Mbunge wa Kawe-CHADEMA Halima Mdee amepongezwa na wananchi wa eneo la Mji Mpya Mzimuni kwa jitihada zake kubwa zilizopelekea kupatikana mradi wa maji eneo hilo.
Wakihojiwa na Clouds TV wananchi kadhaa wa eneo hilo wamesema kwamba wamekuwa wakipata shida ya maji kwa miaka mingi na maji waliyokuwa wanatumia ni ya chumvi tu.Wamesema hiyo ni kero ya miaka mingi ambayo wabunge wote waliopita walishindwa kutatua.
Hata hivyo wananchi hao wa vyama tofauti tofauti vya kisiasa wamesema alipokuja Halima Mdee na kusikiliza matatizo ya wananchi hao kwa muda mfupi ametafuta ufadhili ambao kwa kushirikiana na Manispaa eneo hilo limepatiwa mradi wa maji safi.
Wananchi hao wamewataka wabunge wengine kuiga mfano huo huku wakimwagia sifa kemkem mbunge huyo wa Kawe.
Source:Clouds TV Habari.