Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Hapa Mwenyekiti ashafunga mjadala kwamba sio wanachama. Waendelee tuu bungeni ila chama hawana. Imeeisha
 
Eti "Wanachama wa hiari" nimecheka kinoma. Mume akikupa talaka tatu unajipa ka cheo ka "mke wa hiari".
Kama wanakipenda CHADEMA wasingekisaliti.
 
Ila CHADEMA wanapenda kutukana sijaona, aise wamemtukana huyu dada na Matiko matusi ya nguoni kabisa, ya kudhalilisha na kuwafanya kuonekana kama hawana haki au siyo binadamu!
Tunawashauri CDM waende taratibu, wasiwe na hasira kihivyo, waache matusi hata ikitokea mtu wao kahama chama...
"Don't hate the players, HATE THE GAME.."
 
Ila Chadema wanapenda kutukana sijaona, aise wamemtukana huyu dada na Matiko matusi ya nguoni kabisa, yakudhalilisha na kuwafanya kuonekana kama hawana haki au siyo binadamu!
Tunawashauri CDM waende taratibu, wasiwe na hasira kihivyo, waache matusi hata ikitokea mtu wao kahama chama...
"Don't hate the players, HATE THE GAME.."
Wakati wa kampeni walipokuwa wanatukanwa na wanaCCM wenzako walikuwa wanapakwa mafuta?
 
Halima hasizunguke,aseme majina ya wateule 19 yaliteuliwa vipi?na katika kikao gani na yalifikaje Tume?.
Hahaha hapo ndio tatizo lao kujiamulia kwenda CCM kuanzisha mgogoro, kama walitaka wao ndio waende wangeomba kwenye chama, kisha wasubirie majibu.

Kwasasa nitaishangaa CHADEMA ikibadilisha maamuzi ya kuwavua nyadhifa na kuwafukuza uanachama.

Kuwa wanachama wa hiari hakuwapi haki ya kuwa wabunge viti maalum. Kwasababu wanachama wote ni wanachama wa hiari, hakuna aliyelazimishwa kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Alipaswa kukanusha ubunge aukane kisha arudi chamani kujadili taratibu za kuomba kusamehewa, yeye kuwa mwanachama kwa miaka 16 hakumpi kinga kutokufukuzwa chamani.

Akafikirie upya, au amalizie taratibu zao za kujiunga na CCM.
 
Wapambe wa CHADEMA wangeweka akiba ya maneno, kina Hilda wametoa kila aina ya matusi sasa ndio watapewa somo la siasa. Mdee hawamuwezi alishapiga hesabu zake siku nyingi.
 
Jibu la 2010, 2015 kwamba kwanini walienda bungeni? Linajibika kirahisi kwamba documents ngazi zote zilikuwa wazi hata ziliweza kutumika mahakamani kupinga uchaguzi, Sasa 2020 wanalamika hawakupewa documents zozote kuanzia ngazi ya kata.
 
Watanzania ni kama tunachanganywa.

Spika Ndugai amesema wabunge 19 wanawake wa Chadema wananyanyasika kwa sababu chama hicho kina mfumo dume tena ni kampuni inayoongozwa na mtu mmoja.

Naye mwenyekiti wa Bawacha anasema yeye na wenzake 19 wamejengwa na Mbowe na kwamba watu wasiwachonganishe na kiongozi wao mkuu wa chama.

Sasa tushike la nani tuache la nani?

Au ndio za kuambiwa tuchanganye na za kwetu?

Maendeleo hayana vyama!
Hata wewe mzee mstaafu hujui la kufanya?
 
Back
Top Bottom