Halima Mdee: Mifuko ya Jamii hoi, pensheni hatihati kulipwa

28 Dec 2018

Magufuli : Trilioni 1.2, lililokuwa deni la serikali mifuko ya hifadhi ya jamii

Mh Rais asema wakati tunaingia madarakani tulikuta deni la Shilingi Trilioni. 1.2 kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini hadi kufikia machi 2017 tulimaliza kulipa madeni yote”- Rais @MagufuliJP
 
Ukitaka kujua watu wanasemaje kuhusu hii serikali ambayo imefanya tuwe donor country nenda kawaulize wastaafu watakupa majibu sahihi.

Ila wkt unawauliza hayo uwe umekaa distance ya 10m,usiniulize kwanini.
...😂😂😂... Wastaafu wamepigika mno awamu hii wengi wana madeni kibao tu.
 
...😂😂😂... Wastaafu wamepigika mno awamu hii wengi wana madeni kibao tu.
Acha kabisa mkuu na wala jamaa hawana habari sanasana kila wakipata nafasi ya kuongea utasikia wanaongelea mamiradi makubwa huku wakijisifu wanaitekekeza kwa kutumia fedha zetu za ndani.
 
Mkuu una hoja ya uhakika. Mbowe angetoka mwaka huo akaruhusu damu mpya asingekuwa anapata shida hizi. Mwaka jana aliogopa kutoka kwa sababu aliona akitoka watasema anakimbia baada ya kuona chombo kinaenda mrama; akajiapiza kwamba wacha kimfie tu. Kweli naona CHADEMA kinakata roho mikononi mwake.
CHADEMA ilikuwa na historia nzuri ya kurithishana madaraka kuanzia Mzee Mtei na Bob Nyanga Makani. Pia akina Mzee Brown Ngwilulupi. Alivyoingia Mbowe sijui kabadili Makamo Wenyeviti wangapi? Makatibu wangapi lakini YEYE YUPO! Kamkuta Kabourou, kaondoka yeye yupo! Kaja Slaa kaondoka Mboqe yupo! Kaja Mashinji katoka Mbowe yupo!!! Chacha Wangwe, kaja kaondoka; MBOWE YUPO! Mzee Arfi kaja kaondoka, MBOWE YUPO! Kaja Prof Safari kaondoka, MBOWE YUPO!! Lowassa kaja kaondoka, Mbowe yupo! Sumaye kapita, Mbowe YUPO!
Na uzuri ni kwamba Mbowe akiondoka na hela za kuwalipa wastaafu zitapatikana kwa wingi maana inaonekana mbowe ndiye amezuia pesa hizo.
 
Tatizo la Mifuko ya jamii katika awamu ya 4 lilichukuliwa Kisiasa kwa ajili ya kuwafurahisha wastaafu.
Tunasema Watanzania wote ni sawa lakini ukiangalia kilichofanyika katika awamu ya 4 ya uongozi wa Inchi kuhusu wafanyakazi utaona kuwa hakuna usawa.
Katika awamu ya nne wafanyakazi walipandishwa sana mishahara na mafao yao.
Mtumishi moja mwenye cheo cha kawaida kabisa ambaye kabla ya 2005 alikuwa analipwa mafao ya shilingi 6,000,000 na pesheni ya mwezi ya shilingi 200,000, mtumishi wa cheo kile kile katika miaka ya 2010 na kuendelea wamekuwa wanalipwa mafao ya shilingi zaidi ya 100,000,000 na pesheni ya mwezi ya shilingi zaidi ya 1,000,000.
Wastaafu wa namna hii ni wengi na makusanyanyo toka kwa wanachama walioko kazini ni kidogo kwa hiyo mifuko inakosa pesa za kuwalipa wastaafu pesa kwa haraka.
Pia mifuko mingi ilijiingiza kwenye kujenga majumba ya biashara nayo hayana marejesho mazuri.
Maamuzi mengi yaliyofanywa kwa maslahi ya Wafanyakazi yataendelea kuwaathiri kama kiko kotoo hakitabadilishwa ili kiendane na mapato.
 
Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA ndiyo anayezuia serikali ya awamu ya tano isiwalipe wastaafu stahiki zao?

Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA ndiyo kilichosababisha serikali ya awamu ya tano kupandisha makato ya bodi ya mikopo kutoka 8% to 15%?

Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA ndiyo kinachosababisha ongezeko la mafukara wengi katika taifa eeh ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Mbowe angeheshimu Demokrasia ndani ya Chama kama ilivyoasisiwa na waasisi wa Chedema kwa ajili ya maendeleo ya nchi kupitia upinzani makini leo Chadema ingekua chini ya Zito Zuberi Kabwe kijana asiye na chembe ya uoga.
Awamu ya Tano ingekua na wakati mgumu sana kwa wananchi.

Hayo uliyoyataja yamesababishwa na serikali yenyewe lakini watanzania hawaoni pa kukimbilia mana Tegemeo lao lilikua ni Chadema na Chadema imekosa uongozi wenye nia ya dhati kulikomboa Taifa hili.
Sasa watu wanaona ni bora upinzani ubaki ndani ya CCM mana huko wanawatumia vizuri wale wenye maono makubwa Toka upinzani.
Leo hii Tundu Lisu akirudi CCM atakua na nafasi kubwa ya kuwa waziri wa Katiba na Sheria au Mwanasheria mkuu wa serikali na kulisaidia Taifa letu kuliko kukaa kwenye Chama kinachoendesha mambo yake kama CCM au kwa ubaya zaidi.

Mbowe alikua na nafasi kubwa ya kuivuruga CCM endapo angejenga Demokrasia ndani ya Chama chake.

Kukubali Demokrasia ndani ya Chama au serikali ni jambo gumu sana na linahitaji na linahitaji kujengwa kuanzia ndani ya vyama ambavyo vinategemewa kuunda serikali .
Sasa He,ndani ya Chadema kuna Demokrasia ?
Hivi Mbowe anaona hasara gani kuwaachia wenzake baada ya muda wake kuusha Mara ya nne sasa?
Hivi angewashukuru watanzania na kuwaomba waendelee kupigania Demokrasia ingekua na tatizo gani?

Angeimarisha chaguzi huru ndani ya Chama mana huko ndiko kipimo cha serikali ya Chedema kilipo lingekua ni jambo LA kuigwa sana.
Demokrasia ina gharama kubwa sana ikiwa ni pamoja na kuachia madaraka wakati bado mtu anayapenda au wananchi bado wanampenda.
Kupendwa kwa Mbowe na baadhi ya wanachama au viongozi wa Chama sio sababu ya kukiuka Miongozo na miiko iliyokuwa imewekwa na waasisi wa Chama.
Kuvuruga katiba na kuondoa kikomo cha uongozi kiliwakera watu wenye maono ndani ya Chama na kukifanya kuwa Chama chenye migogoro ya ndani isiyoisha na inayosulihishwa kwa kufukuzana.
Kufukuzana ni kupunguza nguvu ya Chama na shahidi ni CCM. Kufukuzana kwa Chadema kusilinganishwe na CCM kwani CCM wanasimama na dola kudhibiti wale wanaowafukuza. Na kama sio nguvu ya dola CCM ingeathirika sana na fukuza fukuza japo sio kubwa kama Chadema.

Chadema wasiige tu mfumo wa kufukuzana kwani ni mfano mbaya kidemokrasia. Mtu apewe nafasi ya kujieleza na kusikilizwa na hata kuonywa na sio vinginevyo ndiyo gaharama ya kujenga Demokrasia,uwazi na utawala bora ndani ya Chama na serikali.

Haya ndiyo majibu ya maswali yangu hapo juu ?

Ndiyo maana huko kwenu mmeamua kikodi wapinzani ili wawasaidie kwenye Baraza la mawaziri.

Wengi wenu hamnazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom