Halima Mdee: Elimu bila malipo maana yake serikali imeshindwa elimu bure, tujiandae na michango

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
IMG-20170420-WA0034.jpg
IMG-20170420-WA0035.jpg

Ukawa tukisema hawa wanakurupuka kucopy na kupest mnakuwa wakali mnadai uchochezi, elimu bure imewashinda sasa wazazi wajiandae kuletewa michango waliodai wameifuta
 
Tehehe! Halima bhana,pale msalato mzee Mdee Yahya,alikuwa hakugharamii chochote? Yaani unaenda tu,daftari,kalamu,unavikuta huko huko.
 
Aliyekosea sana atakuwa ni pombe au naye hajui maana alisema "NIKISEMA BURE NI BURE KWELIKWELI"!! kamavipi mmwambie afute kauli...
Kimsingi hiyo bila malipo nayo mshafeli maana kunawaraka umetolewa kuwa michango yoote iidhinishwe na DED. Badilisha tena chawene nadhani mlisema elimu bila malipo mengi.
 
View attachment 498819 View attachment 498817

Ukawa tukisema hawa wanakurupuka kucopy na kupest mnakuwa wakali mnadai uchochezi, elimu bure imewashinda sasa wazazi wajiandae kuletewa michango waliodai wameifuta
Kwenye kampeni ALITUAMBIA, "...MKINICHAGUA SERIKALI YANGU ITATOA ELIMU BURE KUANZIA DARASA LA KWANZA HADI SEKONDARI..... ".

Hii misamiati mingine ya KIPUUZI inatoka wapi??????!!!!!!!!
 
Mdee kichwa maji anataka serikali inunue hadi sare za wanafunzi na madaftari?
Sare ni miundominu?
Shule hazina vitabu, mfano vile vya fasihi. Ukimwambia mzazi amnunulie mwanae kitabu anakwambia elimu ni bure.
Shule zingine zina upungufu wa madawati hadi leo. Hali hii imechangia kudorora kwa elimu kwa sababu watoto wanakwenda kwa shift 2 na hivyo kupunguza idadi ya vipindi darasani. Hatimaye mihtasari haimaliziki. Ukikaa na wazazi/walezi kujadili namna ya kuliondoa tatizo hili, wanakwambia wanaisubiri serikali.
Matokeo ya mitihani mwaka huu ni trela tu, picha lenyewe linakuja.
 
Yote haya yanafanyika kwa sababu CCM inatujua vema watanzania! Na mwaka 2020, trust me kuna watanzania wengi wataipigia CCM kura zao iendelee na mazingaombwe yake.
 
Ni kweli unapewa nyingine na baba yako.
Inawezekana hukusoma kipindi hiko...Madaftari na kalamu vilikuwa vinatolewa bure shuleni (shule ya msingi). Kwa Sekondari kwa waliosoma shule za kutwa mchana msosi ulikuwa bure shuleni na ada ya shilingi elfu nne kwa muhula.
 
Hapo mkuu ndipo kiswahili kimegongana umesema kulikuwa na ADA. Sasa bure vipi tena?
 
Back
Top Bottom