Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee juzi alifanya ziara ya kuwatembelea wapiga kura wake kuwashukuru kwa kumchangua ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao.
Akiwa maeneo ya Jogoo alishangazwa na kutokuwaona viongozi wa serikali za mitaa pamoja na diwani wa kata usika,
Ndipo alipojitokeza mwananchi mmoja ambaye alimwambia kuwa viongozi hao wamepewa amri ya kutokumpa ushirikiano, na atakaye kiuka amri hiyo ataondolewa kwenye nafasi yake...
Mdee alionekana kutokushtushwa na maneno hao na kuwaambia wananchi kuwa taarifa hizo anazo na kuwa amepita baadhi ya sehemu na kukutana na vitu kama hivyo, akawaambia kuwa sehemu hizo walizonyima ushirikiano ameunda kamati iliyo shirikisha wananchi wa maeneo usika ambao watakuwa wakiwasilisha kero zao kwake....
Ulipofika muda wa wananchi kueleza kero zao,alishangzwa na hofu waliyokuwa nayo wananchi ya kushindwa kuelezea kero zao zinazo wakabili kwenye maeneo yao,aliwaambia hawapaswi kuwa waoga na kuwatolea mfano wa yeye mwenyewe kuwa endepo angekuwa mwoga asinge shinda ubunge, bali ujasiri na uthubutu wake ndio uliomfikisha hapo...
Alimalizia kwa kuwaambia kama wanaogopa kutoa kero zao wana mpunguzia kazi....
Kwa kweli nimesikitishwa sana vitendo vya watendaji waserikali za mitaaa, na hii ni kampeni ya ccm ya kutaka ashindwe kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kama alivyo sema mwenyewe Mdee.
Nilifuatilia baadhi ya hizo ziara za Mdee. niliona kwamba organisation ilikuwa na matatizo. kwanza ni kweli CCM wameamua kutotoa ushirikiano kwa CHADEMA kutokana na kitendo cha ile Parliamentary-walkout, ambayo wanaitafsiri kama kumvunjia heshima rais na mwenyekiti wa CCM. lakini pamoja na hilo, inaonekana kuna watu wa serikali za mtaa mbalimbali katika jimbo lake ambao wako tayari kushirikiana naye, wanatofautisha serikali na chama. lakini badala ya yeye kuwasiliana nao na kuweka utaratibu wa kutembelea maeneo, yeye au katibu wake wanatoa tu taarifa za kutembelea mahali. kwa maana hiyo hata wale wenyeviti wa mitaa ambao wangekuwa tayari kutoa ushirikiano, wanawaweka pembeni na kuwakatisha tamaa.
halafu nimeshuhudia katika baadhi ya maeneo, hao wanaochaguliwa kuwa ndio kamati ya kukusanya kero na kuwasiliana naye, wengine kwa kweli usingeweza kusema kwamba ni watu makini. nadhani ana very hard times ahead. itabidi ajipange vizuri. kuna mtu alishauri kwamba pengine angekuwa na program of action yake mwenyewe kutokana na ahadi zake na utafiti wake, angeanza na hiyo kwanza. pia awe mwangalifu na hizo kamati za kero, zisijekuwa ni vikundi vya walaji wengine.
mwisho namshauri asiendekeze sana jazba katika utendaji. pamoja na ujana wake, ajifunze kuwa mtulivu. ameshashinda kiti, awe conciliatory ili kupata cooperation ya wengine, kama anavyofanya obama sasa hivi kwa Republicans