVICHA nakumbuka alileta vurugu kubwa ndani ya BAVICHA kiasi kwamba kuchelewa kwa chama kumfukuza ilikuwa al manusura akigawe chama, ilikuja kufahamika baadae kumbe Juliana hakuwa peke yake alikuwa ametangulizwa kama chambo, nyuma yake walikuwepo kina Zitto, Kitila, Mwigamba na wengineo.

Chama kimshukuru Mdee kwa kuijenga BAWACHA na yote aliyokifanyia chama lakini kitendo cha yeye kama kiongozi kukiuka maamuzi ya chama hakiwezi kuvumilika na chama kikiendelea kumlea anaweza kuambukiza mbegu ya uasi ndani ya chama na kuleta madhara makubwa ‘irreparable’ kwa sababu hatujui walio nyuma yake ndani na nje ya chama ni akina nani na wana nguvu kiasi gani.
 
CHADEMA hivi hakuna kitengo cha intelligence? Kama mmeshindwa si bora muwe mnamsoma Kigogo2014 kule Twitter, maana kila anachokutabiri kinatokea.

Waombeni hao wahisani wenu, wawapeleke vijana nje wakasome ujasusi.
Huwezi kuendesha taasisi kubwa bila ya kuwa kitengo imara cha kukusanya taarifa, kuzichakata na kuzitafsiri.
Information is power
 
Chadema hivi hakuna kitengo cha intelligence? Kama mmeshindwa si bora muwe mnamsoma Kigogo2014 kule Twitter, maana kila anachokutabiri kinatokea.
Waombeni hao wahisani wenu, wawapeleke vijana nje wakasome ujasusi.
Huwezi kuendesha taasisi kubwa bila ya kuwa kitengo imara cha kukusanya taarifa, kuzichakata na kuzitafsiri.
Information is power
Mkuu ulitaka labda chama kifanye nini kuzuia hali hii.
 
Mnaonaje mkitulia tuli na msubiri wenye chama chao watoe kauli rasmi?

Kudhani kwamba wale akina mama wameenda bungeni bila ridhaa ya Mwenyekiti na kwamba labda wameforge barua ni uzwazwa na kutokuzijua siasa za Wapinzani wa Bongo. Sisi ni watu wa matukio

Kwa kuwa tuligoma kutoka nje na kuandamana kuwasupport pale walipotupwa lupango, wana haki ya kufanya maamuzi yao bila pressure kutoka kwa yeyote
 
Mnaonaje mkitulia tuli na msubiri wenye chama chao watoe kauli rasmi?

Kudhani kwamba wale akina mama wameenda bungeni bila ridhaa ya Mwenyekiti na kwamba labda wameforge barua ni uzwazwa na kutokuzijua siasa za Wapinzani wa Bongo. Sisi ni watu wa matukio

Kwa kuwa tuligoma kutoka nje na kuandamana kuwasupport pale walipotupwa lupango, wana haki ya kufanya maamuzi yao bila pressure kutoka kwa yeyote
Una maana watu wasitoe mawazo yao.
 
Wazee wa keyboard, Mdee kavuja damu, kalala selo, kapigwa virungu sababu ya CHADEMA na ni Mbunge wa CHADEMA sasa hivi kwa mujibu wa katiba ya nchi wala sio hisani, sasa hapa wewe mzee wa kwenye keyboard hujawahi hata kutokwa na jasho, sio hata damu kwa ajili ya CHADEMA unadai Mdee afukuzwe. Hovyo sana nyie. Mdee na wenzake hawajakurupuka, wana baraka za Mbowe.
 
Una maana watu wasitoe mawazo yao.
Kutoa mawazo ‘after the fact’ ni kupoteza muda.

Unapotoa wazo eti mtu ajiuzulu au aondolewe haraka wakati alichokifanya kwa ujasiri ndicho maamuzi na matashi ya viongozi wake huoni kama unapoteza muda wako?

Wanawapimia upepo kwanza waone reactions zenu then watatafuta namna ya kuhalalisha lililofanyika. Weka akiba ya maneno kwa sasa.
 
Wazee wa keyboard, mdee kavuja damu, kalala selo, kapigwa virungu sababu ya chadema na ni mbunge wa chadema sasa hivi kwa mujibu wa katiba ya nchi wala sio hisani, sasa hapa wewe mzee wa kwenye keyboard hujawahi hata kutokwa na jasho, sio hata damu kwa ajili ya chadema unadai mdee afukuzwe. Hovyo sana nyie. Mdee na wenzake hawajakurupuka, wana baraka za mbowe.
Mkuu Mdee hajavuja damu peke yake wala hakujichagua mwenyewe kuwa M/kiti BAWACHA kachagulia na watu ambao wengine ni marehemu kwa kumpigania yeye ajulikane, hata unaowaita wazee wa keyboard wana mchango wao kwake.
 
Kutoa mawazo ‘after the fact’ ni kupoteza muda.

Unapotoa wazo eti mtu ajiuzuru au aondolewe haraka wakati alichokifanya kwa ujasiri ndicho maamuzi na matashi ya viongozi wake huoni kama unapoteza muda wako?

Wanawapimia upepo kwanza waone reactions zenu then watatafuta namna ya kuhalalisha lililofanyika. Weka akiba ya maneno kwa sasa.
Wewe unajuaje alichofanya Mdee ni maamuzi ya chama.
 
Haya yanayotokea sasa ndio lengo kuu la CCM na ama kwa hakika wamefanikiwa kwa asilimia zote, "Divide and Rule" that's it.

Yule Polepole hayupo kwa bahati mbaya pale.

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Back
Top Bottom