Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA aidha ajiuzulu au aondolewe haraka kabla hajaleta madhara kwa Chama

Infact anayetakiwa kuwekwa pembeni ( to rescue himself) kwenye chama ni Anti ambaye amekitia hasara kubwa sana chama kifedha na kisiasa. Na baada ya kufanya hivyo yeye kuamua kusepa
 
Rafiki wa kweli mtamjua wakati wa njaa!! Atakuja adui atawatupia mfupa kuwapima imani yenu... ni kweli hapo ndipo utajua kiwango cha mshikamano wenu kikoje...
Uko sahihi, ila najua BAWACHA bado itakuwa imara hata bila Mdee.
 
Chama kina taratibu zake za kupata habari na kuzifanyia kazi may be huu ndio muda mwafaka wangefukuzwa mapema watu wangedhani wanaonewa.
Huo utaratibu umesaidia nini toka enzi za kuunga juhudi mpaka kina Mdee? kufukuzwa leo itasaidia nini,unadhani CCM itawaacha wafukuzwe?
 
Zitto na Tundu wanawadawanya chadema.Act haina cha kupoteza so long us zanzibar wana serikali ya umoja wa kitaifa.Chadema msipokubari hili la wabunge wa vitu maalum know that Zitto anawadanganya sana na alipiza kisasi akishirikiana na Lissu. You should know that hakuna uchaguzi tena till 2025.
 
Mnaamisha magoli,tatizo la Mbowe mwenye chama mnaliamisha kwa Mdee.
taasisi inayoongozwa na Mbowe aiwezikuwa madhubuti,madhaifu yake mengi yalizibwa na Dr,Slaa akiwa Chadema.
 
Chadema wamevurugana lakini wameelewana.Japo Katibu Mkuu anasema hana habari za kupeleka List ya wabunge lakini anayo habari ya figisu zilizotokea siku chache kabla akina Mdee kuapishwa.Hata hivyo kwanini chama kiliitikia wito wa kutengeneza list in the first place na kuituma NEC?

Yawezekana katika figisu hizo Mdee na wenzake walipata kuelewa kwanini Lissu na Zitto wamegangania wasiende bungeni. Labda ndio sababu iliopelekea wenye chama Chao kuingilia kati na kuwezesha akina Mdee kupewa ruksa kwenda kuapishwa. Bora wayamalize kimya kimya kwani wanaume wakijitia mbogo Mdee and Co watafungua mdomo.
 
Mkuu binafsi sina imani na CDM kama chama makini au taasisi imara....
Si wewe tu, wengi hatukuamini kama Halima Mdee anaweza kuwa kirusi ndani ya chama, yes Kigogo alionya ila wengi wengi hatukumwamini. Yametimia.

Kinachotakiwa baada ya uasi huu ni WAY FOWARD tu, ambayo tunaisubiri tuipate kupitia kwenye hiyo press ya leo.
 
Nidhamu katika taasisi yeyote ile ni jambo la msingi sana, iwe sehemu ya kazi iwe jeshini, kwenye biashara, pesa zako bila nidhamu huwezi kufanikiwa...
Yote hayo ndio mnayaona leo? je tukiwaita wanafiki tutakuwa tumekosea? hizo ngonjera zako hazisaidii kitu,leo ndio mnamuona Mdee hana nidhamu afukuzwe,mlipokuwa mnaambiwa huko nyuma kuwa Mdee hana nidhamu hatukisikia mkitoa mapovu hayo sabuni ya FOMA.
 
CHADEMA watakuwa walikaa kwenye drawing board wakaconsider critically faida za kususia then wakacompare na hasara zake. Huhitaji kuwa na degree kuona kwamba kuna hasara nyingi zaidi ya faida.

Muungwana huswallow pride pale anapogundua ameshashindwa vita na ni uzuzu kuingia vitani huku unajua kabisa umeshashindwa kabla hata risasi moja haijafyatuliwa kwa kuwa huna nyenzo za kupambana na adui

Maalim Seif nae anakwenda kukubali kule Jenji. Itakuwa zamu ya Zitto sasa kufanya mpango labda apewe vile viti maalumu vya Rais
 
Nidhamu katika taasisi yeyote ile ni jambo la msingi sana, iwe sehemu ya kazi iwe jeshini, kwenye biashara, pesa zako bila nidhamu huwezi kufanikiwa...
Huo ni mpango wa Mbowe hayo unayoyasema mkuu hayawezi kufanyika abadan mbowe anajuwa kila kitu hebu watokee waseme hiyobaruaya majina kwenda kwa nec imefojiwa tuone wasiposema hivyo mjue ni mbinu za mbowe hizo
 
Back
Top Bottom