Halikuwezekana huko nyuma ila Waziri Ndalichako ameliweza, apewe tuzo ya heshima mapema tu!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Karibia katika awamu zote za Uongozi hapa nchini Tanzania kuanzia ya Hayati Nyerere, Mwinyi, Mkapa na ya Kikwete huku ukiiondoa hii ya sasa ya Shujaa kutoka Chato Rais Dkt. Magufuli mara nyingi sana Mitihani ya ama darasa la Saba au Form Two au Form Four au Form Six huvuja mno kisha kupelekea Tanzania kupata ' Wasomi ' wa ' hovyo hovyo ' ambao kimsingi yawezekana ndiyo wameifikisha Tanzania hivi na kuichelewesha Kimaendeleo.

Jana usiku hadi mida ya Saa 7 niliamua kufanya ' utafiti ' wangu mwenyewe wa kwa kupitia maeneo mbalimbali ambapo Wanafunzi wa Kidato cha Sita walikuwa wakijiandaa na Mitihani yao ya kumaliza ambayo wameianza rasmi leo nione kama nitakutaka na ' Feki Papers ' nyingi kama ilivyokuwa kawaida huko nyuma.

Nikiri tu kuwa kwa mara ya Kwanza tangia nchi hii ijipatie Uhuru wake miaka 50+ jana usiku hadi leo Wanafunzi walipomaliza kufanya Mitihani yao ya Kwanza ndiyo nimegundua kuwa hakukuwa na Mtihani wowote ule ambao ' uliliki / ulivuja ' kama ambavyo ilikuwa ' desturi ' huko nyuma.

Ifuatayo ni nukuu yangu moja tu ambayo niliipata baada ya kuhojiana na Mwanafunzi mmoja juu ya Mitihani yao hii na kama kuna ' Feki ' lolote walipashana nalo jana usiku na leo asubuhi kabla ya kuanza Mtihani wao na jibu lake jioni hii alipotoka chumba cha Mtihani lilikuwa ni kama lifuatalo
" Duh Kaka hakika Mama Ndalichako kabana na mpaka sasa nimeshafungwa mbili bila ( akimaanisha idadi ya Mitihani aliyoifanya leo ) kwani jana usiku tumeletewa Feki kama Sita hivi tena na Watu ambao tunawaamini kabisa wanaotoka huko huko Jikoni lakini unaambiwa leo tumeingia chumba cha Mtihani ile kuambiwa tu tuangalie pepa hakuna hata moja tuliloliona katika yale Mafeki yote Sita ya jana usiku. Huyu Mama ( Waziri Ndalichako ) balaa na sijui Rais Magufuli kamtoa wapi kwani anakaba utadhani Alesandro Nesta Beki wa Italia. Kwa dalili hii ya leo Kaka nakuambia tena kwa kukuhakikishia kabisa kuwa mwaka huu tutafeli sana na Wazazi wetu watatusamehe tu Mama Ndalichako noma sana " mwisho wa kumnukuu huyo Dogo Mwanafunzi.

Hivyo kwa ' tathmini ' hii tu fupi nami naungana nae ' Dogo ' kwa kuongezea kusema kuwa kama Tanzania ' imebarikiwa ' kuwa na Waziri ambaye ama hakika anaitendea haki nafasi yake na ni kama vile Kipele kimempata mkunaji basi ni Waziri wa Elimu Professor Mama Joyce Ndalichako. Huyu Mama hata tu ' rekodi ' yake huko nyuma ni ya ' kutukuka ' kabisa na pengine huyu nadhani ndiyo ameupata ' Uprofesa ' wake kihalali kabisa kuliko wale wengine wa ' hovyo hovyo ' wa Buguruni, Maji na Mstaafu Nguli wa Katiba UDSM kipindi hiko.

Bila kuchelewa kwa hii picha tu ya leo ya Mitihani ya Form Six kushindwa ' Kuliki ' kama tulivyozoea au tulivyozoeshwa huko nyuma kupitia awamu zote Nne ( 4 ) nadhani Waziri Professor Joyce Ndalichako anastahili TUZO ya HESHIMA kabisa kwa kuweza kurudisha ' nidhamu ' ya Elimu na Taaluma hapa nchini Tanzania na Watanzania wote tunatakiwa kuanzia sasa tumuunge mkono huyu Mama ili aturejeshee Elimu yetu katika Ubora wake tuweze kushindana na majirani zetu Kenya, Uganda na Rwanda.

Nawasilisha na enyi ' Madogo ' wa Form Six ' Kazeni ' kwani awamu hii ya Tano ( 5 ) siyo ya Ki sport sport na habebwi Mtu hapa na hivi maisha sasa ndiyo yanazidi kuwa magumu a.k.a tight mkifeli tu mjue kuwa safari ya Wazazi wenu kuwarudisheni Vijijini kuvuna Mpunga na Mbaazi itakuwa imewadia na humu mijini tutabaki sisi tu Great Thinkers ' tuliotukuka '. Shauri zenu!!!!!!!
 
Elimu ya Tanzania inapima uwezo wa kukariri na si uelewa wa mtu hivyo,hao wasomi wa hovyohovyo wataendelea kuwepo hadi pale mfumo mzima wa elimu utakapobadilishwa....

Kama waziri hatoliangalia hili kamwe hatopita katika mawazo yangu kama shujaa bali upepo uliofuata mgandamizo wa hali ya hewa..

Alafu pia, usitoe hitimisho kwa kuangalia mtu mmoja maana haileti picha kamili
 
Labda mwaka huu 2017 ila mwaka Jana 2016 mbn ilivuja na ndalichako waziri itakuwa umeongea na shule znazovujishiwa mtihani na siyo mabigwa wa kununua pepa na maana shule za kawaida

Nimeanza kumpima mwaka huu kwani ' technically ' tu mwaka jana wote alikuwa bado anafanya Office ' familiarization ' na mwaka huu Ofisi ' imemkubali ' na ' matunda ' yake ndiyo kama hayo unayoyaona Mkuu wa ' Madogo ' kulalamika kukosa ' Feki Pepaz ' kama walivyozoea na kujikuta wanalishwa tu ' matango pori ' na Matapeli wa Taaluma.
 
Sasa kama mitihani haivuji halafu Bashite anabadili mpaka jina na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar unajivunia nini hapo?
 
Mkuu umepita wapi na wapi???...Isije ukawa umepita shule za serikali walala hoi afu unakuja toa conclusion hapa...

Nimepita Shule zote kuanzia za Saint, Academia na Kayumba za hapa jijini Dar es Salaam na hata ile mvua ya jana usiku imenikutia nikiwa mitaani nafanya hii ' tafiti ' ndogo tu Mkuu. Huyu Mama Watanzania tunatakiwa tumpe TUZO upesi sana kwani kupitia Yeye Mwenyezi Mungu katupa bonge la ' Zawadi ' na hofu yangu tusipomuenzi nchi jirani zinaweza hata ' kumrubuni ' tu na kumpa Ulaji na Uraia wa kutukuka.
 
Nimepita Shule zote kuanzia za Saint, Academia na Kayumba za hapa jijini Dar es Salaam na hata ile mvua ya jana usiku imenikutia nikiwa mitaani nafanya hii ' tafiti ' ndogo tu Mkuu. Huyu Mama Watanzania tunatakiwa tumpe TUZO upesi sana kwani kupitia Yeye Mwenyezi Mungu katupa bonge la ' Zawadi ' na hofu yangu tusipomuenzi nchi jirani zinaweza hata ' kumrubuni ' tu na kumpa Ulaji na Uraia wa kutukuka.
Promo zingine bhana!!!
 
Back
Top Bottom