Uchaguzi 2020 Halima Mdee apelekwa kupekuliwa nyumbani kwake na Jeshi la Polisi baada ya kwenda kuripoti matukio ya kutishiwa amani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,632
218,060
Jeshi la Polisi limemkamata mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Dada Halima Mdee na sasa wanakwenda naye kumpekua nyumbani kwake Mbweni.

Halima Mdee alikwenda kuripoti Polisi juu ya Matukio ya kutishiwa Amani lakini cha kushangaza alipofika amewekwa chini ya Ulinzi.

polisi.JPG

=====
Mdee ahojiwa kwa tuhuma za kumiliki vifaa vya kunasa sauti

Mgombea ubunge Kawe (CHADEMA), Halima Mdee jana Ijumaa Oktoba 23,2020 alikamatwa na jeshi la polisi kituo cha Mbweni na kuhojiwa kwa tuhuma za kumiliki vifaa vya kunasia sauti kinyume na sheria za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Edwrd Bukombe alipotafutwa na gazeti hili kutolea ufafanuzi tukio hilo alisema hadi saa 1:20 jioni mgombea huyo alikuwa nje lakini akisisitiza kuwa hajawasiliana na waliomhoji, akiahidi kuwa atakapowasiliana nao atatoa ufafanuzi zaidi muda ambao wakili wa Mdee, Edson Kilatu alisema mgombea huyo muda huo alikuwa akitoa maelezo kituo cha polisi.

Hata hivyo jana saa 3 usiku Kilatu alisema Mdee aliachiwa kwa dhamana baada ya kuchukuliwa maelezo na kutakiwa kuripoti polisi atakapohitajika.

Awali, Kilatu alisema Mdee alishikiliwa kituoni hapo baada kwenda kuripoti tukio la watu wanaomuwinda kutaka kupanga kwenye nyumba iliyopo jirani.

Alisema baada ya Mdee kushikiliwa na jeshi la polisi lilifanya upekuzi nyumbani kwake kwa zaidi ya saa moja na kuondoka na kompyuta mpakato moja.

“Baada ya kwenda kuripoti na kuandika maelezo ndipo polisi walipokuja na hoja ya kumiliki vifaa vya mawasiliano kinyume na sheria za TCRA ambapo baada ya kufanya upekuzi wameondoka nae na kurudi kituoni,”alisema Wakili Kilatu.

Meneja kampeni wa Mdee, Felista Njau alipotafutwa na gazeti hili alisema asubuhi mgombea huyo alienda kutoa taarifa kituo cha polisi Mbweni kuwa kuna magari yanayomfuatilia yakiwa na namba tofauti.

Alisema baada ya kufika kituoni hapo aliwekwa chini ya ulinzi na kuelezwa kuwa kuna jalada lake kituoni hapo nakutakiwa kwenda kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake.

Juzi katika ukurasa wake wa Twitter,Mdee aliandika “Kesho nitaripoti Polisi…,kuna watu wananifuatilia nyumbani kwangu, wanaongeza dau kwa nyumba ya jirani yangu (ghorofa ambalo halijaisha) ili waweze kukodi chumba ili wafanye yao ,nilisema juzi naona hamjakoma leo mmekuja tena nakuongeza dau. Tusilaumiane.”
 
Dada yetu alienda kuripoti polisi juu ya kuhofia usalama wake lakini polisi wa kituo cha Mbweni wamemweka chini ya ulinzi na wanaenda kupekua nyumbani kwake hapo Mbweni.

Taarifa zaidi zitakujia.

Nimepenyezewa toka ndani ya kambi ya ushindi wa Mdee hapo Kawe.
 
Back
Top Bottom