Halima Mdee: Jumba la Mch. Rwakatare nalo libomolewe ili Kuepuka Double Standard! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halima Mdee: Jumba la Mch. Rwakatare nalo libomolewe ili Kuepuka Double Standard!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Boflo, Sep 30, 2012.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,393
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.

  Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare, zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.

  Julai mwaka huu, nyumba za wananchi waliojenga katika maeneo tengefu ya ufukwe wa Jangwani, mto Ndumbwi na mto Mbezi, zilibomolewa katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (Nemc).

  Operesheni hiyo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta nane. Lakini cha kushangaza nyumba ya Mchungaji Lwakatare ambayo imejengwa kinyume cha sheria haikuguswa
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,872
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  PICHA: HEKALU JIPYA LA MCHUNGAJI MAMA RWAKATARE  [​IMG]
  Muonekano wa mbele wa hekalu la Mchungaji Rwakatare
  [​IMG]
  MC na mchungaji Haris Kapiga wa Clouds FM
  [​IMG]
  Mc Harris Kapiga akiwa kazini.
  [​IMG]
  Watu wakijiachia
  [​IMG]
  Kabati la vyombo
  [​IMG]
  Akiwa katika ofisi yake ya nyumbani, kuna sehemu ya kufanyia mikutano, Salon, Studio, na sehemu ya mazoezi.
  [​IMG]
  Wadau wakijiachia kwenye moja wapo ya kochi la kifahari mjengoni humo
  [​IMG]
  Wakati wa msosi
  [​IMG]
  Mambo ya dressing table
  [​IMG]
  Kitanda chake cha kulalia
  ---
  Mchungaji Getrude Rwakatare amehamia rasmi katika nyumba yake mpya iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya Hindi. Inaripotiwa kuwa waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika mahali hapo kwa kushuhudia nyumba yake hiyo ya kifahari.
  Kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba nyingine ya kifahari pia.

   
 3. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Sidhani kama suala hilo litawezekana, lakini na hao NEMC walikuwa wapi wakati jamaa wanatandaza beam mpaka leo ndio waje bomoa?????????????????????????????
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono 100% Libomolewe tuu! sheria msumeno bana.
   
 5. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,341
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Sheria inatakiwa iwe active pande zote!!!
   
 6. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 7,189
  Likes Received: 693
  Trophy Points: 280
  Kubomoa sawa ila wakati mwingine ha waliopo madarakani lazima wawajibike kuanzia wanasiasa na watendaji nikiwa na maana na diwani wa kata husika (hawa mara nyingi hujifanya kuwa upande wa wananchi kwa kujifanya kuwatetea pindi wanapovunjiwa wakati alikuwa ana nafasi ya kuwashauri waache - wazushi hawa sometimes), meya wa jiji, mkurugenzi wa manispaa, afisa ardhi na kama kuna building permit basi idara nyingi zinaingia maana kibali cha kujenga kina sahihi za watu wengi kuanzia mipango miji, afya, wahandisi anbao wanatia sahihi ku-justify kwamba ujenzi ni salama kujengwa eneo husika (HII ITAUA UTARATIBU WA WATU KUPIGA SAHIHI BILA KUJUA KIUNDANI ENEO HUSIKA - WANAFANYA DESK BASED JOB)
   
 7. k

  katalina JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani waliobomolewa walikuwa walala hoi? au hatujui maana ya mlalahoi........!
   
 8. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,884
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mnataka mlima wa moto ubomolewe? Nadhani huo nao ni upepo na utapita tu.
   
 9. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,172
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Sheria inawaminya masikini majizi ya sadaka kama haya nevaeva hili mama sizani kama ni safi.
   
 10. m

  makeda JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hahahahahaha!mkuu umenichekesha sana,Dah!

  Stop using God as a form of manipulation to get what you want out of people
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,800
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Labda Lwakatare ahamie chadema ndo litabomolewa
   
 12. Micha

  Micha JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyo ana vibali vyote vya kujenga hiyo nyumba, kwahiyo kabla ya kubomoa Serikali iwashughulikie kwanza waliompa ruhusa ya kujenga, na kwanini hawakusimamisha ujenzi wakati unaanza wanasubiri mpaka mtu anahamia?
   
 13. Root

  Root JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 19,891
  Likes Received: 5,140
  Trophy Points: 280
  jamani si vibali amepewa au wanataka watu wafe kwa presha? we hela zote halafu wavunje ahahaha
   
 14. N

  Ndinimbya Senior Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hilo swali ulitakiwa uulize tangu wameanza kubomoa za awali, siyo kwakuwa wanataka kuishusha nyumba ya bepari aliyevaa ngozi ya uchunagaji.
   
 15. B

  Big GM Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi tunamwomba mama mchungaji atuambie ni sadaka au ni ruzuku za ubunge?naomba takukuru wanchunguze huyu mama
   
 16. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 364
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili nalo neno. Ila atajitetea shule zake.
   
 17. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,005
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hivi halima mdee hana kingine cha kufanya zaidi ya (kuongelea ) kuvunja majumba ya watu. Au kuna masilahi huko kwenye kuvunja vunja?????
   
 18. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,562
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  Unajenga mtoni mvua ikija maji yanabomoa madaraja huyo mtu serikali ipi itamvumilia?!!
   
 19. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,562
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  To my knowledge sio kazi ya Nemc kugawa viwanja...so mtu mwenye akili atafanya search mwenyewe kujua eneo analojenga nyumba ya dhamani kama hii ni salama kisheria
   
 20. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160

  Poverty mentality.
   
Loading...