Halima Mdee aibuka shujaa Kawe

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mbunge wa Kawe-CHADEMA Halima Mdee amepongezwa na wananchi wa eneo la Mji Mpya Mzimuni kwa jitihada zake kubwa zilizopelekea kupatikana mradi wa maji eneo hilo.

Wakihojiwa na Clouds TV wananchi kadhaa wa eneo hilo wamesema kwamba wamekuwa wakipata shida ya maji kwa miaka mingi na maji waliyokuwa wanatumia ni ya chumvi tu.Wamesema hiyo ni kero ya miaka mingi ambayo wabunge wote waliopita walishindwa kutatua.

Hata hivyo wananchi hao wa vyama tofauti tofauti vya kisiasa wamesema alipokuja Halima Mdee na kusikiliza matatizo ya wananchi hao kwa muda mfupi ametafuta ufadhili ambao kwa kushirikiana na Manispaa eneo hilo limepatiwa mradi wa maji safi.

Wananchi hao wamewataka wabunge wengine kuiga mfano huo huku wakimwagia sifa kemkem mbunge huyo wa Kawe.

Source:Clouds TV Habari.
 
Ahsante kwa taarifa mkuu. Sijui gamba MAFILILI litaficha wapi sura yake?
 
safi sana mbunge wetu,njoo na huku mbezi juu,maeneo ya jogoo mabomba ya wachina hayatoi maji,tumefuatilia dawasco hadi tumechoka!karibu muheshimiwa
 
safi sana mbunge wetu,njoo na huku mbezi juu,maeneo ya jogoo mabomba ya wachina hayatoi maji,tumefuatilia dawasco hadi tumechoka!karibu muheshimiwa

Huko Mzimuni ni wapi?
Hapa sehemu hizo za Mbezi hakuna barabara, si za halmashauri wala tanroads.
Wananchi wanachanga mpaka wamechoka.
 
Clouds wemesifia wabunge chadema ujue hiyo ni kweli na haina chenga.!
 
Hongera kamanda halima kwa kuwapigania wanyonge wa nchi ambao wamekatishwa tamaa na magamba kwa kufanyiwa fadhila hata ya maji ambayo ni haki ya msingi kwa binadamu.
 
Safi sana Mdee...Juzi Mnyika alikua kwenye kijiwe kimja cha kahawa pale Manzese wananchi walifarijika sana na wakaomba siku nyingine arudi tena...seems jinsi wananchi wanavyowaubali makamada wa CDM
 
Back
Top Bottom