Halima Mdee amewataka Watanzania kumpa nafasi Rais Samia Suluhu na kuachana na tabia ya kuhoji wanawake wanapokuwa viongozi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,497
9,278
Mbunge wa viti maalum, Halima Mdee amewataka Watanzania kumpa nafasi Rais Samia Suluhu na kuachana na tabia ya kuhoji wanawake wanapokuwa viongozi.

Mdee alitoa kauli hiyo jana Ijumaa Machi 26, 2021 akiwa wilayani Chato Mkoa wa Geita katika shughuli ya kumuaga Hayati John Magufuli.

“Tumepata Rais mpya Samia Suluhu tunaamini atafanya kazi nzuri, watu wampe nafasi kwa sababu tuna tabia ambayo si nzuri sana ya kuhoji wanawake wanapopata nafasi wakati wao ndio wanaofanya kazi kubwa majumbani kuhakikisha wengi wanafika mbali, basi tuamini kwamba rais wetu anaweza kutuletea maendeleo katika nchi yetu.”

“Ushauri ambao ninaweza kumpa Rais Samia aangalie mapungufu ya aliyemtangulia hasa masuala ya demokrasia na uhuru wa kujieleza na kuhakikisha anarudisha demokrasia iliyokuwepo kabla ya mwaka 2015 pamoja na changamoto zake,” amesema Mdee.

Mdee ambaye alifukuzwa uanachama Chadema pamoja na wenzake 18 wakidaiwa kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho amesema, “ninaamini akiwa makamu wa rais kuna vitu alikuwa anaona kwa jicho jingine ambalo rais alikuwa halioni.”

“Alikuwa amezungukwa na wapambe na sasa atatumia nafasi hii kuyafanyia kazi mazuri ambayo mtangulizi wake aliyafanya ayaboreshe zaidi.”

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu nae hebu anyamaze pumbavu zake. Haoni upumbavu aliofanya?!

Helafu anataka kuaminiwa.

Swali ni hivi, mpo safarini dereva ghafla kaumwa ameshindwa kuendelea na safari kisha utingo akashika usukani. Unadhani swali la kwanza litakuwa ni nini?!

Watu wana haki ya kumhoji bi mkubwa hili taifa linachangamoto na ombwe kubwa sana la maadili ya kiuongozi kiasi kwamba ni mtihani sana kuamini kirahisi kuwa mama ataweza.
 
Huyu nae hebu anyamaze pumbavu zake. Haoni upumbavu aliofanya......?!

Helafu anataka kuaminiwa......


Swali ni hivi, mpo safarini dereva ghafla kaumwa ameshindwa kuendelea na safari kisha utingo akashika usukani.... Unadhani swali la kwanza litakuwa ni nini?!

Watu wana haki ya kumhoji bi mkubwa hili taifa linachangamoto na ombwe kubwa sana la maadili ya kiuongozi kiasi kwamba ni mtihani sana kuamini kirahisi kuwa mama ataweza....
Halima mwenyewe anaweza akawa chanzo cha alama ya kuuliza ( ?), maana hana uwezo wa kutunza kauli 'public figures have to keep their words '
 
Halima is simply trying to serve a right table with a wrong dish, yeye mwenyewe ni 'mbunge' wa zao la 'mazingaombwe' ya Meko.

Si katiba yetu wala japo ya jirani yetu inaweza mtambua Halima kama mbunge, ajikague kwanza yeye kama ana moral authority ya kutoa ushauri kwa Madam.
 
Wahabarishaji muanze kutupa mambo ya kimapinduzi yaliyo fanywa na Wanawake walio wahi kushika maongozi ya mataifa yao. Kina Magreth Thacher, Indirra Gandhri, nk.
 
Viongozi wote Tanzania huchaguliwa kwa kufuata sheria na kwa mujibu wa kikatiba,

Mpaka leo hii pamoja na katiba yetu yenye mapungufu makubwa hakuna chama wala mtu binafsi aliyehoji mchakato au uwezo wa mheshimiwa Rais mama Samia

Haya maneno ya Halima yanalenga kupewa huruma na ngao kwenye kesi ya COVID-19 19 ya kuingia bungeni kwa kupitia mlango wa gereji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom